Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Pia ni ishara ipi nitajua sehemu nilipo kunajini
Mwili utabadilika na kuwa na hali fulani ya moyo kwenda mbio sana na kupata hali ya kukosa utulivu wa nafsi na mara nyingine wakiamua kukuonesha vibweka utapata kuona vivuli na watu huwaoni. Vinyweleo kusimama kuliko kawaida na kama ni shetani akikuingia utahisi baridi na utosi wa kichwa kuvuta sana kifupi ni hayo ila yapo mengi.
 
Je mwanadamu wa kawaida apitie atua ipi awe na sehemu fulani ya uwezo wa kijini
Kwanza kuepukana na woga kisha kuna kitu kinaitwa hateyn tariqa ( njia mbili) kuzifungua.
Hizi ni njia maalum ni mfano wa mistari minyoofu miwili mmoja ni mweupe na mwingine ni mweusi na kila mmoja una kazi yake . Sasa huu mweupe lazima ufunguliwe ujae nguvu na hapo huyo binaadamu anakuwa na uwezo wa kiroho mkubwa sana.
Na kuufungua huu ni ndani ya zile siku 28 nilieleza katika swali lako la awali
 
Mkuu naomba kujulishwa, mwonekano wa jini upoje?
Huweza kuonekana kwa namna tofauti tofauti kama ifuatavyo.
1. Moshi mwembamba
2. Mwili wenye kichwa tuu
3. Muonekano wa mwili wenye misuli mikubwa
4. Muonekano wa kama unavyoangalia television yaani yeye yumo ndani ya kioo na wewe unatazama na kusikia anachosema
5. Na muonekano wa binaadamu kamili
Na zaidi ya hii niliyotaja.
Nb: Muonekano wa mapembe kichwani hawa ni shetani huwa na muonekano huu .
 
Buraq Mustapha

1.Kitu gani majini hayataki?
2. Wafuasi wa Imani ipi si rafiki wazuri wa majini?
3. Kuna uwezekano wa kuwa na jini na bado usijitambue?
Jini anaweza kuwa na mtu yeyote bila kuzingatia dini , ingawa kadiri unavyokuwa na ahlaki njema ndio wanavyozidi kuvutiwa na wewe .

Kitu wasichotaka kabisa ni kuwakashifu na kuingilia uhuru wao .
Ndio unaweza kuwa na majini na usitambue mpaka siku unakufa
 
Wazee wenye nywele na ndevu nyeupe si wanapandaga basi la simba...🙂ikawaje sasa huko?
eti bwana mganga😄?
 
Back
Top Bottom