Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Wakuu,

Disclaimer🫢 Hapa hatuongelei pesa madafu

Kuna mtu alisema ameenda kwa rafiki yake akakuta wana pump ya mafuta kwao🤣🤣🤣🤣

Yaani mambo za kwenda sheli si habari zao. Wanamaliza tuu hapo nyumbani

Hata mimi ningeshtuka kwa kweli 😀

Wewe ni nini uliona kwa Watu ukajua pesa ipo?
Mimi binafsi nikikuta mwanamke mwenye nyashi ya haja najua hapo hela ipo
 
Maisha hatufanani..kabisa nimekuja kuona tena kitu kama hicho kwa boss wangu mmoja mzungu nae anapaka wake nyumbani wanabudget kubwa kama laki 4 kwa mwezi isee mapaka manene hadi kutembea yanashindwa..

paka wananunuliwa hadi toy za kuchezea..
Jamaa akaniambia hawa paka waliokotwa kwenye jaa kwanza hawataki mazoea na rangi nyeusi kabisa wakiwaona wanaondoka na yule mzungu alivyo mweu anasema hataki wageni kwake wanawapa stress paka wake..
Nikacheka sana nikasema hao paka wanajua balaa la jua kali huko nje wamekubali kuwa machawa hapa maisha yaende..mzungu aamini hivyo anaamini wale paka wanapata msongo wa mawazo sababu sisi waafrica tuna watisha na kuwapiga ovyo bila sababu.
Umenikumbisha kisa Cha yule mchezaji anaitwa Kurt Zouma (sijui kama nimeamdika sawasawa)... Huyu jamaa alituhumiwa kumpiga Paka wake.... Wazungu walikuja juu mpaka jamaa akawa anakatwa mshahara wake.... Na akafunguliwa mashtka kwa kosa la kunyanyasa wanyama.... Ilivuma sana hii kesi pale England.....🤣🤣🤣
 
Nilipata connection sehem yenye maslah zaidi kupitia hyo hyo kampuni so sikuondoka kwa ubaya anytime namm naenda as a customer now and kuwapa hi washkaj na mabos wangu walinibless coz hata wao ni waajiliwa tu anytime fursa mpya ikitokea wanaweza sepa pia.
Congratulations, ipo siku na mimi nitakuwa naamka kwenda ofisini narudi nyumbani jioni
 
Congratulations, ipo siku na mimi nitakuwa naamka kwenda ofisini narudi nyumbani jioni
Kutoka ndani ya uvungu wa moyo nakuombea mkuu kikubwa usichague kazi kamwe huwez kupata kazi kama hauna kazi humu humu kwny maofisi tunayoanza nayo ndiyo tunakutana na fursa mpya.

Kikubwa kuwa muadilifu na mchapakazi kuna watu wanakufatilia pasipo wewe kujua hii ndiyo kitu pekee ilonifanya nikawa shifted kutoka nilipokuwa mpaka nilipo, jali na upende unachofanya.
 
Mzee wangu alitokea familia ya kimaskini Sana.
Babu alikuaga na ngo'mbe wengi Sanaa
Kimiujiza miujiza miaka ya 60's watoto wa Babu kwa miaka tofauti tofauti walikua wanafaulu darasa la saba na kuchaguliwa shule za SERIKALI

Walisomaga zamani na wakabahatika kupata kazi nzurii serikalini na wote wamekua watumishi mpaka Kustaafu kwao utumishi serikalini.

Kwenye tumbo la mama tupo wa 5 hakuna hata mtoto mmoja ambae Hana degree wa mwisho ndio kamaliza hapo Udsm mwaka huu

NB.
Kuna familia ukizaliwa unakua mwenye bahati na chance kubwa ya kuwa na option mbali mbali za kutimiza ndoto/goals E.t.c
Na kuna zingine ukizaliwa umekwisha😅😅
 
Umenikumbusha Leo wakati natoka safari flani nchi jirani nklivyofika mitaa ya jiji la mwenye bunge nikaona jengo flani Zuri na jipya kwa juu inaonekana apartments ila nimekuwa disappointed kuona kamba zimeanika nguo tena karibu unit tano nikajiuliza hivi hawa awana drier
Apo chacha.
Yale ma apartments ya kariakoo jee yanavoning'inia maguo. Ht haipendezi
 
Back
Top Bottom