Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Of course tuliendelea kuongeza wengine, maana Wazee tulipokuwa Edeni tulipewa maagizo kwenda kuzaa na kuijaza Dunia 🤗🏋️

Binafsi sikupata changamoto zozote kwani nilijiandaa kuwa Baba Kwa muda mrefu

Na binafsi napenda watoto, hata sasa pamoja na kuzeeka 😜

Nashauri Vijana kabla hamjawa Wazazi(Kuwa Baba/Mama) hakikisheni mmejiandaa Kwa hilo

Binafsi sipendi kuona watoto wakiteseka mitaani Kwa kukosa huduma wakati tunajua fika kwamba Kuna watu wawili walijificha sehemu wakakubaliana kuvuana nguo ili kuwatafuta hao watoto (unless otherwise)

Suala la kubambikiwa watoto lipo kwenye jamii zetu, japo miaka ya hivi karibuni limeanza kuwa sugu baada ya Wasichana wengi kuwageuza watoto kitega Uchumi. Wengi huwafungulia Kadi mbili mbili Kwa mtoto mmoja, hivyo akija Kwa Mzee Grahams natoa Hela ya matunzo ya mtoto na akienda Kwa Kijana mwenzie apewe tena hela za matunzo Kwa mtoto huyo huyo mmoja

Binafsi nina njia zangu za kuweza kujua mtoto niliyepata Kwa Mpenzi/Mke wangu ni wangu kweli ama nilibambikiwa 😜
Hahaha, hebu nipe hizo mbinu we mzee.
Huenda zika nifaa siku za karibuni😁
 
una ushauri upi kwa vijana wanao elekea huko??.(Hasa sisi wanaume).

hebu tuambie suala zima la kuwa baba likoje??!.
Kama ilivyo raha kuwa mzazi hasa kwa mara ya kwanza basi inapaswa kuelewa kuna karaha pia. Baada ya mama kujifungua huo ndio mwanzo hasa wa challenge yenyewe.

Kuna kukesha usiku mzima sababu mtoto analia, kuna mtoto kuumwa usijue hata umsaidie vipi, kuna kununiana na mwenza wako sababu ya stress ya ulezi. Ila hii yote ni sehemu ya kuwa baba na kufuzu hasa katika hili ni kukubaliana na kila linalokuja mbele yako.

Umeuliza swala la kuwa baba likoje kwangu. Ni hisia iliyo bora kuliko kitu kingine chochote. Nina watoto 4 sasa, hakuna faraja kubwa ninayopata kama kurudi tu nyumbani na kusikia zile kelele za kushangiliwa nimerudi nyumbani, hakuna raha kama kupewa kesi baina yao wenyewe ya kuwa huyu kanipiga, huyu kanifinya.

Kadri umri unavyokwenda nahisi na enjoy zaidi swala la kuwa baba. Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa na kipaumbele kwangu kama vile kutoka na marafiki weekends. Lakini leo hii kila weekend asilimia kubwa nipo na watoto wangu. Ni faraja kubwa kukaa sebuleni ukasikia watoto wako wana discuss baina yao kuwa kesho Jumamosi baba haendi kazini na furaha wanayokuwa nayo kujua kuwa mtakuwa wote.

Ile hali ya kujua kuwa kwa vitu vidogo unathaminiwa na viumbe wengine ni furaha kubwa mno maishani. Leo hii ukisikia watoto wako wanajivunia kuwa nitamwambia baba yangu pale wanapokerwa na kitu/mtu wakiamini you have some kind of super powers ni hisia ambayo haimithiliki na chochote kile.

Ukiniambia leo nibadilishe chochote katika kuwa kwangu baba basi hakika sina ambalo nitakalo libadilike. Na maudhi yao yote ila faraja ya watoto haiwezi fanya nitake utofauti wowote.
 
