Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Mm sipendi matoto matundu of course siyapendagi matoto tundu😊
Muulize mama au mlezi wako kama yupo bado ikiwa ulikuwaga mtundu? Kama ndivyo mtoto wako atakuwa *100 😂

Kakaangu wanae ni watundu kinoma, huwa kuna muda anakasirika sana, mama yetu humwambia weeee tena kaa kimya, maana yeye ndio alikuwa balaa 🤣 ila wanae ndio hatari na nusu.
 
Nilikuwa na hofu sana lakini uzuri mama wa huyu mwanamke wangu alikuwepo.Nilikuwa kwenye kibar karibu karibu tu na hospitali.Hiyo hisia ya kuwa baba sijui hata niifananishe na nini.
Kuhusu malezi namlea binti yangu kwa namna mimi baba yake naona inafaa.Kwenye kila moments za maisha yake nipo na ntakuepo,elimu ameshaanza kupata ya uhakika,viboko sitaki kusikia kabisa na ole wake mtu aje athubutu kumchapa mwanangu.Atakachotaka kuwa mimi ntamsapoti asilimia 100.Kuhusu jina mama yake alikuwa anataka aitwe Gianna mimi nikaongeza na la kikwetu/kikabila .Vipaumbele na mipango sasa vinafanyika kumzunguka yeye kwanza ndio wengine wanafuata.Usikue bi mzuri wangu natamani uendeelee kuwa mtoto hivi hivi milele.
 
Nilitawaliwa na wasiwasi Je nitazaa salama , mwanangu atakuwa Hai , atafananaje na nitakuwa mama Kweli, nitaweza hekaheka za Leba kila siku zikisonga mawazo yalizidi

Mwishowe 😅😅 nikatoboa Raha sanaa.
Kwa maneno haya, it means uli toboa mkuu😊.
Una ushauri upi kwa mabinti wanao elekea huko, yapi waji funze na yapi waya epuke.
 
Nilikuwa na hofu sana lakini uzuri mama wa huyu mwanamke wangu alikuwepo.Nilikuwa kwenye kibar karibu karibu tu na hospitali.Hiyo hisia ya kuwa baba sijui hata niifananishe na nini.
Kuhusu malezi namlea binti yangu kwa namna mimi baba yake naona inafaa.Kwenye kila moments za maisha yake nipo na ntakuepo,elimu ameshaanza kupata ya uhakika,viboko sitaki kusikia kabisa na ole wake mtu aje athubutu kumchapa mwanangu.Atakachotaka kuwa mimi ntamsapoti asilimia 100.Kuhusu jina mama yake alikuwa anataka aitwe Gianna mimi nikaongeza na la kikwetu/kikabila .Vipaumbele na mipango sasa vinafanyika kumzunguka yeye kwanza ndio wengine wanafuata.Usikue bi mzuri wangu natamani uendeelee kuwa mtoto hivi hivi milele.
Hongera Sana mkuu, ulicho andika kina onesha furaha yako kwa kiasi Kikubwa.

Vipi changamoto mlizo kumbana nazo, kabla na baada ya kupata mtoto??.

Uli jisikiaje baada ya kupewa taarifa, kuwa wewe ni baba mtarajiwa?!.

Una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala Hilo la uzazi, hasa Kwa sisi wanaume.
 
nina week mbili toka toka mwanangu azaliwe tarh 04/04, ila nafikir reality ya sasa nmekuwa baba haijanipata vizur bado nina mawenge kuna mda siamin kama tayari ni baba, sielewi ni uoga, furaha au naona kawaida tu au sababu mambo ni mengi!

Sielewi lolote nipo tu!!
 
Hahaha, hongera kwako mkuu. Hop e mli tengeneza wengine😁.
Vipi Kuhusu changamoto Mlizo kumbana nazo mkubwa??.

una ushauri upi kwa vijana kuhusu suala Zina la uzazi, hasa Kwa sisi wanaume!?.

vipi kuhusu kubambikiziwa, Kuna precaution gani za kuchukua 😁
Of course tuliendelea kuongeza wengine, maana Wazee tulipokuwa Edeni tulipewa maagizo kwenda kuzaa na kuijaza Dunia 🤗🏋️

Binafsi sikupata changamoto zozote kwani nilijiandaa kuwa Baba Kwa muda mrefu

Na binafsi napenda watoto, hata sasa pamoja na kuzeeka 😜

Nashauri Vijana kabla hamjawa Wazazi(Kuwa Baba/Mama) hakikisheni mmejiandaa Kwa hilo

Binafsi sipendi kuona watoto wakiteseka mitaani Kwa kukosa huduma wakati tunajua fika kwamba Kuna watu wawili walijificha sehemu wakakubaliana kuvuana nguo ili kuwatafuta hao watoto (unless otherwise)

Suala la kubambikiwa watoto lipo kwenye jamii zetu, japo miaka ya hivi karibuni limeanza kuwa sugu baada ya Wasichana wengi kuwageuza watoto kitega Uchumi. Wengi huwafungulia Kadi mbili mbili Kwa mtoto mmoja, hivyo akija Kwa Mzee Grahams natoa Hela ya matunzo ya mtoto na akienda Kwa Kijana mwenzie apewe tena hela za matunzo Kwa mtoto huyo huyo mmoja

Binafsi nina njia zangu za kuweza kujua mtoto niliyepata Kwa Mpenzi/Mke wangu ni wangu kweli ama nilibambikiwa 😜
 
nina week mbili toka toka mwanangu azaliwe tarh 04/04, ila nafikir reality ya sasa nmekuwa baba haijanipata vizur bado nina mawenge kuna mda siamin kama tayari ni baba, sielewi ni uoga, furaha au naona kawaida tu au sababu mambo ni mengi!

Sielewi lolote nipo tu!!
Maybe talk with your parents, itakuwa Kuna kitu kina miss labda.
Take a vacation na familia, ili mchill ita saidia mkuu.
 
Kwa maneno haya, it means uli toboa mkuu😊.
Una ushauri upi kwa mabinti wanao elekea huko, yapi waji funze na yapi waya epuke.
Nilitoboa vizuri Sana , Wasikurupuke kubeba Mimba , hasa Sisi wanawake ukishaingia kwenye ulezi binafsi nawekaga miaka 3 hii nikulea tu ata baadhi ya shughuli za uchumi zinazohitaji Muda wako zinaweza zikasimama.
 
Vipi kuhusu shemeji yetu Baada ya kuona taarifa hizo.
Ali furahi au ndo mshituko wa ghafla 😁
 
Back
Top Bottom