Ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani ulipokuwa mtoto?

Ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani ulipokuwa mtoto?

Futbol na Check number, hii chek namba nilikuwa nakimbia sana.
 
Nilikuwa kichaa wa games

Need for speed 2
Mortal kombat 4
Gta
Thief demo
Delta force
Moto racer
Dave, Mario, Angelo

Sina hamu tena na magem sikuhizi,
Hebu nitumie hilo game la need for speed 2
 
nilikua natmba sana watoto wawatu wenzangu wakienda kucheza mpira mimi nabaki nadadazao🙁🙁🙁
 
Mchezo wa kibaba mama,mtaani kwetu wadogo kipindi hicho Kuna ka manzi mama yake alikuwa jaji wa wilaya,kwao matawi kalikuwa cheupeee,ila nlikuwa napenda kukaa nacho karibu,watu wakawa wanatuita wachumba wachumba,Mimi hapo nina miaka 6 sijui lolote kuhusu madem.Basi kila tukicheza huu mchezo ananichagua Mimi kuwa baba,basi nakumbuka nlinenepa Sana Kwa muda mfupi,ila Hali ilibadilika na nkauchukia huu mchezo baada ya dogo mmoja mdasalama kuhamia mtaani,manzi akamchagua Jamaa awe baba mi nkaambiwa niwe mjomba,kwakweli sijui hata hasira zilitoka wapi maana nilizichapa Sana na mdasalama,na mchezo huo mtaani pale uliisha siku Hiyo maana wazazi walipata taarifa,kikafuatia kipigo Cha maana kwa tulioshiriki.
Mwanaume ameumbwa kuwa mtawala meaning tangia mdogo anataka kuwa na milki/ngome yake. Anapotokea wa kutokea huwa inampandisha hasira na uchungu. Na ndo maana hata mwanamke akicheat ni ngumu kusamehe kwa sabbu mnaona kama ngome yenu imeingiliwa. Na sifa ya mtawala ni kuwa the overall overseer wa ongoings za ngome yake. Ndo maana hamuoni shida kuhonga majumba na magari...sasa huyu mwanadaslam alikuja kuingilia ngome yako..bibie akakufriend zone...ni hatari 😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom