Kuna dogo nilikua namfundisha kuendesha gari mtaani mbona nilikoma.
Kuna sehemu tulipita mtaani kwao, njia haikua nzuri kwa mtu anaejifunza, hivyo nikamwambia twende tukazungukie mbele.
Kumbe pale kwenye njia mbovu kuna masela wake na yeye anataka awaonyeshe anajua gari, si akakunja kona ghafra palepale.(mmmk)
Sasa namuuliza unafanya nini na mie ticha nimekukataza usipite hapa tayari akaingia panic mode, akakanyaga wese mpaka kibati, gari yenyewe cresta gx 110 mpyaaa, alooooooo!!! Ni kama ilipaa mzee kuja kustuka tupo sebuleni kwa mtu.
Pua yooote ya gari ipo sebuleni, tumekuta jamaa anaangalia TV.
Sema katika moja na mbili jamaa alikua muelewa akasema nimjengee tu pale nilipovunja, nikaita mafundi tukalimaliza kiume, vijumba vyenyewe vile vya kota vimechakaa.