Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Hii ni ukweli na uwezo wa kupata sehemu ya uwezo wa kijini inawezekana kabisa lakini inahitajika siku 28 kamilifu ambayo ni idadi ya mzunguko wa mwezi na kila siku Kuna ya kufanya hapa unafungua kuna vitu kupata flow of energy kikamilifu.
Ni vitu gani vya kufanya ili uwe na uwezo wa kijini
 
Hii ni ukweli na uwezo wa kupata sehemu ya uwezo wa kijini inawezekana kabisa lakini inahitajika siku 28 kamilifu ambayo ni idadi ya mzunguko wa mwezi na kila siku Kuna ya kufanya hapa unafungua kuna vitu kupata flow of energy kikamilifu.
siku 28 why that days?
 
Simulizi ya kweli inayonihusu mimi mwenyewe moja kwa moja.
Sehemu ya kwanza .

1. Namna majini walivyoshiriki katika makuaji yangu .
Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikishuhudia vivuli vilivyokuwa vikinifata kila nilipokwenda, kiukweli nilikuwa nikiogopa sana ingawa nilikuwa simwambii mtu yeyote hata mama na baba .

Siku zilizidi kwenda na kila siku nilikuwa nikijionea mambo mapya na hadi kufikia wakati nilikuwa nikiona watu wenye ndevu nyingi nyeupe, mavazi maupe sana waliokuwa wakinifata nyuma ninapotembea. Ndani ya kundi la watu hao kulikuwa na watoto waliokuwa sawa sawa na umri wangu kwa kipindi kile na kulikuwa na wanamama waliokuwa wakijitanda mavazi marefu ya kuburutika hadi chini .

Kiukweli nilikuwa nikijionea mambo mengi hadi ilifika wakati ninapopita mazingira ya hatari basi wazee wale hutokea ghafla na kunizuia kupita au kubaki maeneo hayo .

Siku moja nilipokuwa kijijini kwa kina bibi niliondoka na watoto wenzangu hadi mtoni (kisimani) , lakini ghafla tulipokuwa kando ya kisima hicho niliteleza na kuingia kisimani.

Mawasiliano yangu na wenzangu yalipotea lakini kwa mbali sana nilisikia kelele zao za kutaka kuniokoa bila mafanikio.

Nilizama hadi chini ya kisima nasikuwa najua kuogelea kamwe.

Nilitapatapa sana bila matumaini lakini ghafla nikamuona mzee mwenye ndevu nyingi nyeupe, kanzu na kitambaa cha kijani na pete kidoleni alitokea na kunishika mkono . Usoni sikumuona vizuri lakini alionekana kufurahi kuniona. Alinishika sana eneo la kichwani na kifuani huku akiniangalia kwa umakini mkubwa.
Nilimuona akipuliza kiganja chake cha mkono wa kulia na kisha kunifuta kwa mkono ule mwilini kisha alinisogeza hadi kando ya kisima na kuniweka kando nje ya kisima.
Halafu baada ya ndoto kuisha ulijisikiaje kuwa kumbe ilikuwa ndoto
 
Huyu ni jini mwanamke ni msomi mzuri sana na ana uwezo mkubwa sana anayo misafara mikubwa ya biashara nasaba yake ni kubwa sana ukoo wake ni wenye mali ni mzuri vilevile.
Haya ni machache kuhusu yeye
Kuna jamaa humu alileta uzi kuhusu Arsis alisema ni mwanaume.
UZi unaitwa "niliyoyaona baada ya kufunguliwa macho" mtoto wa mzee mabruk
 
Halafu baada ya ndoto kuisha ulijisikiaje kuwa kumbe ilikuwa ndoto
Sio ndoto kama unavyofikiri wewe , na vile vile hata ingekuwa ni ndoto bado ni sehemu ya msingi ni wakati ambao macho yanapofumba roho hutoka na kwenda kushuhudia ambayo ukiwa kwa miguu huko huwezi fika kwa haraka.
Endelea kujifunza hapa tafadhali
 
