Nilikosea kutokuwa serious na elimu pia kufata passion badala ya uhalisia
Kipindi nipo shule sikuwa makini na elimu, nilijiamini nina akili hivyo kwa vyovyote vile nitafaulu tu, na cha ziada niliona hakuna maajabu yoyote kwani hata waliofaulu sana wengi wanasota mtaani kusaka ajira, hivyo nikawa sio mhudhuriaji mzuri wa darasani n.k
Hii ilipelekea kuja kupata matokeo ya kawaida sana 4m4 na 6, ilhali ningeweza kupasua vizuri sana
Cha pili, baada ya kumaliza 4m6 nikaamua kuweka shule pembeni na kufata "passion" nisake hela na kutimiza ndoto zangu za tangu utotoni, wengi wanasema hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu unachopenda
Kuna ukweli ndani yake, lakini unaweza kukutana na stress hizo usiweze amini kwani kitu nilichoamua kufanya kilinipa stress (ilikuwa masuala ya sanaa) coz ili kutoboa ilinipasa kulamba watu miguu (kitu ambacho kamwe sitokaa kufanya) , kujipendekeza kwa watu wa media, kuwekeza fedha nyingi halafu output ndogo, kuishi maisha ambayo sio yangu n.k
Japo ilinifanya nifahamiane na watu wengi na hata kupata heshima mtaani lakini kiuhalisia sikuingiza hela yoyote ya maana na umri ulikuwa unasogea tu. . .
Baada ya miaka takribani nane ndio nikarudi tena shule kutafuta degree, wakati huo niliosoma nao tayari wana degree zao na wengine washapata kazi kabisa mimi napuyanga tu, hata kukutana nao naona aibu
Kozi niliyopanga kuisoma kipindi kile haikuwezekana kwa sasa ikabidi nichague kozi moja ambayo ilikuwa the only option na kila mtu aliiona ya ajabu ( ndugu zangu wengi wasomi kuna baadhi ya kozi ukitaja wanakuona looser sana ) hivyo nikachukuliwa kama mtu aliepoteza dira na nikasemwa sababu nilikacha shule
Ona Mungu alivyo wa ajabu sasa, kozi hiyo ilikuwa m'baraka mkubwa kwangu kwani nilianza kupata mishe bado nipo chuo na hata baada ya kumaliza, nilisota kidogo tu mtaani kisha nikapata kazi ambayo imenipa maslahi makubwa ambayo hata ndugu zangu wanashangaa inakuwaje nimeanza na scale kubwa hiyo
ni Mungu tu alinipigania, funzo nililopata kamwe usichezee elimu na pia kamwe usifate au uamue kitu kisa unakipenda bali fuata uhalisia
Ni bora mara 100 ufanye kitu usichopenda ila ni halali, kina maslahi kwako na mchango kwa jamii kuliko kufata unachopenda halafu unasota na njaa