Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 6,958
- 16,358
Hili ndio linanifanya kila siku "Niwaze jinsi ya kuacha Kazi""Kufanya kazi za watu muda mrefu hadi usiku nakusahau kupambania ndoto zangu. Kumbe niligeuzwa ngazi ya kuwapandisha wengine badala ya kujituma kuboresha malengo yangu
Wewe ni nouma asee🙌Hahahahah
Kuoa hakuna ishu, ila kuzaaa NI SAWA.Kuchelewa kuoa. Then kuchelewa kuzaa
Binafsi siamini kwenye Uwekezaji wa Ardhi.Nikiwa bado shababy miaka Hi you Dodoma, 2008!, kazi, nyumba, niliwekewa mpaka house girl na mlinzi na kampuni, Sina mke, wala mtoto, mi Gym na muviii tu,
Badala ya kuwekeza kununua ardhi, nikanunua gari, la kutembelea tu!
Kampuni ilipokufa, nikapata kazi nyingine, maokoto kiduchu! Gari nikauza! Laiti ningenunua ardhi Leo ningrkua bilionea,
Kuna Dogo tulikuwa wote kazini, aliuza ardhi yake kwa bilioni 1.5 kwa nssf!
Sasa hv ana nyumba kama 10 hv!
Mie bado nachechemea! Hatsri Sana,
Wekeza kwanza keenye ardhi
Faculty au Course mzee baba, no wonder kwa sasa unauza nyanya...Nilikosea kuchukua faculty ya "BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION" instead of "TECHNICAL EDUCATION", Nna degree 3 kwa sas nauza nyanya Karatu.
Na hiv juzjuz hapa ROMA alinitag kwenye wimbo wake wa "MAUA YANGU"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umeongea kiutu uzima sana [emoji23]Sina ninachojutia. Kila nilichopitia kilikuwa daraja la kunifikisha nilipo hivi sasa.
Najitahidi kuwa bora, nisiwe kama nilikotoka.
Majuto yafaa nini ikiwa maisha ni sasa?
Anza kuishi sasa, achana na yaliyopita.
Ilitakiwa ukamae huko huko.Nilikosea kutokuwa serious na elimu pia kufata passion badala ya uhalisia
Kipindi nipo shule sikuwa makini na elimu, nilijiamini nina akili hivyo kwa vyovyote vile nitafaulu tu, na cha ziada niliona hakuna maajabu yoyote kwani hata waliofaulu sana wengi wanasota mtaani kusaka ajira, hivyo nikawa sio mhudhuriaji mzuri wa darasani n.k
Hii ilipelekea kuja kupata matokeo ya kawaida sana 4m4 na 6, ilhali ningeweza kupasua vizuri sana
Cha pili, baada ya kumaliza 4m6 nikaamua kuweka shule pembeni na kufata "passion" nisake hela na kutimiza ndoto zangu za tangu utotoni, wengi wanasema hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu unachopenda
Kuna ukweli ndani yake, lakini unaweza kukutana na stress hizo usiweze amini kwani kitu nilichoamua kufanya kilinipa stress (ilikuwa masuala ya sanaa) coz ili kutoboa ilinipasa kulamba watu miguu (kitu ambacho kamwe sitokaa kufanya) , kujipendekeza kwa watu wa media, kuwekeza fedha nyingi halafu output ndogo, kuishi maisha ambayo sio yangu n.k
Japo ilinifanya nifahamiane na watu wengi na hata kupata heshima mtaani lakini kiuhalisia sikuingiza hela yoyote ya maana na umri ulikuwa unasogea tu. . .
Baada ya miaka takribani nane ndio nikarudi tena shule kutafuta degree, wakati huo niliosoma nao tayari wana degree zao na wengine washapata kazi kabisa mimi napuyanga tu, hata kukutana nao naona aibu
Kozi niliyopanga kuisoma kipindi kile haikuwezekana kwa sasa ikabidi nichague kozi moja ambayo ilikuwa the only option na kila mtu aliiona ya ajabu ( ndugu zangu wengi wasomi kuna baadhi ya kozi ukitaja wanakuona looser sana ) hivyo nikachukuliwa kama mtu aliepoteza dira na nikasemwa sababu nilikacha shule
Ona Mungu alivyo wa ajabu sasa, kozi hiyo ilikuwa m'baraka mkubwa kwangu kwani nilianza kupata mishe bado nipo chuo na hata baada ya kumaliza, nilisota kidogo tu mtaani kisha nikapata kazi ambayo imenipa maslahi makubwa ambayo hata ndugu zangu wanashangaa inakuwaje nimeanza na scale kubwa hiyo
ni Mungu tu alinipigania, funzo nililopata kamwe usichezee elimu na pia kamwe usifate au uamue kitu kisa unakipenda bali fuata uhalisia
Ni bora mara 100 ufanye kitu usichopenda ila ni halali, kina maslahi kwako na mchango kwa jamii kuliko kufata unachopenda halafu unasota na njaa
Wengi wao kero sana ukimweka ndani, matako makubwa akili kiduchu.Kuoa mwanamke mwenye matako makubwa,..
