Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?

Hongera Sana mkuu, vipi kuhusu changamoto zozote mlizo kumbana nazo??.
Iwe kabla au Baada ya kupata mtoto.

Una ushauri upi kwa vijana, kuhusu suala Hilo la uzazi??
Changamoto zilikuwa nyingi sana.Ukizingatia mke wangu wazazi wake wote nikimaanisha baba na Mama ni wanasheria haswa.
Ila niseme tu mwanamke alikuwa muelewa na mimi nilikuwa muelewa.

Pili, nimempata katika wakati bado nina umri ambao wengi hawafikirii. Mke wangu alipopata mimba kwa % kubwa alifanya akili yangu ifanye kazi sana. Nilikuwa nafikiria ni namna gani ninalea Hicho kiumbe. Ukilinganisha uwezo wa kwao na kwetu kwao wana uwezo mkubwa sana kipesa lakini hakuwahi hata siku moja kuonyesha dharau.

Kingine alikuwa anapenda kunywa maji ya uhai ya chupa. Hapa nilikuwa natamani nimpige. Na lazima ukirudi urudi na udongo wa kula. Mpaka anakuja kujifungua zile chupa za maji nilikuwa naweza fungua kiwanda.

Kingine ni mara ya kwanza hivyo alikuwa anakasirika mda wowote. Ilinipa shida sana. Anaweza akakasirika au akakujibu vbaya baadae anakupigia simu Babe nimekumiss sana na huu usiku nataka kuwa kwenye mikono yako. Hakuna namna narudi.

Moment ni nyingi sana😂❤️ Huwa tukikaa tunafurahi na kukumbushana.
 
Wewe Tena mbinu, masuala ya nta kufundisha. Baadae.
Yasije kuta Nisha pewa limbwata🤣😂.

Halafu hizo pigo za kitanda haki zao haramu, yaishie huko daslam 😂😂
Ukiishi hiyo slogan kwamba Kitanda hakizai haramu hautapata tabu ya kwenda kuwapima DNA watoto wako na Mkeo, kama Sisi Wazee tunavyofanya

We ukipewa Sema hewara tu 😜😅
 
Nilipata mtoto wangu wa kwanza nikiwa na miaka 17, kiukwrli nilikuwa na hisia mchanganyiko.
-Nilikua naogopa yet sijui naogopa nini
-Nilikuwa nina aibu as nilijiona dah, mi ndo naonekana muhuni mtaani
-Nilikuwa na majuto as niliona nimeaibisha walezi wangu as baba na mama walikwishafariki
-Nilikuwa nina hasira as nilijua sitasoma tena
-Nilikuwa ninahamu ya kumuona mwanangu as nilihisi atakuwa kama kamdoli
-Nilikuwa ninawivu as nilijua boyfrien wangu angeniacha
Yani tu kwa ujumla nilikuwa na sintofahamu kibao.
Binti yangu sasa ana miaka 26.
Leo hii ukiniuliza nitakwambia yafuatayo
KUTUNZA MIMBA NA KUKUBALI KUWA MAMA KWA UMRI ULE, ILIKUWA NI UAMUZI THE BEST NILIWAHI KUFANYA KWENYE MAISHA YANGU!
 
Ukiishi hiyo slogan kwamba Kitanda hakizai haramu hautapata tabu ya kwenda kuwapima DNA watoto wako na Mkeo, kama Sisi Wazee tunavyofanya

We ukipewa Sema hewara tu 😜😅
Wee Kuna Jamaa Ali pata mtoto, kalea kuanzia mimba Hadi mtoto kaja.
Halafu binti ana mwambia sio wake, Jamaa Ali sepa na mtoto aisee🤣😂.

Mbona wali rudisha mizigo ya jamaa×3
 
Nilikuwa na mixed feelings, shauku na uoga.

Nilipata bahati ya kuwepo mtoto alipokuwa anazaliwa na kupata fursa ya kumbeba alipofutwa tu. Kwa mara ya kwanza nadhani nilitokwa na machozi ya furaha, yani nilijikuta machozi tu yananitoka.

Ilikuwa ni hisia nzuri mno.

Hakuna mtu yeyote anaeweza kukufundisha jinsi ya kuwa mzazi bora, just be the best you can be kwa kuwepo katika kila hatua ya ujauzito mpaka kujifungua kwa mzazi mwenzio. Kumbuka kila kitu kwako ni kipya hivyo ni sawa kuwa na hofu na uoga.

Funzo pekee ambalo nahisi ni muhimu ni kupanga na mwenzi wako kupata mtoto, nahisi hapo utaenjoy zaidi process yote mpaka mtoto kuzaliwa.

