Buraq Mustapha
JF-Expert Member
- Jul 13, 2021
- 228
- 561
- Thread starter
- #301
Basi baba alipokea ile pesa na kuiweka mfukoni mwake lakini nilimwambia kuwa pesa ile asiitumie wala kwenda maduka ya kubadilisha fedha aiache hadi baada ya siku saba na sikumwambia sababu.MUDA UMEWADIA TUNAENDELEA.
Basi baba alinisimulia kile alichokiota na kuniuliza nini maana yake. Kwa kuwa mzee Ruhaby alinambia nimwambie kila kitu basi nilimwambia baba kuwa ile sio ndoto ni uhalisia, mwili wake ulibaki kitandani lakini nafsi ilifika mbali .
Na hapo nilimwambia ukweli wote kuanzia kwenye kusima siku ya kwanza kumuona yule mzee hadi siku ile aliyokuja pale nyumbani na mengi kuhusu silsila ya babu yaani baba yake baba yangu.
Baba hakushtuka sana sababu tayari kwenye ndoto alishaelezwa ukweli kamili hivyo mimi nilikuwa nikiongezea tuu .
Ni kama mimi nilikuwa mbele ya muda kufahamu mambo ya majini na kushirikiana nao ila yeye baba alichelewa kujua kuwa hata babu yaani baba yake alikuwa ni swahiba wa majini na alipofariki viumbe wake walikuwa wakihitaji mrithi ili kuendeleza silsila ya ushirikiano baina yao na familia kwaujumla.
Kwa siku ile baba nilikuwa nae muda mrefu sana pale chumbani nikimwambia mambo mengi sana yaliyowahi kutokea ndani ya familia tangu wakati wa babu mpaka kufikia kuzaliwa kwao na mengi yaliyokea kipindi sikuzaliwa hivyo baba alibaki kuuliza na kushangaa tuu.
Nilimwambia namna ambavyo babu alivyokwama ndani ya jahazi na shangazi takribani siku saba wakitokea unguja.
" Siku moja baba yule mzee Ruhaby alinambia kuhusu kukwama kwa babu na shangazi baharini takribani siku saba wakiwa na abiria wengine wakitokea unguja na hapo babu alimuomba Mungu msaada kisha akamuita baba yake mzee Ruhaby kuwatoa pale walipokwama, na hapo baba yake mzee Ruhaby alikuja na jeshi kubwa la majini na kusukuma jahazi kwa kasi sana hadi ufukwe wa bahari kigombe, lakini alitoa sharti moja kuwa watu wasigeuke nyuma na yeye mwenyewe alikaa nyuma kabisa ya jahazi..." Nilimwambia baba na kisha yeye kukiri hii dhoruba ilitokea na kipindi hicho nilikuwa sijazaliwa bado.
Muda sio mrefu nakumbuka baba alikwenda kuchukua kile kitabu alichopewa na mzee Ruhaby kukifungua kurasa kadhaa kulikuwa na maneno yaliyosomeka
" Bismillah almuhitw aldayimu alqadim aladhiy malag'hsutwiqh nuri wajhih alq'kwan wag'hmdaha biquwat jadhbatihi ana hayhut sultwan, g'halay kul malik wajin wainsay washaytwan wasultwan fakhafituh jamia makhluqatih waadhinat watawadat alkarubiuwna............ mwisho kukawa na wa almalaaykatu wa asyad alruhaniaty... Jibril, mikail, israfil, izrail "
Kisha baada ya hapo kukawa na majina haya baalshaqish, mahraqish, aqshamaqish, shaqmunhish, Raksha, kashlakh, a'kish na twahish.
Baba aliendelea kufunua kile kitabu kidogo hivi jalada la ngozi hadi kuna ukurasa kulikuwa na pesa ya karatasi mpya yenye kunukia sana .
Hapo baba aliacha kufunua na kuniuliza maneno yaliyoandikwa na majina yale nane ni nini ? Nilimuelezea kuwa majina nane yalikuwa ni tahatil yanaitwa na yale maneno yalikuwa ni maneno ya wito wa kuita kila kiumbe kikujie iwe ni jini, shetani au binaadamu, awe mfalme au vyovyote aje na kutii wito na majina ya malaika mwisho mwa maneno yale ni wasimamizi wa ilmu ambayo imo ndani ya kitabu kile .
Naomba niwaambie kuwa maneno yote yaliandikwa kiarabu na ndio mara yangu ya kwanza kuona kitabu kile ukizingatia na umri wangu lakini niliweza kumjibu baba maswali yake yote .
Ile pesa nakumbuka baba alinambia nikae nayo mimi lakini kupitia nafsi nilipata hisia kuwa nimwambie akae nayo yeye ili uchumi ufunguke zaidi aweze kuhudumia familia vizuri mimi bado ni mdogo .
Sasa hapo nikawa rasmi mwalimu wa baba yangu na kwa mara ya pili majini walishiriki kumfungua macho mtu wa pili baada ya dada sasa ni baba yangu nae swahiba wangu wa kijini wakina mzee Ruhaby na wenzie wanamfungua na kumuweka karibu.
Swala ya alaasiri nakumbuka tuliswali pale nyumbani na baada ya swalat tukabaki wote chumbani kwangu pale, na hapo nilimwambia baba asome suratul yaasin na suratul jinn kuweka sawa mwili baada ya nafsi yake kutoka muda mrefu kwenda kushuhudia mambo na alienambia nimwambie ni mzee Ruhaby japo kwa muda ule pale chumbani hakuja lakini sauti yake niliisikia.
Na hata kuhusu ile pesa kuwa asiitumie hadi baada ya siku saba ni yeye mzee Ruhaby ndio alinambia nimwambie na mara hii alinambia kuwa anataka afanye kitu kwaajili ya baba yangu mimi sikujua ni kitu gani na sikumuuliza sababu nisingeweza kuongea na yeye huku naongea na baba .
Lakini alinipa maelekezo ya kumfanyia baba baada ya swalat magharibi kuna kiasi chake cha pesa kingi tuu kwa watu wake anaodai atalipwa na atapata safari nyingine ya dar es salaam kuchukua pesa nyingi tuu.
Hapo sikuwa najua kama baba kuna watu anawadai pesa nyingi na hawataki kumlipa au wanamzungusha kumpa, hivyo ilibidi nimuulize baba vizuri na kisha alikiri kusema anakaribia hadi kukata tamaa juu ya kupata pesa hizo . Na kuhusu dar es salaam nako alisema hana matumaini maana keshaahidiwa sana .
Baaada ya maongezi mengi na mengi magharibi ilifika na baada ya swalat kumalizika mzee Ruhaby alinambia kuwa nichukue bakuli la maji, niweke ile pesa niweke ubani na udi na matone ya asali na niende kule kwenye mkuyu kuna kitu kitadondoshwa kutoka juu niokote niweke, sasa kwakuwa muda ulienda sana ikabidi nimwambie dada Aisha aende kukileta.
dada alienda kilianguka kitu kinawaka sana dada aliokota na kuja nacho kabla ya kuona ni nini nilifahamu kuwa ni ua la mkuyu.
Basi nilichanganya vizuri vile vitu huku nikipata maelekezo muhimu kwa mfumo wa sauti yake mzee Ruhaby.
Kuna maneno kadhaa alinambia nifatishe kusema, nilisema maneno na kisha akanambia nimpe baba yake maji anawe mikono na kuosha uso yaani afanye kama mwenye kuweka udhu ila abakishe mengine ataoga kidogo na mengine asubuhi atatumia muda sio mrefu ataitwa akachukue pesa .
Baada ya zoezi kukamilika tuliingia ndani muda wote baba yupo kimya tuu ni kama mtu anaeshangaa kuona nafanya mambo ambayo yeye mwenyewe hayajui wala hajawahi kuyaona sehemu.
Lakini tulipoingia ndani mama alikuwa akisema kuwa karibu na jikoni amepishana na mtu amevaa kanzu lakini hana uhakika kuwa ni kweli au ni macho tuu yamemdanganya.
Nakumbuka baada ya zoezi lile baba alitoka na kile kitabu kuingia chumbani huku yale maji akiondoka nayo nikamwambia ayaweke mvunguni mwa kitanda .
Mimi nilibaki chumbani kwangu tuu pale na haikuchukua muda mrefu kaka zangu waliingia wakitokea kwenye biashara na kuniuliza baba yuko wapi .
Walimpatia salamu kuwa wamekutana na mzee Othman kesho aende wakaongee na huyu mzee Othman ni mzee ambae anadaiwa na baba pesa nyingi tuu . Nilishangaa na sikutaka kuamini kuwa kile tulichofanya tayari kimetoa jawabu kabla ya usiku kumalizika.
Asubuhi kuamka kulikuwa na mvua sana ikawa vigumu kutoka kwenda masjid badala yake tulikaa sebleni na ibada ya alfajir tulifanya pale pale nyumbani.
Kisha nikamuacha baba akifanya nyiradi mimi sikuweza nilirudi chumbani kulala sababu usiku sikulala vizuri sababu ya mawazo ya rafiki yangu abushiri alikuwa akiumwa sana .
Nililala sana hadi nilipokuja kuamshwa kwaajili ya kifungua kinywa, baada ya kula nikarudi tena chumbani na haikuchukua muda nilimsikia baba akisalimiana na mtu pale sebleni, nilitoka nilijuwa rafiki yake sheikh Yusuf.
Ni yule mzee Othman alikuwa na amekuja yeye mwenyewe kumpa baba fedha zake na alisema kuwa usiku mzima hakulala na alitamani asubuhi ifike haraka aonane na baba ampe pesa zake moyo ulikuwa ukimuuma na kujiskia vibaya kukaa na pesa za mtu muda mrefu.
Baba alipokea tuu pesa na kuzihesabu na mzee yule hakukaa sana aliondoka.
"Deni lilikuwa la muda mrefu sana lakini sasa limelipwa lote kikamilifu mola wangu nakushukuru " baba alisema na kuondoka kuingia chumbani na ule mfuko wa pesa .