Ulikuwa na umri gani ulipotengeneza milioni yako ya kwanza?

• Habari wana JamiiForums na wafanyabiashara wenzangu, nataka nitengeneze milioni yangu ya kwanza mapema mwaka huu. Hata hivyo, Maana nimekuwa kila nikitafuta hela nashindwa kufikisha million , nataka kujua ni umri gani nyie mlitengeneza milioni ya kwanza na jinsi mlivyofanya au uwekezaji mliofanya mpaka mkapata hiyo million.

• Ndiyo! uchumi si wa kutabasamu kwa sasa, Lakini hii inaweza tumika kama motisha kwa ndugu, jamaa na marafiki, ambao bado wapo kwenye ajira ndogo ndogo na Wanataka kujiajiri au wapo kwenye hatua ya kudunduliza mitaji.

• Tuambie ni lini ulitengeneza milioni yako ya kwanza na kwa njia gani?

View attachment 2859386
Juzi kati apo ilijipendekeza sensa nakumbuku nilikuwa nafukuzia 25 alafu Phil foden analipwa paundi life is not fair

Unajua maisha hayana formula hata siku moja, wakati nipo home masela waliokuwa wanapangisha geto waliniona mtoto wa mama nmemaliza chuo bado nipo home.

Akili zao ndogo wanajisifu geto kali kodi nalipa kubwa, ukipiga hesabu geto la bei ghali unakuta analipa 50, siku nilipota kazi walijiona wao wajinga sana, maana tukiwa maskani wakati tunapiga story naingiza story zao zakunicheka na wanaishia kunitukana

Hapo ulipo kuna sekunde unaweza piga hatua ya mtu aliyepambana hata miaka 5, lakini ndani ya muda mchache ukaweza archive mambo yote ya mtu aliye hustle 5 yrs.

Kabla hujalala sema money is now flow freely to me.
 
• Duh, Hongera sana mkuu, ingawa ulipitia maporomoko ya moyo, lakini hukukata tamaa,
• Mkuu 2024 imefika sasa, unamshauri nini kijana, ambaye anatarajia kuvuna milioni ya kwanza 2024
waonee uchungu pesa wanayoitafuta. Nikimaanisha ulevi wa aina yoyote waache kbs kama sio kupunguza
 
Juzi kati apo ilijipendekeza sensa nakumbuku nilikuwa nafukuzia 25 alafu Phil foden analipwa paundi life is not fair
Pole sana mkuu, Mwaka huu weka mambo safi, ili tuvune milioni ya kwanza 2024
 
Unajua maisha hayana formula hata siku moja, wakati nipo home masela waliokuwa wanapangisha geto waliniona mtoto wa mama nmemaliza chuo bado nipo home.

Akili zao ndogo wanajisifu geto kwali kodi nalipa kubwa, ukipiga hesabu geto la bei gali unakuta anlipa 50, siku nilipota kazi walijiona wao wajinga, maan tukia maskani wakati tunapiga story naingiza story zao zakunichek na wanaishi kunitukana

Hapo ulipo kula sekunde unaweza piga hatua ya mtu aliyepambana hata miaka 5, lakini ndani ya mud mchache ukaweza archive mambo yote ya mtu aliye hustle 5 yrs.

Kabla hujalala sema money is now flow freely to me.
Maneno ya kishujaa sana haya mkuu, Shukran sana,
 
Hongera mkuu, milioni uliivuna mapema sana, Mkuu kwa sasa upo na uzoefu wa pesa, ebu tusaidie sisi Vijana Tufanyaje ili tuvune milioni 2024,
Hesabu za pesa hazihitaji namba za miaka mkuu utakuta december hii hapa lengo halijatimia u-force ujiharibie mtaani.

Kikubwa baada ya kumtanguliza Mungu unaemuamini kwa imani yako pesa inataka nidhamu,usiige rafiki anakunywa bia na wewe unywe bia anahonga malaya na wewe ukahonge malaya mwisho wa siku ikitokea errors kila mtu anakufa na zake,mimi wakati huo nilifungua account NMB nikawaambia wasinipe uwezo wa kufanya chochote zaidi niwe naweka hela tu baada ya muda nikaenda kuangalia (wakati wa Kikwete) nikakuta kuna hela kiasi nikawaambia wakubwa zangu nataka kiwanja nikanunua uwanja nikiwa aged 21 na ndiyo ninapoishi leo.

