Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Yan mkuu watu wanatumia bajeti ya 400k kwa paka wakati mm mshahara wangu ni 280k🥺
 
Kwa 1989 bila baba yako kuwa mtu mkubwa serikalini au mfanyabiashara mkubwa ungepata wapi hayo?
 
Hizo nguo unaanikaje? Au unaweka ngazi?
Umenikumbusha Leo wakati natoka safari flani nchi jirani nklivyofika mitaa ya jiji la mwenye bunge nikaona jengo flani Zuri na jipya kwa juu inaonekana apartments ila nimekuwa disappointed kuona kamba zimeanika nguo tena karibu unit tano nikajiuliza hivi hawa awana drier
 
paka majini lazima wale
 
Kwa kichwa changu ningezaliwa 70'S ningekuwa niko njema sana😁
 
Sio Kama zamani Tv mnaibeba mnapeleka chumbani enzi izo Kuna wizi wa fatuma..

Ni kweli Ila at least siku izi kuwezi pita nyumba 10 bila kukutana na vitu ivyo vimekua vya kawaida Sana kwenye Maisha ya town.
Wa kumshukuru ni mchina maana kama hali ingekuwa ile ile ya kumiliki JVC, SONY na Panasonic nafikiri kwa sasa bei ya TV ingekuwa ni sawa na bei ya magari mengi yaliopo barabarani😀
 
Kuna ofisi moja nilikuwa nafanya kazi miaka kma mitatu nyuma, nlikuwa cashier mm na mwenzng.

Akaja mteja mmoja wkt huo mm nilikuwa namuhudumia mteja mwengine mwenzng akampokea uyo jamaa, sasa jamaa bill yake ilikuwa inasoma milion mbili na jamaa alitoa card ya bank kulipia.

Kikichotokea mwnnzg akakosea kuandika zile digits baada yakuandika two milions jamaa akakosea akaandika milion mia mbili na akaprint na risit na akampa jamaa nae akaondoka wote bila kujua.

Mziki ukaja wkt wakufunga hesabu tukashangaa mbona mauzo yapo juu kuliko kawaida huku na huku ndiyo kugundua error ilofanyika huwez amini ilipita wiki nzima na jamaa hakushtuka kabisa uzuri kwny risit kuna option yakuandika namba ya mteja ndiyo anapigiwa anaambiwa yan hata yeye hana hbr wala kushtuka ikabidi kampuni imuombe samahan tu aje na jamaa alikuja kurud badae sna nkasema kuna watu wana mbumba aisee milion mia mbili inatolewa na bdo mtu hashtuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…