Tuewekee hapa uenda ikasaidia mdau mwingine anaepita hapa kujifunza na kuepuka makosa.
Mimi nilikuwa na tabia ya kumuamini sana mtu hasa km amenipa ishara njema za kumuamini pale mwanzo.
Ila baada ya kulizwa sana hapo kati nimejifunza hautakiwi kumuamini mtu kwa 100% na usimuamini mtu wakati wote.
Kila mara hakikisha unakuwa makini na wanaokuzunguka.
We jamaa una madini sana mkuu... Uko vizuri mkuuIlitakiwa ukamae huko huko.
Kama umesoma kitabu cha Napolean hill na Kawasaki.
'The principle of persistence ' kuna sehemu Ndpolean kasema 'One meter from the Gold'
Unapokuwa una jambo ulilowekeza muda mwingi ni sawa mtu kuacha dhahabu one meter na kuuza shimo kwa mtu mwenigine halafu mda mfipi unasokia shimo limetema.
Saa wewe ulisha kusanya skill nyingi i sana ktk mziki sasa ulitakuwa utumie fursa zingine kwenye muziki badala ya kukacha.
Hata chuo ilitakiwa uendeleze fani yako ktk mlengo wa kisomi.
Shida kubwa ni kwamba tunakosa washauri na wasimamizi wazur.
Sanaa, michezo na siasa ya TZ imejengwa ktk mfumo wa kujuana juana.
Kwa hio ulitakiwa ujishushe ndio upate.
Hata makazini bila kuwa chawa chawa hupati cheo, seminar promotion nk.
Sisi waafrika ni watu wa hovyo hivi hapa duniani.
Usiiache talent yako hata kama umepata kazi. Talent ndio utajiri aliokupa mungu.
Mi nakushauri uongeze na elimu ya mziki au sanaa uifanye tofauti na mwanzo.
Digiital platform inasaidia sana hata bila mainstream media unaweza julikana.
Thank mkuu ila mengi yeme evaporate maana maisha yana stress nyingi hasa ukiwa baba unaetegemewa. Miaka 10 iliopita nilikuwa nafanya maokoto ya maneno ya magwoji wanaojua kufikiri, kutafiti na kuandika. Sasa hivi naokoteza okoteza ba ku share hspa jf. Vile vike najifunza humu JF kuna watu wanajua mengi sana sana.We jamaa una madini sana mkuu... Uko vizuri mkuu
Thanks mkuu, japo umeandika kidogo lakini nimeokota mengiThank mkuu ila mengi yeme evaporate maana maisha yana stress nyingi hasa ukiwa baba unaetegemewa. Miaka 10 iliopita nilikuwa nafanya maokoto ya maneno ya magwoji wanaojua kufikiri, kutafiti na kuandika. Sasa hivi naokoteza okoteza ba ku share hspa jf. Vile vike najifunza humu JF kuna watu wanajua mengi sana sana.
Haujutii hata kuwapigia kura fisiemu!Sina ninachojutia. Kila nilichopitia kilikuwa daraja la kunifikisha nilipo hivi sasa.
Najitahidi kuwa bora, nisiwe kama nilikotoka.
Majuto yafaa nini ikiwa maisha ni sasa?
Anza kuishi sasa, achana na yaliyopita.
Sijawahi!Haujutii hata kuwapigia kura fisiemu!
lakn ukishajitambua si inakuwa imeisha iyoKufanya kazi za watu muda mrefu hadi usiku nakusahau kupambania ndoto zangu. Kumbe niligeuzwa ngazi ya kuwapandisha wengine badala ya kujituma kuboresha malengo yangu