Ulikuwa wapi miaka yote hiyo, umefika miaka 40 ndio unaanza kupambana?

Ulikuwa wapi miaka yote hiyo, umefika miaka 40 ndio unaanza kupambana?

Oh sasa ndio najitambua in early 40, mwanzo yalikuwa ni yaleyale maisha ya ujana ukiwa na mafanikio kula bata na kusogeza mipango mbele. Ila yote juu ya yote inategemea umekulia katika jamii ya aina gani na mazingira yaliyokuzunguka kuanzia ya kifamilia na mengineyo. Hakjna watu wanaochelewa sana kuanzisha familia kama wanaojitegemea wenyewe bila kupata miongozo ya ndugu especially kama wazazi walishatangulia mbele ya haki. Maisha ya kimafanikio hayana formula ya age flani
Upo sawa, unaweza kuanza vizuri ukamaliza vibaya na unaweza kuanza vibaya ukamaliza vizuri.
 
Guys kwanini miaka 40? Watu wengi wanakuwa serious wanapofika umri wa miaka 40.

Yaani akishafikisha 40 ndio anaanza kuwa na mikakati, saving, biashara, kujenga etc, ulikuwa wapi huko nyuma?

Je! Huko 30+ ulikosa fursa? Je! Unaweza kufanikiwa kimaisha ukiwa serious kwenye umri huo? Huko nyuma ulipata fursa ukazitumia vibaya, baada ya kufika 40 ndio unaona sasa niwe serious.
Kuna ule msemo wa kiinglish unaosema life starts at 40 unaujua??
 
Guys kwanini miaka 40? Watu wengi wanakuwa serious wanapofika umri wa miaka 40.

Yaani akishafikisha 40 ndio anaanza kuwa na mikakati, saving, biashara, kujenga etc, ulikuwa wapi huko nyuma?

Je! Huko 30+ ulikosa fursa? Je! Unaweza kufanikiwa kimaisha ukiwa serious kwenye umri huo? Huko nyuma ulipata fursa ukazitumia vibaya, baada ya kufika 40 ndio unaona sasa niwe serious.
Nitaleta Uzi kuhusu number 40 hii number nayo Ina maajabu yake Jitu la kienyeji
 
Issue ni vipaumbele. Kuna wengine wanaweza kufanya tofauti na kujenga, biashara na savings. Kumbe wanatengeneza fyucha kubwa zaidi ya hayo.
 
At 40
  • -Mtoto wa kwanza wengi ana 15+ yrs anaanza kukuamsha kuwa ushaanza kuzeeka jipange.
  • -60 umri pendwa unaiona ndani ya 10 moja na kidogo, inaanza kukustua kwamba nguvu zintakuishia soon.
  • -Itakuwa umeshajua udhaifu wako uko wapi kutoka na kunguka kama kulitokea.
  • -Wengi uliouwa unawaona wakubwa unaona mlingana mpo kwenye kategori moja., just imagine ulipokuwa darasa la 9 ukiwa na miaka 14 mwenye miaka 24 alikuwa mtu mzima sana kwako, ila leo wewe una 40 na yeye 50.. wote mnaugua tezi dume
  • -Mambo ya "nita" yanaondoka inabaki "nina" maana ishu siyo muda ila nguvu zinayeya kiaina.
Sawa ila haya mambo ya umri yanachanganya sana ivi ushawai kujiuliza Mimi Nina miaka 20 na wewe una miaka 60 maana yake Mimi ni mara 3 ya umri wako! Lakini baada ya miaka 20 Mimi nitakuwa na miaka 40 na wewe 80 kwanini siwi tena mara tatu yako?
 
Mimi niko na miaka 75

Nikiwa 40 nilikua nimejipambanua, stable income, ya kunitosha mimi na familia yangu ndogo

by 60, nikabaki mwenyewe, watoto wakaenda kwenye mihangaiko yao, nikahama kutoka kwenye nyumba kubwa nikahamia apartment ndogo ya kwangu.

Sasa hivi niko mwenyewe still, nikiamka asubuhi, naenda kanisani, misa ya asubuhi, nafanya mazoezi, naangalia mambo yangu ya kiuchumi, nakunywa chai, nakunywa Balimi, nasoma magazeti naingia jamii forums, nakunywa tena Balimi.

Maisha ya mwanadamu ni ubatili, tafuta kwanza ufalme wa Mungu, mengine yatakuja kwa ziada
 
Katiba inasemaje kwani?Tafsiri ya kupambana kwako ipoje?unafikiri huko nyuma huyo mtu alikuwa hapambani?
 
Back
Top Bottom