Ulikuwa wapi miaka yote hiyo, umefika miaka 40 ndio unaanza kupambana?

Kwani kuwa na pesa inatakiwa uwe na miaka mingapi?

Mbona Lil Bow wow alianza kushika pesa akiwa na miaka 13 ,je ndiyo tuseme kwamba kuanzia miaka 13 uanze kupata pesa? Mmiliki wa KFC alitoboa akiwa na zaidi ya miaka 70 ,sasa Benchmark ya kupata pesa ni Umri gani hasa?

Hata katika huo umri wako wa miaka 26 Dayamondi alikuwa tayari kashatoboa kwenye huo umri...sasa umri sahihi wa kuwa napesa ni upi?
 
Tema mate chini...
 
Life begin at 40
 
Na walio filisika, kuke geita vijana wengi wamekamata hela kwenye early 20s leo hawana kitu usichukulie poa maisha mkuu
 
Machalii kule geita wametengeneza millions of money migodini leo hawana kitu, life bhana
 
Maisha hayana umri wala kanuni. Unaweza ukawa na kila kitu leo ila ikaja dhoruba moja tu ikakuondoa kabisa kwenye mfumo. Kila mtu angependa kufanikiwa mapema ila ndo haiwezekani kwa wote. Kusema kuwa wenye 40 wanaopambana hawakuwa na mipango unakosea sana. Kuna watu walikuwa bright darasani, wacha Mungu na wenye malengo mengi maishani ila hadi leo hii wanasulubika mambo ya fedha hayajakaa sawa. Kuna wengine hawajali sana ila hela zinawafuata.
 
Si kila anayefika 40 amechelewa, wala si kila aliyefika 30 alikuwa tayari. Maisha hayana ratiba moja kwa kila mtu. Wengine wanapata fursa mapema, wengine wanapitia majukumu, makosa na changamoto zinazowachelewesha.

Cha muhimu ni pale unapogundua umefanya makosa, usipoteze muda kujilaumu. Anza ulipo, tumia ulicho nacho na pambana kwa nidhamu. Hata ukiwa 40, 50 au zaidi, bado unaweza kujenga maisha mazuri. Maadamu bado una uhai, ukurasa haujafungwa.
 
Sema una point.Kijana Kujitambua mapema kuna faida zaidi, wengine wanabarikiwa kupata hela wakiwa vijana kwenye miaka 20s lakini kutokana na kuamini kuwa muda bado wanafanya ndivyo sivyo na kuja kuwa serious kwenye miaka 40s.

Lakini sio wote wanaopambana zaidi kwenye 40s sio kwamba walizembea kwenye miaka ya 20s au 30s.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…