Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Mmeongea habar za paka kutumia laki hadi nmecheka
Nakumbuka miaka kadhaa nyuma Bro alikuja home, hakuwa home kwa muda so akarudi na rafk ake sasa skuio wakapikiwa wali na samaki wakatengewa wali na samaki mkubwa uyoo sa ngap muda wa kunawa pale yule paka akarukia yule samaki akashuka nae mpka chini,
Aisee nlikua naskiaga paka anaroho saba ila sjajua labda skuio alitembea nayo moja ama vipi maana alipokea rungu moja ata sjui bro alitoa wapi rungu lile maana hazikuisha hata sec 30 toka bwana paka azingue na paka alikaa kmya hadi leo hii navyoongea ndugu waandxh wa habar
Yan mkuu watu wanatumia bajeti ya 400k kwa paka wakati mm mshahara wangu ni 280k🥺
 
Miaka ya 89's nyumbani tulikuaga na Tv, fridge, washing machine,choo Cha kukaa, nyumbani Kuna umeme, mashine ya kunyolewa, jiko la umeme , oven , pressure cooker N.K
Kumiliki ivyo vitu enzi izo yaani mnaonekana matajir wakubwa Sanaa 😊

Maisha yamebadilika Sanaa Sanaa sikuizi hivyo vitu sio big deal tenaa...
Kwa 1989 bila baba yako kuwa mtu mkubwa serikalini au mfanyabiashara mkubwa ungepata wapi hayo?
 
Hizo nguo unaanikaje? Au unaweka ngazi?
Umenikumbusha Leo wakati natoka safari flani nchi jirani nklivyofika mitaa ya jiji la mwenye bunge nikaona jengo flani Zuri na jipya kwa juu inaonekana apartments ila nimekuwa disappointed kuona kamba zimeanika nguo tena karibu unit tano nikajiuliza hivi hawa awana drier
 
Enzi hizo nipo form six tumetoka shule jumamosi kufanya test tukaenda nyumbani kwa rafiki yetu huyo..

Dah..tumefika tu tunakuta maagizo kwa house girl wao eti mama yake ameacha laki 100,000... jamaa akachukue chakula cha paka da nilishtuka sana.. nikamwambia jamaa yaani paka wenu hawa wanabudget nzuri hivyo kuliko watanzania wengi sana kweli maisha hatufanani.... akacheka tu.

Paka wenyewe wawili 2 nikiwaangalia kama wa mitaani tu..wamejilaza kwenye makochi
Hiyo ni mwaka 2014..

Kifupi jamaa hata chuo akwenda hakusubili matokea akasepa zake state hadi leo yupo huko alisoma chuo hukohuko ameoa hukohuko kifupi maisha kwenu yakiwa kwenye hali nzuri kuna uwezekana mkubwa sana watoto pia wakaishi maisha mazuri tu hata wakikuwa.

Yule jamaa napiga nae story hadi leo namkumbusha wale paka anasema walikufa.yeye anawaita na majina kabisa.
paka majini lazima wale
 
Mzee wangu alitokea familia ya kimaskini Sana.
Babu alikuaga na ngo'mbe wengi Sanaa
Kimiujiza miujiza miaka ya 60's watoto wa Babu kwa miaka tofauti tofauti walikua wanafaulu darasa la saba na kuchaguliwa shule za SERIKALI

Walisomaga zamani na wakabahatika kupata kazi nzurii serikalini na wote wamekua watumishi mpaka Kustaafu kwao utumishi serikalini.

Kwenye tumbo la mama tupo wa 5 hakuna hata mtoto mmoja ambae Hana degree wa mwisho ndio kamaliza hapo Udsm mwaka huu

NB.
Kuna familia ukizaliwa unakua mwenye bahati na chance kubwa ya kuwa na option mbali mbali za kutimiza ndoto/goals E.t.c
Kwa kichwa changu ningezaliwa 70'S ningekuwa niko njema sana😁
 
Sio Kama zamani Tv mnaibeba mnapeleka chumbani enzi izo Kuna wizi wa fatuma..

Ni kweli Ila at least siku izi kuwezi pita nyumba 10 bila kukutana na vitu ivyo vimekua vya kawaida Sana kwenye Maisha ya town.
Wa kumshukuru ni mchina maana kama hali ingekuwa ile ile ya kumiliki JVC, SONY na Panasonic nafikiri kwa sasa bei ya TV ingekuwa ni sawa na bei ya magari mengi yaliopo barabarani😀
 
Kuna ofisi moja nilikuwa nafanya kazi miaka kma mitatu nyuma, nlikuwa cashier mm na mwenzng.

Akaja mteja mmoja wkt huo mm nilikuwa namuhudumia mteja mwengine mwenzng akampokea uyo jamaa, sasa jamaa bill yake ilikuwa inasoma milion mbili na jamaa alitoa card ya bank kulipia.

Kikichotokea mwnnzg akakosea kuandika zile digits baada yakuandika two milions jamaa akakosea akaandika milion mia mbili na akaprint na risit na akampa jamaa nae akaondoka wote bila kujua.

Mziki ukaja wkt wakufunga hesabu tukashangaa mbona mauzo yapo juu kuliko kawaida huku na huku ndiyo kugundua error ilofanyika huwez amini ilipita wiki nzima na jamaa hakushtuka kabisa uzuri kwny risit kuna option yakuandika namba ya mteja ndiyo anapigiwa anaambiwa yan hata yeye hana hbr wala kushtuka ikabidi kampuni imuombe samahan tu aje na jamaa alikuja kurud badae sna nkasema kuna watu wana mbumba aisee milion mia mbili inatolewa na bdo mtu hashtuki.
 
Back
Top Bottom