Asalaam alykm...
Napenda na nimevutiwa na unavyojibu maswali yetu kwa unyenyekevu mkubwa na kwa busara kabisa... Nahisi anayetujibu ni huyu jin mwema! Au la kama ni wewe basi sishangai watu wanaokutembelea na ukatatua shida zao.
SWALI LANGU
Je mwenyezi Mungu, ameruhusu tushirikiane na hawa majini wema? Kama ndivyo kwa nini tumeaminishwa kwenye baadhi ya dini hizi za kizungu kuwa majini ni mashetani na pepo wachafu, kiasi kwamba tukisikia jini unajua ni jitu haribifu tu?
Asante mengi nitakuja inbox.