Kuna jamaa humu alileta uzi kuhusu Arsis alisema na mwanaume.
UZi unaitwa "niliyoyaona baada ya kufunguliwa macho" mtoto wa mzee mabruk
Ni jina tuu huwenda ikawa jini wake yeye alikuwa na jina hilo sababu baadhi ya nyakati hutumia jina lao la ukoo hawa viumbe. Kwahiyo niliepata kusikia ana jina hili alikuwa ni mwanamke kama nilivyopata kuambiwa na Rauhiyah
 
hapo inategemea ukiwa wa kiume utamuoma aries wa kike na ukiwa wew mwanamk utamuona wa kiume...
Hahaha hivyo jin jinsia yake inabadirika kutegemea na jinsia ya mtu. Ukiwa mwanaume jini huyo huya ana kuwa wa kike, na ukiwa mwanamke hilo hilo jini linakuaa la jinsia ya kiume.
 
Muendelezo.

Basi pale ikafanyika kitu mfano wa maulid lakini pakapita tangazo kuwa anasubiriwa sayyid wa Zanzibar ( huyu nitakuja kumzungumzia mbeleni mwa kisa hiki ) . Haikupita muda nilichukuliwa na kuwekwa katikati nikazungukwa duara na wazee walioonekana kuwa ni wasomi wazuri wa dini walikaa karibu na mimi na kuna maneno waliyokuwa wakisema ila sikuwa nayafahamu. Mzee yule niliyekuwa nimemuona tangu kisimani alitoa amri ya kuwaambia wengine kuwa sasa inatosha mrudisheni kijana umbali wa Iran na Tanga sio mkubwa sana lakini piteni na Yemen.
Basi mambo yalifanyika haraka sana nashindwa kuelezea sababu yote haya yalipokuwa yakiendelea sifikiri kama yalimaliza hata nusu saa , sababu mpaka kurudishwa tena nyumbani niliona dada Aisha yupo anamalizia kupanga vyombo tulivyotumia kula chakula.

Sasa pale Yemen nilioneshwa hospital kubwa ya kitiba ambayo majini hutumia. Na nilioneshwa mti wenye kutibu mambo mengi sana. Huu mti unafanana sana na miti Fulani inaota kwenye majabali . Same Kilimanjaro niliiona mingi sana kipindi nipo masomoni. Karibu na kituo cha shule inaitwa kirinjiko hii miti ipo mingi sana.
Mti huo ni miongoni mwa miti inayotumika kuunda shajarat al jinn ( nitakuja kuielezea huko mbeleni) .
Pale Yemen huu mti upo juu ya jiwe kubwa sana lakini kulikuwa na kitu mfano wa nyoka mkubwa juu yake .
Bora hata mwanzo ilikuwa dizaini ya mchaichai nzuri kwa afya, ila hapa ilipofikia nikasema dah hawa malenga yoo, malenga wapyaaa hii chai ni super kibena jani limekolea
 
hapo inategemea ukiwa wa kiume utamuoma aries wa kike na ukiwa wew mwanamk utamuona wa kiume...
Hiyo ni story ya jamaa mmoja anasema yeye ni ukoo wa Simba, alikuwa anapendwa na huyo Jin mkuubwa sana mwenye nguvu kuliko majini wengi anaitwa ARSIS, msome humu yumo JF.
Ukienda kwenye JF search uka type Arsis utauona uzi unaitwa " "niliyoyaona baada ya kufunguliwa macho"
 
Anhaa nitafatilia lakini nimeshtuka kidogo kusikia ukoo wa Simba ni mtu wa wapi huyo mtu?
 
Hahaha hivyo jin jinsia yake inabadirika kutegemea na jinsia ya mtu. Ukiwa mwanaume jini huyo huya ana kuwa wa kike, na ukiwa mwanamke hilo hilo jini linakuaa la jinsia ya kiume.
sio hvyo mkuu unaposema jini aris au yoyot haimaanish kwamb atakuw wa jinsia moja tu let say jini mahaba ukiwa wa kiume anakuja dume kukugegedua wew au kam atakuw jin wa kike utamgegedua lakin wote hawa wanajulikan kam jini mahaba haijalish wa kike au kiume hapo umenipat mkuu
 
Back
Top Bottom