Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Haikuchukua muda aliondoka na ghafla niliskia mlango wangu wa chumbani ukigongwa mfululizo nilifungua mlango na baba aliingia pale chumbani.
Kiukweli ninao kaka zangu watatu lakini baba yangu yupo karibu sana na mimi na muda mwingi anapenda kuwa karibu na mimi na sio baba tuu hata mama pia.
Na umri wangu niliokuwa nao lakini baba alikuwa akiota kitu lazima aniulize nimpe tafsiri sijui kwanini lakini ndio ilivyo, mbali na baba hata watu wengine nilipokuwa Tanga huja na ndoto zao niwape maana .
Jambo hili lilimsukuma sana baba kunambia ndoto yake kama alivyonambia mzee Ruhaby kuwa baba ataota ndoto na kunambia
" Wee mswahili ( aliniita baba kwa utani ) bwana nimeota kitu sielewi kabisa, hivi yule mgeni aliyekuja inawezekana vipi nimuote kwa muda mfupi huu, au ndoto za mchana hizi ? Alisema.
Alinambia ndoto yake kuwa palikuja watu watatu vijana mmoja kati yao ni msichana, walimsalimia na kumwambia tumetumwa na baba tukuchukue tukupeleke nyumbani, walitoka nae na kupanda farasi mweupe mzuri sana na kuna sehemu walivuka bahari eneo kubwa sana lilikuwa na maji na majengo ya rangi nyeupe. walifika katika mji na kuuacha na kufata eneo la jangwa, hadi kwenye mti mkubwa wa mtende hapo wakamfunga farasi na kutembea hadi kwenye lango kubwa mfano wa geti na hapo walikuja watu wawili kuwapokea.
Mandhari yalikuwa mazuri sana ni mfano wa kasri la kifalme. Kuta za nyumba zilikuwa na rangi yenye kuwaka sana.
Pia aliona njiwa wengi weupe na hapo waliingia kwenye ukumbi mkubwa sana na kumuona mzee aliyekuwa amekaa katika kiti huku yupo na fimbo ndogo pembeni.
Hapa nikakumbuka safari yangu ya Iran nilikofanyiwa maulid nikagundua alikwenda pale nilipoenda mimi, yule mzee akamuuliza unanikumbuka? Mimi ni Ruhaby sultan na hapa ni Iran rejea maongezi yangu na wewe pale nilipokujia nyumbani kwako na kukupa kitabu .
Vitabu hivi vipo viwili tuu kimoja nimekupatia wewe na kingine kipo hapa , nimetuma watu wangu kukuleta hapa kukufungua uweze kujua ukweli.
Kwa muda mrefu nimekuwa swahiba na mtoto wako lakini muda haukuwa muafaka wewe kufahamu.
Hapa ni himaya yangu mimi ni sultan wa makazi ya hapa zaidi ya miaka mia tano nipo Iran na baba yangu alikuwa swahiba mkubwa wa babu wa mtoto wako . Baba yangu ni wa hapa Iran na mama yangu ni kutoka Oman.
Baba yako wewe alikuwa na uswahiba mkubwa na baba yangu na mimi nimefanya uswahiba na mtoto wako.
Hapo kwa mujibu wa baba alivyonieleza kuliletwa kitabu kikubwa cha ngozi kikafunuliwa na kumuona babu akiwa na mzee na aliona mandhari ya kigombe na boza pangani. Mbele yake ilisogezwa kitu kama pazia akawa anamuona baba yake yaani babu akiwa katika mazungumzo ya mara kwa mara na watu waliokuwa na mavazi ya kanzu na ndevu nyingi na vilemba kichwani.
Kwa mujibu wa maelezo yake baba aliona mti wa mbuyu na kisima kidogo pembeni na yalikuwa ni mandhari ya kigombe ni kando kabisa ya bahari ( na hili eneo hadi leo lipo na kisima kipo ) hapo aliona mara kwa mara pakifungwa farasi mweupe na akaambiwa farasi aliyempanda ndio yule anaemuona katika pazia lile anazaidi ya miaka 120.
ITAENDELEA
Naendea majukumu mengine ya hapa na pale thread hii ifatilie mtajifunza kitu : utulivu wenu na maswali yenye nia ya kujifunza utafanya niwaeleze mengi bila kuweka password
Allah akusaidie umalize kwakweli mana kwa uzoefu wangu wa kusoma ilmu za namna hii humu asilimia kubwa hua hawamalizi na sababu nlishazisema huko juu
* Ubinafsi mbaya sana wa watu , wanataka wao tu ndio wajue na wanaitumia kuwachaji watu pesa nyingi kuwasaidia matatizo yao

*Kugusa Siri flan ambazo Hawataki wengine wajue japo katika falme yako umeruhusiwa kuongea ..mwisho kabisa hufuatwa kuambiwa waache kusimulia. Wengine huanza kuleta mambo ya udini. Kuna sehem najua ukifika tu wataanza kuja...saiv ni kama wamekaa attentive mode..
 
Allah afanye wepesi kama ilivyotakiwa niwafikishie basi nifikishe kikamilifu mola anijaze nguvu na kunitanulia kifua kuhimili.
 
Kilichotumika ni kitu kinaitwa tel Al ard au ardhini ( kukunja ardhi kupunguza umbali ) ni sawa sawa na kuvusha mguu kutoka kizingiti cha mlango kwenda nje ni muda mfupi sana upo Tanga na muda mfupi sana upo Iran.
Na hii ni sehemu ya ilmu katika kusafiri hakuna kipando unapanda ila ni kukunja ardhi na kupunguza umbali kufumba na kufumbua upo Iran.
Sababu ya wao kujitenga ni energy difference baina ya majini na binaadamu.
Nishati ya majini na binaadamu ni tofauti hivyo kuna mmoja humuathiri mwenzie kwa miale au mionzi ya nishati ya mwili
Hongera kwa hii elimu.
 
ACHA WIVU MAKU WE
Yaani mi nikuonee wivu we maskini, mashamba na limbukeni? Nimeanza kubalehe 1990 na nikeshaona kila aina ya mwanamke na pia nina watoto kama wewe.

Hayo masuala ya ngono unayofanya yalikuwa na umuhimu gani kutueleza watu wasiohusika wala wasiokujua tena kwenye uzi usiohusiana na ngono?

Inawezekana we dogo ni punga na ndio maana una pretend kuwa kidume. Alafu acha ushamba, kwa ulimwengu wa sasa hakuna anayejivunia umalaya. Watu tunajivunia pesa.

Maskini na gasho mkubwa.

Pumbavu. Usiwe unatukana watu. Mi Baba yako.
 
Nimeuliza nahitaji kufahamu,niliwahi sikiliza stori hizi,pia natamani niwe na uwezo wa kijini
Hii ni ukweli na uwezo wa kupata sehemu ya uwezo wa kijini inawezekana kabisa lakini inahitajika siku 28 kamilifu ambayo ni idadi ya mzunguko wa mwezi na kila siku Kuna ya kufanya hapa unafungua kuna vitu kupata flow of energy kikamilifu.
 
Allah akusaidie umalize kwakweli mana kwa uzoefu wangu wa kusoma ilmu za namna hii humu asilimia kubwa hua hawamalizi na sababu nlishazisema huko juu
* Ubinafsi mbaya sana wa watu , wanataka wao tu ndio wajue na wanaitumia kuwachaji watu pesa nyingi kuwasaidia matatizo yao

*Kugusa Siri flan ambazo Hawataki wengine wajue japo katika falme yako umeruhusiwa kuongea ..mwisho kabisa hufuatwa kuambiwa waache kusimulia. Wengine huanza kuleta mambo ya udini. Kuna sehem najua ukifika tu wataanza kuja...saiv ni kama wamekaa attentive mode..
sema unacho nena nichakwel kabis aviola mm naona wanakuw na tabia za kutulambisha asali alafu badae wanatulisha sumu kwa kudhani ni asali kumbe ndo wanatutoa kafal hvyoo....
 
Yaani mi nikuonee wivu we maskini, mashamba na limbukeni? Nimeanza kubalehe 1990 na nikeshaona kila aina ya mwanamke na pia nina watoto kama wewe.

Hayo masuala ya ngono unayofanya yalikuwa na umuhimu gani kutueleza watu wasiohusika wala wasiokujua tena kwenye uzi usiohusiana na ngono?

Inawezekana we dogo ni punga na ndio maana una pretend kuwa kidume. Alafu acha ushamba, kwa ulimwengu wa sasa hakuna anayejivunia umalaya. Watu tunajivunia pesa.

Maskini na gasho mkubwa.

Pumbavu. Usiwe unatukana watu. Mi Baba yako.
Msigombane kaka mambo kuvumiliana binaadamu wote ni sawa hivyo kuvumiliana tuu
 
sema unacho nena nichakwel kabis aviola mm naona wanakuw na tabia za kutulambisha asali alafu badae wanatulisha sumu kwa kudhani ni asali kumbe ndo wanatutoa kafal hvyoo....
Hapana, watu wema wa kusema haya wapo kama mleta mada...ninaowazungumzia ni ambao wakiona mtu anatoa elimu wanakuja ku disturb , sababu hawataki watu wajue kweli ...kifupi kwa lugha tafsiri matajiri hua hawapend maskin ajue njia ya kua tajiri ili wao wawe wachache na maskin wawe wengi ili wawe chawa na vijakazi..umeelewa..
 
hapo nimekupat vizur sanaa
 
Back
Top Bottom