Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Ulimwengu wa majini na mambo niliyoshuhudia na kujifunza kwao

Kwahiyo ndgu Buraq Mustapha majini wana miili kama sisi?? Wana maumbo kama yetu kila kitu?

Na vipi hizi vita wao haziwaathiri? Au wao vita za binadamu haziwahusu??

Na kwanini wao wanakuja kwetu kiholela kama hivyo halafu kwenda kwao sheria nyingi?
Kwanza hakuna mtu amekatazwa na majini kufika kwao ni swala la uwezo na maarifa tuu.
Vita za binaadamu wao haziwaathiri serikali yao haina migogoro kama za binaadamu. Wao Wana uwezo wa kujibadili katika umbo lolote
 
Kwanza hakuna mtu amekatazwa na majini kufika kwao ni swala la uwezo na maarifa tuu.
Vita za binaadamu wao haziwaathiri serikali yao haina migogoro kama za binaadamu. Wao Wana uwezo wa kujibadili katika umbo lolote
Je mabomu mazito mazito yanayotupwa na wanadamu katika vita je hayaathiri makazi ya majini
 
MUDA UMEWADIA TUNAENDELEA.
Basi baba alinisimulia kile alichokiota na kuniuliza nini maana yake. Kwa kuwa mzee Ruhaby alinambia nimwambie kila kitu basi nilimwambia baba kuwa ile sio ndoto ni uhalisia, mwili wake ulibaki kitandani lakini nafsi ilifika mbali .
Na hapo nilimwambia ukweli wote kuanzia kwenye kusima siku ya kwanza kumuona yule mzee hadi siku ile aliyokuja pale nyumbani na mengi kuhusu silsila ya babu yaani baba yake baba yangu.
Baba hakushtuka sana sababu tayari kwenye ndoto alishaelezwa ukweli kamili hivyo mimi nilikuwa nikiongezea tuu .
Ni kama mimi nilikuwa mbele ya muda kufahamu mambo ya majini na kushirikiana nao ila yeye baba alichelewa kujua kuwa hata babu yaani baba yake alikuwa ni swahiba wa majini na alipofariki viumbe wake walikuwa wakihitaji mrithi ili kuendeleza silsila ya ushirikiano baina yao na familia kwaujumla.

Kwa siku ile baba nilikuwa nae muda mrefu sana pale chumbani nikimwambia mambo mengi sana yaliyowahi kutokea ndani ya familia tangu wakati wa babu mpaka kufikia kuzaliwa kwao na mengi yaliyokea kipindi sikuzaliwa hivyo baba alibaki kuuliza na kushangaa tuu.
Nilimwambia namna ambavyo babu alivyokwama ndani ya jahazi na shangazi takribani siku saba wakitokea unguja.
" Siku moja baba yule mzee Ruhaby alinambia kuhusu kukwama kwa babu na shangazi baharini takribani siku saba wakiwa na abiria wengine wakitokea unguja na hapo babu alimuomba Mungu msaada kisha akamuita baba yake mzee Ruhaby kuwatoa pale walipokwama, na hapo baba yake mzee Ruhaby alikuja na jeshi kubwa la majini na kusukuma jahazi kwa kasi sana hadi ufukwe wa bahari kigombe, lakini alitoa sharti moja kuwa watu wasigeuke nyuma na yeye mwenyewe alikaa nyuma kabisa ya jahazi..." Nilimwambia baba na kisha yeye kukiri hii dhoruba ilitokea na kipindi hicho nilikuwa sijazaliwa bado.

Muda sio mrefu nakumbuka baba alikwenda kuchukua kile kitabu alichopewa na mzee Ruhaby kukifungua kurasa kadhaa kulikuwa na maneno yaliyosomeka
" Bismillah almuhitw aldayimu alqadim aladhiy malag'hsutwiqh nuri wajhih alq'kwan wag'hmdaha biquwat jadhbatihi ana hayhut sultwan, g'halay kul malik wajin wainsay washaytwan wasultwan fakhafituh jamia makhluqatih waadhinat watawadat alkarubiuwna............ mwisho kukawa na wa almalaaykatu wa asyad alruhaniaty... Jibril, mikail, israfil, izrail "
Kisha baada ya hapo kukawa na majina haya baalshaqish, mahraqish, aqshamaqish, shaqmunhish, Raksha, kashlakh, a'kish na twahish.
Baba aliendelea kufunua kile kitabu kidogo hivi jalada la ngozi hadi kuna ukurasa kulikuwa na pesa ya karatasi mpya yenye kunukia sana .

Hapo baba aliacha kufunua na kuniuliza maneno yaliyoandikwa na majina yale nane ni nini ? Nilimuelezea kuwa majina nane yalikuwa ni tahatil yanaitwa na yale maneno yalikuwa ni maneno ya wito wa kuita kila kiumbe kikujie iwe ni jini, shetani au binaadamu, awe mfalme au vyovyote aje na kutii wito na majina ya malaika mwisho mwa maneno yale ni wasimamizi wa ilmu ambayo imo ndani ya kitabu kile .
Naomba niwaambie kuwa maneno yote yaliandikwa kiarabu na ndio mara yangu ya kwanza kuona kitabu kile ukizingatia na umri wangu lakini niliweza kumjibu baba maswali yake yote .
Ile pesa nakumbuka baba alinambia nikae nayo mimi lakini kupitia nafsi nilipata hisia kuwa nimwambie akae nayo yeye ili uchumi ufunguke zaidi aweze kuhudumia familia vizuri mimi bado ni mdogo .
Sasa hapo nikawa rasmi mwalimu wa baba yangu na kwa mara ya pili majini walishiriki kumfungua macho mtu wa pili baada ya dada sasa ni baba yangu nae swahiba wangu wa kijini wakina mzee Ruhaby na wenzie wanamfungua na kumuweka karibu.
 
Back
Top Bottom