Ulijifunza kuendesha gari ukiwa na umri gani?

Ulijifunza kuendesha gari ukiwa na umri gani?

Kitu pekee watu wote wameweza endesha wakiwa na umri mdogo ni "kupoop kwa mcharazo"
 
Nilipelekwa Driving nilivomaliza form 4 kipindi nasubir matokeo ya Advance na Bamkubwa...Nimetoka bush kwenda kuish kwake watoto wake walikuwa ni wadogo kwangu ila walikuwa wanasukuma Cruza mkonga.
Bamkubwa ndio nani? Kwamba baba yako alikua na watoto kwa mke mwingine au
 
I was 22 yrs Old. Barabara ya mafunzo ilikuwa Sam Nujoma ,from Ubungo kuja mpaka mwenge , Sinza at that time.

Sijajua kwanini mwalimu alipendekeza hii route lakini naamini ilikuwa katika kupata uzoefu wa kuhandle kashikashi za mji, foleni n.k.

I thank him, was a best teacher Ever!
 
Kuna dogo nilikua namfundisha kuendesha gari mtaani mbona nilikoma.

Kuna sehemu tulipita mtaani kwao, njia haikua nzuri kwa mtu anaejifunza, hivyo nikamwambia twende tukazungukie mbele.

Kumbe pale kwenye njia mbovu kuna masela wake na yeye anataka awaonyeshe anajua gari, si akakunja kona ghafra palepale.(mmmk)

Sasa namuuliza unafanya nini na mie ticha nimekukataza usipite hapa tayari akaingia panic mode, akakanyaga wese mpaka kibati, gari yenyewe cresta gx 110 mpyaaa, alooooooo!!! Ni kama ilipaa mzee kuja kustuka tupo sebuleni kwa mtu.

Pua yooote ya gari ipo sebuleni, tumekuta jamaa anaangalia TV.

Sema katika moja na mbili jamaa alikua muelewa akasema nimjengee tu pale nilipovunja, nikaita mafundi tukalimaliza kiume, vijumba vyenyewe vile vya kota vimechakaa.
 
Kuna dogo nilikua namfundisha kuendesha gari mtaani mbona nilikoma.

Kuna sehemu tulipita mtaani kwao, njia haikua nzuri kwa mtu anaejifunza, hivyo nikamwambia twende tukazungukie mbele.

Kumbe pale kwenye njia mbovu kuna masela wake na yeye anataka awaonyeshe anajua gari, si akakunja kona ghafra palepale.(mmmk)

Sasa namuuliza unafanya nini na mie ticha nimekukataza usipite hapa tayari akaingia panic mode, akakanyaga wese mpaka kibati, gari yenyewe gx 110 mpyaaa, alooooooo!!! Ni kama ilipaa mzee kuja kustuka tupo sebuleni kwa mtu.

Pua yooote ya gari ipo sebuleni, tumekuta jamaa anaangalia TV.

Sema katika moja na mbili jamaa alikua muelewa akasema nimjengee tu pale nilipovunja, nikaita mafundi tukalimaliza kiume, vijumba vyenyewe vile vya kota vimechakaa.
Gx ipi? Landcruiser version au
 
Wazee wa magomeni na sinza nadhani mnamfahamu jamaa anafundisha gari huku amening'iniza bakora nje ya dirisha 😂😂 nimesahau jina la hiyo driving school
 
Back
Top Bottom