binafsi nilifurahi sana, hasa baada ya kukaa miaka mingi kwenye ndoa bila kupata mtoto, hakika nilimshukuru Mungu aliyeniona hata mimi akanifanya niwe na uzao. Mimi na mke wangu tuliteseka sana, tulitukanwa sana, mke wangu alitukanwa matusi yote, na ndugu zangu hata majirani. kuna siku mtoto wa jirani alifanya kimbwanga akamkemea kama mzazi, mamake akaja akamwambia wazazi tuzae wagumbe muleee, imagine unaambiwa hivyo ukiwa kwenye jaribu la kutafuta mtoto. ninachoshukuru Mungu sikwenda kwa mganga wa kienyeji na sikunywa dawa za kienyeji, tulikubaliana na mke wangu kwamba tutapata watoto wa baraka toka kwa Mungu ama la kama tunabaki hivi tutazeeka hivihivi. SISEMI HIVI ILI KUWAHUKUMU WALIOTELEZA NA KWENDA KWA WAGANGA, No, bado mnayo nafasi ya kutubu, mkamwambia Mungu tumeenda kwa waganga hawajatusaidie, tunarudi kwako tunaomba utusaidie, yeye atawasamehe na atajitwalia utukufu.
naandika hivi ili kuwashauri wanaotafuta watoto, msipoteze muda kwa waganga, mwaminini Mungu.
katika siku tusiyodhania, tukiwa tumekata tamaa tumefika mwisho, Ndipo Mungu alianzia. ile line wewe unafika mwisho wa harakati zako zote hapo ndipo Mungu huwa anatake over na kuanza. ghafla, mke wangu akaanza kujisikia vibaya. nilinunua pregrancy test zaidi ya sita, na kwenda hospitali kadhaa wa kadhaa, nilipima PT zote zikaonyesha mistari ya mimba ila nilikuwa siamini. kumbuka mimi nilikuwa nazijua sana PT kwasababu miaka mingi kila mke wangu akipitisha period nilikuwa napima nione imenasa kumbe bado. tulipima kote wakasema ana mimba, sikuamini bado, nilikuja kuamini nilipoona tumbo limeanza kuwa kubwa na anakataa vyakula kadhaa. hadi anajifungua. KILICHOPO SASAIVI, TUMEPATA WATOTO WENGI HADI TUNAPAMBANA KUZUIA MIMBA ama la inaingia anytime. wale waliokuwa wanatafuta mimba Mungu amebadilisha kibao wanapambana kuzuia mimba. Sifa na utukufu kwa Mungu.
KAMA UNAPITA KWENYE JARIBU LA KUPATA MTOTO, ZINGATIA MISTARI HII, IAMINI, UTAPATA WATOTO, MISTARI HII NDIYO TULIKUWA TUNAIPITIA NA KUIAMINI HADI MUNGU AKATUPATIA WATOTO.
Mwanzo 1 :28, Mungu akawabarikia akisema, zaeni mkaongezeka mkaitiishe nchi.
Zaburi 127 :3, watoto ni zawadi toka kwa Bwana.
Mwanzo 9:1,7, Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, zaeni mkaongezeke. We are the remnants of Noah, we are the survivors of the flood and God blessed us to go and multiply.
Walawi 26: 9, kama tukiyashika maagizo ya Mungu, ataongeza uzao wetu. Tutakuwa na uzazi mwingi, na Mungu atalithibitisha hili agano lake analoliweka nasi kwetu.
Zaburi 128:3, yeyote amchaye Bwana, mkewe atakuwa kama mzabibu uzaao nyumbani mwake. Wanawe watachipua kama miche ya mizeituni wakiizunguka meza yake.
Mwanzo 33:5, Yakobo aliinua macho akaona watoto wa Esau, Esau akasema hawa ndio watoto ambao Mungu alimpa kwa neema yake. Mungu wetu ni wa neema na rehema, anatoaga watoto. Bado anayo neema ya kuwapa watu watoto hata leo hivi, kwasababu yeye ni yeye yule jana leo na hata milele. Habadiliki.
Mwanzo 17:6-7, Mungu alimwambia Ibrahim, Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa na wafalme watatoka kwako. Agano hili alilifanya kuwa kwa vizazi vyake vyote. Kitabu cha Wagalatia 3:6-9 kinasema ya kuwa, sisi tu warithi wa ahadi na baraka zote za Ibrahimu.
2wafalme 13:23, Mungu aliwaangalia wana wa Israel, akawasikitikia, akalikumbuka agano aliloliweka pamoja na ibrahim. Mungu huliangalia Neno lake apate kulitimiza. Neno lake linaweza kutimizwa, lazima litatimizwa kwa mtu yeyote anayeamini. Kama Mungu katika Neno lake anasema kuwa watoto hutoka kwake, na hawatoki kwa mganga wa kienyeji wala kwa miungu iwayo yote, basi, ukidai ahadi hii kwa Mungu atakupa watoto. Ijulikane kuwa, Mungu anao uwezo wa kutoa au kutokutoa watoto kwa watu. Mungu ni juu ya yote, akisema ndiyo hakuna wa kusema hapana, akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo. Hata kama waganga wa kinyeji au wachawi walikuharibu kimazingara usizae, au manuizo ya kiuchawi ya namna yoyote ile, Mungu ana nguvu kuliko wachawi na waganga wa kienyeji. Anaweza akakuponya na utapata watoto. Uwezo huo Mungu anao. Yeye ndiye aliyeumba mbingu na dunia, aliumba mwanadamu pia. Hivyo, hata kama wachawi au shetani amekudhuru, au hata kama dhambi imekudhuru kabisa, imeharibu kizazi mamba inaporomoka, imeng’ofoa kizazi kimazingara ili wakafanyie biashara, hauendi hedhi, hauna nguvu za kiume n.k, Mungu anaweza akakuumba upya, uwezo huo Mungu wetu anao, anaweza akakuumba upya na ukawa mzima na kutimiza yote unayotaka, na watoto utapata, maadamu tu unamtumainia Bwana peke yake, hautumainii miungu mingine, hautumainii wachawi,waganga na wasoma nyota. Wamtumainio Bwana ni kama mlima sayuni, hawatatikisika milele, mtumaini Bwana ukatende mema, ukae katika nchi upendezwe na uaminifu, nawe utajifurahisha mbele za Bwana,naye atakupa haja za moyo wako.Amina.