Hahaha, hebu nipe hizo mbinu we mzee.
Huenda zika nifaa siku za karibuni😁
Ukifanikiwa kuwa Baba utanishtua nikupe hizo mbinu

Ila tafadhali, usije kumdhuru mtoto ukijua sio wako

Maana hadi unapewa mtoto na Mwanamke ina maana ulifanikiwa kumwagia ndani 😜 kwahiyo hata akifanana na wewe pua inatosha sana 😜🏃🏃
 
Ukifanikiwa kuwa Baba utanishtua nikupe hizo mbinu

Ila tafadhali, usije kumdhuru mtoto ukijua sio wako

Maana hadi unapewa mtoto na Mwanamke ina maana ulifanikiwa kumwagia ndani 😜 kwahiyo hata akifanana na wewe pua inatosha sana 😜🏃🏃
Wewe Tena mbinu, masuala ya nta kufundisha. Baadae.
Yasije kuta Nisha pewa limbwata🤣😂.

Halafu hizo pigo za kitanda haki zao haramu, yaishie huko daslam 😂😂
 
Ukifanikiwa kuwa Baba utanishtua nikupe hizo mbinu

Ila tafadhali, usije kumdhuru mtoto ukijua sio wako

Maana hadi unapewa mtoto na Mwanamke ina maana ulifanikiwa kumwagia ndani 😜 kwahiyo hata akifanana na wewe pua inatosha sana 😜🏃🏃
Wakati wadogo huwa sura zinabadilika badilika mwanagu had saiz ashafanan na watu watatu 😆😆
 
Hongera Sana mkuu, ulicho andika kina onesha furaha yako kwa kiasi Kikubwa.

Vipi changamoto mlizo kumbana nazo, kabla na baada ya kupata mtoto??.

Uli jisikiaje baada ya kupewa taarifa, kuwa wewe ni baba mtarajiwa?!.

Una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala Hilo la uzazi, hasa Kwa sisi wanaume.
Changamoto ndio nilikua nimeanza kazi na kama miaka miwili hivi nilikua na uhaba sana na fedha na vitu vingi sana nilikua nimeandika kwenye diary na kwenye simu mpaka chumba chake tayari nilikuwa nishapanga kitakuaje ila nilijitahidi kufanya vichache nilivyoweza.
Baada ya kuzaliwa changamoto ilikuwa kwa wasaidizi wa kazi walikua hawadumu ,mwanamke wangu ana kakisirani pili dogo mpaka leo hapendi msosi mpaka aone watoto wengine au mimi niwepo nimetia sura ya kikauzu.Lishe yake huyu mwanamke ilikua inamshinda kuandaa ikabidi niingie front kujifundisha( hapa kwenyewe nishaanika ngano ,karanga ,ulezi ushasafishwa nimeuanika😄😄).Kwa swala la afya yake sijawahi kupata tatizo serious ni magonjwa ya madogo madogo tu.
Kingine mkuu wangu kuna vitu nilikuwa sisikilizi na naona miyeyusho tu ,kwa sasa inabidi kusikiliza ,kupay attention kweri kweri mfano siku yake ya kuzaliwa unaletewa budget na inabidi ukubaliane nayo na uwepo.Angalizo usilete kiumbe duniani kama huna pakushika kwani mara ya kwanza kulipa ada yake na usafiri wa shule kidogo kichwa kipasuke kama bisi.
 
Ohh pole na hongera mkuu, vipi kuhusu changamoto zozote kabla na baada ya kuji fungua ??.

Shemeji yetu Ali semaje, Baada ya wewe kumpa taarifa.
asante sana,, changamoto ni io tu uzaz wa kwanza kuto kujielewa mambo tayar m nkabaki nmezubaa ikabid operation,,ila baada ya apo n usumbufu tu wa kawaida wa watoto.

Shemej alikenua tu meno😁
 
Wakati wadogo huwa sura zinabadilika badilika mwanagu had saiz ashafanan na watu watatu 😆😆
Ni kweli Mkuu

Hata akifanana na wewe pua Kwa wiki mbili then akaenda kufanana na mtu mwingine inatosha. Muhimu ukumbuke kumpiga picha pindi anapokuwa amefanana na wewe hiyo pua wakati wa transition for the future use 😜

Kiasili mtoto ni wa Mama, sisi WaBaba tunafanya kupewa tu 😜

Kwahiyo usishangae Mama yupo DSM, alafu mtoto akapewa Mzee Grahams ambaye yupo Nanjilinji huko, kumbe aliwahi kumwagia ndani 🙌🏃🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom