Ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani ulipokuwa mtoto?

Kombolela nliwahi enda kujificha ofis ya mwalimu mkuu [emoji23][emoji23][emoji106] walitafta sana wale watu

Siku nyingine nkaenda chumbani kwa baba nkalala

Ananiamsha asubuhi niende shule [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huo ulikuwa ukorofi😂😂😂
 
Miye miaka pale Tandale lingo la Kuni nilikuwa napenda sana muziki wa kughani,na lilikuwepo kundi lilikuwa linaitwa Niggaz,Kuna siku Mjomba yangu alinikuta naangalia video shooting ya nyimbo ya hao jamaa aisee

Alinikimbiza siyo kitoto na bakora juu
Vipi sasa hivi, huwezi kurudia ukafanya mambo?
 
Mchezo wa kibaba mama,mtaani kwetu wadogo kipindi hicho Kuna ka manzi mama yake alikuwa jaji wa wilaya,kwao matawi kalikuwa cheupeee,ila nlikuwa napenda kukaa nacho karibu,watu wakawa wanatuita wachumba wachumba,Mimi hapo nina miaka 6 sijui lolote kuhusu madem.Basi kila tukicheza huu mchezo ananichagua Mimi kuwa baba,basi nakumbuka nlinenepa Sana Kwa muda mfupi,ila Hali ilibadilika na nkauchukia huu mchezo baada ya dogo mmoja mdasalama kuhamia mtaani,manzi akamchagua Jamaa awe baba mi nkaambiwa niwe mjomba,kwakweli sijui hata hasira zilitoka wapi maana nilizichapa Sana na mdasalama,na mchezo huo mtaani pale uliisha siku Hiyo maana wazazi walipata taarifa,kikafuatia kipigo Cha maana kwa tulioshiriki.
 
Mpira nlkua nacheza sana
Nadhani mpaka leo mtu anaweza hisi unawaza kitu serious kumbe unawaza mpira

Ila ndoto za mpira zliisha nlpovunjika nlmpiga chenga mbaba mmoja akanizoa nikadondoka a
Pole sana....ukakimbia mazima kwenye soka
 
Kuwinda Njiwa porini hahah ile shabaha ningekuwa Dunia ya kwanza huko aisee ningekuwa kwenye kitengo muhimu haha
Vipi sasa hivi bado una shabaha au ishakuwa tia maji tia maji?
 
Wakuu,

Watoto na michezo ni kama samaki na maji, wengi tushazama kwenye michezo mpaka tukaja kufatwa na fimbo huko tulipokuwa. Wakati mwingine mzazi mpaka anapata wasiwasi labda mtoto kapotea, kumbe mtu kazama kwenye kombolela huko?

Katika michezo yote niliyoweza kucheza rede nilikuwa fundi, yaani mpaka watu walikuwa hawataki nicheze maani nikiingia ni kufunga tu, na tukiwa wengi ni mwendo wa kuokoa wenzangu tu. Pia niikua nilikuwa fundi wa kucheza goroli, yaani nilikuwa na makopo yaliyojaa goroli zilizopuna watoto wengine😂😂😂.

Wewe ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani utotoni?

View attachment 2647601View attachment 2647603
View attachment 2647604View attachment 2647598
Ila utoto wa zamani tulifaidi sana mambo yalikuwa reality kabisa sio kama sasa kabisa...
Mpira wa sodo nimefuma sana.. tengeneza ndege naweka mota ya redio panga zinazunguka fresh na inatembea kabisa...gari ndio za kila aina nilikuwa natengeneza...

Kipindi hicho mechi mnaenda kucheza mnajipanga haswa maana chochote kinaweza tokea na hakuna kuachana..

Utoto ulikuwa enzi zetu isee. Ni utoto kweli..!

Kwenye mtaa wetu watoto wote tulipeana majina ya vyeo vya kijeshi mwingine wagambo... captain, luten, koplo, sir major mimi walinipa umajor..tukisema leo tunaenda kuwinda basi lazima turudi na sungura..
Isee nimekumbuka mbali sana.
 
Nilikua dancer wa zile nyimbo za utamaduni(vingoma), ile unajifunga kanga ama kitenge kiunoni afu unakata mauno😀😀🏃‍♀️
 
Goroli ya kishimo nilikua nawapuna balaa wakiishiwa nawakopesha tunahamia kwenye cha boss halaf mimi ndio nakua boss,nilijaza dumu la uhai la lita 5 goroli tupu na madungu ya kutosha,siku hiyo nilifanya msala sikwenda shule nipo kwenye goroli nagawa dozi,ghafla mdingi akanidaka kwenda hom chini ya uvungu wa kitanda anakuta nina dumu la lita 5 limejaa gololi nilichezea kichapo toka siku hiyo gololi ndio ikawa mwisho maana waliitwa watoto wa mtaa mzima huku nakula fimbo huku nagawa sanda kalawe(amina),mwenye kupata (apate)...Dingi alikua mkax sana kwenye ubora wake

Kipindi cha mpito kilivyopita nikahamia kwenye Ludo,huku napo nilikua balaa sema huku ndio nikajifunza na kamari maana nilijifunza kwa mabro ambao mwanzoni nilijua wanacheza kujifurahisha,kumbe wao wanacheza kazi nilivyoiva nami nikachora langu nikaanza kuwafundisha kitaa bure,walivyolijua ikawa ni mwendo wa pesa mbele hili mdingi alivyolijua alienda kukiwasha hadi maskani kwa mabro wanaocheza ludo...Yaani hii siku siwezi isahau maana mzee alikiwasha hadi mabro wakaita difenda mzee alilala ndani hii siku

Picha ya Ludo
Screenshot_20230606-200148_Chrome.jpg
 
Wakuu,

Watoto na michezo ni kama samaki na maji, wengi tushazama kwenye michezo mpaka tukaja kufatwa na fimbo huko tulipokuwa. Wakati mwingine mzazi mpaka anapata wasiwasi labda mtoto kapotea, kumbe mtu kazama kwenye kombolela huko?

Katika michezo yote niliyoweza kucheza rede nilikuwa fundi, yaani mpaka watu walikuwa hawataki nicheze maani nikiingia ni kufunga tu, na tukiwa wengi ni mwendo wa kuokoa wenzangu tu. Pia niikua nilikuwa fundi wa kucheza goroli, yaani nilikuwa na makopo yaliyojaa goroli zilizopuna watoto wengine😂😂😂.

Wewe ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani utotoni?

View attachment 2647601View attachment 2647603
View attachment 2647604View attachment 2647598
Kombolela
 
Nilikuwaga mwizi wa njiwa asee namshukuru Mungu niliachaga manake ningeendelea saivi sijui ningekuwaje!
 
Wakuu,

Watoto na michezo ni kama samaki na maji, wengi tushazama kwenye michezo mpaka tukaja kufatwa na fimbo huko tulipokuwa. Wakati mwingine mzazi mpaka anapata wasiwasi labda mtoto kapotea, kumbe mtu kazama kwenye kombolela huko?

Katika michezo yote niliyoweza kucheza rede nilikuwa fundi, yaani mpaka watu walikuwa hawataki nicheze maani nikiingia ni kufunga tu, na tukiwa wengi ni mwendo wa kuokoa wenzangu tu. Pia niikua nilikuwa fundi wa kucheza goroli, yaani nilikuwa na makopo yaliyojaa goroli zilizopuna watoto wengine😂😂😂.

Wewe ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani utotoni?

View attachment 2647601View attachment 2647603
View attachment 2647604View attachment 2647598
Mwizi
 
Sarakasi. Mama yangu alilia mno nilipoteguka kiuno kwa kuanguka vibaya.

Nikaacha mpaka na leo. Maji hufata mkondo, dogo naye kashaanza kuruka. Nikimuangalia nasisimka kwa kuogopa.
Pole dokta
Muhimu umepata watoto hata kama uliteguka kiuno😂🤸
 
Back
Top Bottom