Kama ilivyo raha kuwa mzazi hasa kwa mara ya kwanza basi inapaswa kuelewa kuna karaha pia. Baada ya mama kujifungua huo ndio mwanzo hasa wa challenge yenyewe.
Kuna kukesha usiku mzima sababu mtoto analia, kuna mtoto kuumwa usijue hata umsaidie vipi, kuna kununiana na mwenza wako sababu ya stress ya ulezi. Ila hii yote ni sehemu ya kuwa baba na kufuzu hasa katika hili ni kukubaliana na kila linalokuja mbele yako.
Umeuliza swala la kuwa baba likoje kwangu. Ni hisia iliyo bora kuliko kitu kingine chochote. Nina watoto 4 sasa, hakuna faraja kubwa ninayopata kama kurudi tu nyumbani na kusikia zile kelele za kushangiliwa nimerudi nyumbani, hakuna raha kama kupewa kesi baina yao wenyewe ya kuwa huyu kanipiga, huyu kanifinya.
Kadri umri unavyokwenda nahisi na enjoy zaidi swala la kuwa baba. Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa na kipaumbele kwangu kama vile kutoka na marafiki weekends. Lakini leo hii kila weekend asilimia kubwa nipo na watoto wangu. Ni faraja kubwa kukaa sebuleni ukasikia watoto wako wana discuss baina yao kuwa kesho Jumamosi baba haendi kazini na furaha wanayokuwa nayo kujua kuwa mtakuwa wote.
Ile hali ya kujua kuwa kwa vitu vidogo unathaminiwa na viumbe wengine ni furaha kubwa mno maishani. Leo hii ukisikia watoto wako wanajivunia kuwa nitamwambia baba yangu pale wanapokerwa na kitu/mtu wakiamini you have some kind of super powers ni hisia ambayo haimithiliki na chochote kile.
Ukiniambia leo nibadilishe chochote katika kuwa kwangu baba basi hakika sina ambalo nitakalo libadilike. Na maudhi yao yote ila faraja ya watoto haiwezi fanya nitake utofauti wowote.