Ulikuwa na umri gani ulipotengeneza milioni yako ya kwanza?

Ulikuwa na umri gani ulipotengeneza milioni yako ya kwanza?

2014 nikiwa na miaka 22 nilikunja mil 1 ya kwanza. Nikanunua uwanja kwa laki 6. Mwaka 2017 nikafulia nikauza kwa ml 1.5, Nikanunua mwingne papohapo kwa laki 9, nikakaa wee nikakosa hela ya kujenga! ilikuwa pori pori wenye hela wakashusha mijengo yao na serikali ikajenga bonge la shule jirani yangu!... mwaka 2022 nikadunduliza nikapata mil 15 cash nikapata kijumba kinauzwa mil 7 nikachukua nikakikarabati mpaka sasa naishi humo... wakuu maisha ni safari ndefu waliotoboa tuwape pongezi!
 
• Habari wana JamiiForums na wafanyabiashara wenzangu, nataka nitengeneze milioni yangu ya kwanza mapema mwaka huu. Hata hivyo, Maana nimekuwa kila nikitafuta hela nashindwa kufikisha million , nataka kujua ni umri gani nyie mlitengeneza milioni ya kwanza na jinsi mlivyofanya au uwekezaji mliofanya mpaka mkapata hiyo million.

• Ndiyo! uchumi si wa kutabasamu kwa sasa, Lakini hii inaweza tumika kama motisha kwa ndugu, jamaa na marafiki, ambao bado wapo kwenye ajira ndogo ndogo na Wanataka kujiajiri au wapo kwenye hatua ya kudunduliza mitaji.

• Tuambie ni lini ulitengeneza milioni yako ya kwanza na kwa njia gani?

View attachment 2859386
Nipo nawazoom 😀😀
 
Hongera mkuu, Unaweza tupa mbinu, sisi ambao hatuja vuna milioni ya kwanza Tufanyaje?,
Kuhusu mbinu mkuu ni uongo sidhani kama nilitumi mbinu as nimeshasema ya kwanza nilifanya kazi part time na ya pili nilipewa. Hiyo ya kwanza labda kuchangamkia vi part time ukisikia vipo, kuomba connection etc.
 
Aged 17 kipindi cha Mkapa awamu ya pili.

Wakati huo shilling ina thamani kweli kweli Tsh 1,000/= kwa siku haiishi hata utumie kwa anasa vipi.
Hongera mkuu, milioni uliivuna mapema sana, Mkuu kwa sasa upo na uzoefu wa pesa, ebu tusaidie sisi Vijana Tufanyaje ili tuvune milioni 2024,
 
Chochote kinachohusu 1M kinanirudisha kwenye ile M1, kapresha kanapanda 😂😂
Hasira zinajidownload..

Mie mkishuka mpaka elf 5 mniite nirudi 🤣🤣🤣
😀😀, Kwa hiyo mkuu, Hutaki kusikia Habari za million
 
2018! Mzee alinisapoti nkalima ekari mbili baada ya mauzo nkapata..... akanifungulia account akaweka humo nlipewa access nlivokua chuo
Hongera sana mkuu, sema haujasema ekari mbili ulilima nini, mpaka ukafanikiwa kuipata milioni ya kwanza.
 
• Ni ya kuitengeneza mwenyewe mkuu,

• Hela ya Boom uliifanyia biashara au uliifanyia matumizi mengine tu?

Nilifanya biashara kidogo kwa miaka kama 2 wakati huo watu hawajaanza kuagiza nguo China...
 
21yrs.... Me katika harakati zangu zote sijawahi kuwa boosted na mtu yoyote hata shilingi moja.... Nimenza harakati nikiwa 18yrs na 0Tsh balance, Now tumepanda viwango kidogo nasubiri kwenye uzi wa first time to own 5m
Nimenza harakati nikiwa 18yrs na 0Tsh balance
Ulichomokaje kwenye hili zimwi mkuu, maana Vijana wengi tunafeli kwenye 0Tsh/Business start with zero Capital, Ebu tupe mbinu, ili tuvune milioni ya kwanza 2024,
 
2014 nikiwa na miaka 22 nilikunja mil 1 ya kwanza. Nikanunua uwanja kwa laki 6. Mwaka 2017 nikafulia nikauza kwa ml 1.5, Nikanunua mwingne papohapo kwa laki 9, nikakaa wee nikakosa hela ya kujenga! ilikuwa pori pori wenye hela wakashusha mijengo yao na serikali ikajenga bonge la shule jirani yangu!... mwaka 2022 nikadunduliza nikapata mil 15 cash nikapata kijumba kinauzwa mil 7 nikachukua nikakikarabati mpaka sasa naishi humo... wakuu maisha ni safari ndefu waliotoboa tuwape pongezi!
• Duh, Hongera sana mkuu, ingawa ulipitia maporomoko ya moyo, lakini hukukata tamaa,
• Mkuu 2024 imefika sasa, unamshauri nini kijana, ambaye anatarajia kuvuna milioni ya kwanza 2024
 
Kuhusu mbinu mkuu ni uongo sidhani kama nilitumi mbinu as nimeshasema ya kwanza nilifanya kazi part time na ya pili nilipewa. Hiyo ya kwanza labda kuchangamkia vi part time ukisikia vipo, kuomba connection etc.
Okay sawa mkuu, ✍️✍️
 
Back
Top Bottom