Njia nzuri ya kuficha shilingi fungua acc kisha usichukue ATM card wala isiwe accessed na Simu Banking (hivi vitu vinakupa udhaifu hata ukiwa na shida ya 50K na ungeweza kuivumilia mpaka kesho uipate kwa njia nyengine ukishakuwa na hivyo vitu viwili hapo juu utakuwa unajitolea hela hovyo tu,ni njia ambayo mpaka sasa naitumia kujiwekea akiba) uwe unaweka hela huku ukiwa na lengo kikifika kiasi fulani nitafanya kitu fulani ununuzi wa ardhi (best option nayoiamini mimi) au kufungua biashara.

Maadui wakubwa wa hela zetu sisi wavuja jasho jingi:marafiki(hawa ni starehe za makundi),ndugu (nina wazo langu la biashara nakuja kwako kwa sababu najua currently upo kwenye mkondo ukinikopesha biashara ikafa haijafa hela yangu ni yako na najua kabisa kunifunga huwezi maana sisi ni damu)wanawake(hawa sina haja ya kukufafanulia habari zao unazijua na hawa ni mtego mmoja m'baya sana kwa era hii maana wamekuja kuwa na njaa ya kuzidi)kutaka kumiliki vitu vikubwa uwezo ukiwa chini (simu za gharama,gari huku sina uwezo wa kuihudumia % kubwa ya kipato kuishia humo).

Watu wanaotakiwa kuifurahia hela yako to the fullest:mama yako mzazi,baba yako mzazi,mkeo na wanao aliokuzalia hakuna mwenye kutoa neno la baraka likafanya kazi haraka kama hao watu hapo juu nina shuhuda nyingi jinsi hali inavyokuwa ukiwafurahisha.kila la heri.
 
Hesabu za pesa hazihitaji namba za miaka mkuu utakuta december hii hapa lengo halijatimia u-force ujiharibie mtaani.

Kikubwa baada ya kumtanguliza Mungu unaemuamini kwa imani yako pesa inataka nidhamu,usiige rafiki anakunywa bia na wewe unywe bia anahonga malaya na wewe ukahonge malaya mwisho wa siku ikitokea errors kila mtu anakufa na zake,mimi wakati huo nilifungua account NMB nikawaambia wasinipe uwezo wa kufanya chochote zaidi niwe naweka hela tu baada ya muda nikaenda kuangalia (wakati wa Kikwete) nikakuta kuna hela kiasi nikawaambia wakubwa zangu nataka kiwanja nikanunua uwanja nikiwa aged 21 na ndiyo ninapoishi leo.

Njia nzuri ya kuficha shilingi fungua acc kisha usichukue ATM card wala isiwe accessed na Simu Banking (hivi vitu vinakupa udhaifu hata ukiwa na shida ya 50K na ungeweza kuivumilia mpaka kesho uipate kwa njia nyengine ukishakuwa na hivyo vitu viwili hapo juu utakuwa unajitolea hela hovyo tu) uwe unaweka hela huku ukiwa na lengo kikifika kiasi fulani nitafanya kitu fulani ununuzi wa ardhi (best option nayoiamini mimi) au kufungua biashara.

Maadui wakubwa wa hela zetu sisi wavuja jasho jingi:marafiki(hawa ni starehe za makundi),ndugu (nina wazo langu la biashara nakuja kwako kwa sababu najua currently upo kwenye mkondo ukinikopesha biashara ikafa haijafa hela yangu ni yako na najua kabisa kunifunga huwezi maana sisi ni damu)wanawake(hawa sina haja ya kukufafanulia habari zao unazijua na hawa ni mtego mmoja m'baya sana kwa era hii maana wamekuja kuwa na njaa ya kuzidi)kutaka kumiliki vitu vikubwa uwezo ukiwa chini (simu za gharama,gari huku sina uwezo wa kuihudumia % kubwa ya kipato kuishia humo).

Watu wanaotakiwa kuifurahia hela yako to the fullest:mama yako mzazi,baba yako mzazi,mkeo na wanao aliokuzalia hakuna mwenye kutoa neno la baraka likafanya kazi haraka kama hao watu hapo juu nina shuhuda nyingi jinsi hali inavyokuwa ukiwafurahisha.kila la heri.

>Njia nzuri ya kuficha shilingi fungua account kisha usichukue ATM card wala isiwe accessed na Simu Banking(hivi vitu vinakupa udhaifu hata ukiwa na shida ya 50K na ungeweza kuivumilia mpaka kesho uipate kwa njia nyengine ukishakuwa na hivyo vitu viwili hapo juu utakuwa unajitolea hela hovyo tu)uwe unaweka hela huku ukiwa na lengo kikifika kiasi fulani nitafanya kitu fulani ununuzi wa ardhi(best option nayoiamini mimi)au kufungua biashara.

Mkuu Kati ya vitu ambavyo umeniongezea leo kwenye ubongo ni hiki hapa, nakubaliana na wewe kabisa hela ikiwa karibu na mfuko wa suluali au kwa namna yeyote, hata ikiwa umepata shida kidogo lazima utazama simu banking kuvuta mkwanja ili umalize tatizo

wanawake(hawa sina haja ya kukufafanulia habari zao unazijua na hawa ni mtego mmoja m'baya sana kwa era hii maana wamekuja kuwa na njaa ya kuzidi)kutaka kumiliki vitu vikubwa uwezo ukiwa chini (simu za gharama,gari huku sina uwezo wa kuihudumia % kubwa ya kipato kuishia humo).

Kweli kabisa, Kati ya vitu ambavyo vinatuludisha nyuma ni wanawake(michepuko, vimada). Hela nyingi wanaume tunatumia kulea vimada, ambao hawana msaada wowote ule zaidi zaidi ni kukuacha maskini na maumivu makali.

Asante sana mkuu kwa mchango wako mzuri
 
Ulichomokaje kwenye hili zimwi mkuu, maana Vijana wengi tunafeli kwenye 0Tsh/Business start with zero Capital, Ebu tupe mbinu, ili tuvune milioni ya kwanza 2024,
Mbinu ni kuachana na wanawake kabisa, Kupambana huku ukimuomba Mungu kila wakati.... Yeye ndo hutengeneza njia wala haina mjadala unajikuta tu amekuweka mahali unaflow.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri murua, 🙏🙏
 
• Safi sana mkuu, bado unaendelea na kilimo cha ufuta?
• Je hiyo million uliifanyia biashara yeyote?
ilinisaidia kulipa ada ya chuo.

kwasasa nimekuwa mkulima mkubwa wa zao hilo la biashara.
 
• Habari wana JamiiForums na wafanyabiashara wenzangu, nataka nitengeneze milioni yangu ya kwanza mapema mwaka huu. Hata hivyo, Maana nimekuwa kila nikitafuta hela nashindwa kufikisha million , nataka kujua ni umri gani nyie mlitengeneza milioni ya kwanza na jinsi mlivyofanya au uwekezaji mliofanya mpaka mkapata hiyo million.

• Ndiyo! uchumi si wa kutabasamu kwa sasa, Lakini hii inaweza tumika kama motisha kwa ndugu, jamaa na marafiki, ambao bado wapo kwenye ajira ndogo ndogo na Wanataka kujiajiri au wapo kwenye hatua ya kudunduliza mitaji.

• Tuambie ni lini ulitengeneza milioni yako ya kwanza na kwa njia gani?

View attachment 2859386
Sikumbuki ni lini niliwahi kuwa na milioni kamili yangu kama yangu ila ninakumbukimbu ya mwaka wa 2010 nikikabidhiwa milioni 5 kash, sikuwahi kushika kiasi kama hicho kabla yake, nilikua mwaminifu wa ile hela japo ikiwa ni ugenini haswa, mwenye kunipa alikua mgeni nami, na mahali aliponipea nilikua mgeni haswa ila nilimaliza kazi nami nikabakiwa na laki na themanini yangu kwa uaminifu mkubwa kabisa.

Kazi yangu inanifanya nakuwa na hela nyingi kuliko uwezo wangi lakini ni za watu , ila falsafa yangu ni uaminifu, nikose mimi apate mwenzangu.
 
Back
Top Bottom