Hongera sana kiongozi
 
Nilipata mtoto wangu wa kwanza nikiwa na miaka 17, kiukwrli nilikuwa na hisia mchanganyiko.
-Nilikua naogopa yet sijui naogopa nini
-Nilikuwa nina aibu as nilijiona dah, mi ndo naonekana muhuni mtaani
-Nilikuwa na majuto as niliona nimeaibisha walezi wangu as baba na mama walikwishafariki
-Nilikuwa nina hasira as nilijua sitasoma tena
-Nilikuwa ninahamu ya kumuona mwanangu as nilihisi atakuwa kama kamdoli
-Nilikuwa ninawivu as nilijua boyfrien wangu angeniacha
Yani tu kwa ujumla nilikuwa na sintofahamu kibao.
Binti yangu sasa ana miaka 26.
Leo hii ukiniuliza nitakwambia yafuatayo
KUTUNZA MIMBA NA KUKUBALI KUWA MAMA KWA UMRI ULE, ILIKUWA NI UAMUZI THE BEST NILIWAHI KUFANYA KWENYE MAISHA YANGU!
nimeipenda hii
 
Kama ilivyo raha kuwa mzazi hasa kwa mara ya kwanza basi inapaswa kuelewa kuna karaha pia. Baada ya mama kujifungua huo ndio mwanzo hasa wa challenge yenyewe.

Kuna kukesha usiku mzima sababu mtoto analia, kuna mtoto kuumwa usijue hata umsaidie vipi, kuna kununiana na mwenza wako sababu ya stress ya ulezi. Ila hii yote ni sehemu ya kuwa baba na kufuzu hasa katika hili ni kukubaliana na kila linalokuja mbele yako.

Umeuliza swala la kuwa baba likoje kwangu. Ni hisia iliyo bora kuliko kitu kingine chochote. Nina watoto 4 sasa, hakuna faraja kubwa ninayopata kama kurudi tu nyumbani na kusikia zile kelele za kushangiliwa nimerudi nyumbani, hakuna raha kama kupewa kesi baina yao wenyewe ya kuwa huyu kanipiga, huyu kanifinya.

Kadri umri unavyokwenda nahisi na enjoy zaidi swala la kuwa baba. Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa na kipaumbele kwangu kama vile kutoka na marafiki weekends. Lakini leo hii kila weekend asilimia kubwa nipo na watoto wangu. Ni faraja kubwa kukaa sebuleni ukasikia watoto wako wana discuss baina yao kuwa kesho Jumamosi baba haendi kazini na furaha wanayokuwa nayo kujua kuwa mtakuwa wote.

Ile hali ya kujua kuwa kwa vitu vidogo unathaminiwa na viumbe wengine ni furaha kubwa mno maishani. Leo hii ukisikia watoto wako wanajivunia kuwa nitamwambia baba yangu pale wanapokerwa na kitu/mtu wakiamini you have some kind of super powers ni hisia ambayo haimithiliki na chochote kile.

Ukiniambia leo nibadilishe chochote katika kuwa kwangu baba basi hakika sina ambalo nitakalo libadilike. Na maudhi yao yote ila faraja ya watoto haiwezi fanya nitake utofauti wowote.
Hongera Sana mkuu, na Niku pongeze Kwa kusimamia kidete kujenga familia Bora.
Asante Kwa ushauri mzuri 🙏
 
Nilipata mtoto wangu wa kwanza nikiwa na miaka 17, kiukwrli nilikuwa na hisia mchanganyiko.
-Nilikua naogopa yet sijui naogopa nini
-Nilikuwa nina aibu as nilijiona dah, mi ndo naonekana muhuni mtaani
-Nilikuwa na majuto as niliona nimeaibisha walezi wangu as baba na mama walikwishafariki
-Nilikuwa nina hasira as nilijua sitasoma tena
-Nilikuwa ninahamu ya kumuona mwanangu as nilihisi atakuwa kama kamdoli
-Nilikuwa ninawivu as nilijua boyfrien wangu angeniacha
Yani tu kwa ujumla nilikuwa na sintofahamu kibao.
Binti yangu sasa ana miaka 26.
Leo hii ukiniuliza nitakwambia yafuatayo
KUTUNZA MIMBA NA KUKUBALI KUWA MAMA KWA UMRI ULE, ILIKUWA NI UAMUZI THE BEST NILIWAHI KUFANYA KWENYE MAISHA YANGU!
Hongera mkuu😍, unaitwa mama nani ety🤣
 
Back
Top Bottom