Ulimwengu wa Scania unaisha. Zuchu Howo ndio mpango mzima

Naipenda sana Howo navutiwa na kule mbele kulivyo kama ndege vile siti ukikalia utasikia inasonya hadi raha
 
Kwenye logistics industry hatufungi ndoa na gari thus chines is the best likirudisha faida tu unamuuzia mtu akafe nalo
 
Kwa biasharaa ya mabus ya abiria bado Mchina ni the best anarejesha pesa haraka sana kuliko scania.
Ni kweli mkuu sikatai,...


Ila wachina watupunguzie utani kwenye hii biashara ya mabus, Kweli kabisa mtu uko serious na fedha zako....

ununue basi inaitwa Zuchu!!!.... seriously! Kweli!!? Meen!
 
Kweli!!? Meen!
Unaangalia faida ya fasta,Marcopolo moja unapata Mchina 2 plus 1 ya mkopo utalipa kwa dhamana ya hizo 2.
Wote level siti scania abiria 60 kwa milion 500, mchina bus tatu abiria 180 kwa hio 500 nauli Mwanza au Mbeya elf 50.
So scania utapata milion 3, mchina utapata milion 9 kwa mtaji wa milion 500.
Mchina atarejesha pesa haraka sana kuliko scania.
Ishu za kukaa na magari miaka hadi mjukuu anarithi ni ya kizamani hata Ulaya hawafanyi.
Gari ikirejesha faida uza ingiza ingine
Ukitaka comfortability chukua mchina ukitaka durability chukua scania.
Kwa transit chukua scania kwa local na tipper chukua mchina,kwa porini anapopita Howo scania apiti.
Kazi zote za site na contract ishu za tipper Mchina the best
 
Acha kufananisha Scania na takataka za kichina.mchina akipiga kazi ngumu miaka miwili tu imeoza wakati Scania aliyonunua babu mpaka mjukuu analikuta na anakuja kuliacha.
 
Mkuu umeenda shule , achana na hawa watu wa Scania wanangangania ma 113 or zinadumu , hawajielewi kabisa
 
Acha kufananisha Scania na takataka za kichina.mchina akipiga kazi ngumu miaka miwili tu imeoza wakati Scania aliyonunua babu mpaka mjukuu analikuta na anakuja kuliacha.
Hello bosses and roses...

Humu watu baadhi wananijua kama computer programmer ila mie ni fundi magari pia. Kiukweli hizi gari za MAN wamejitahidi sana upande wa umeme, wiring iko organized vizuri mno, ukichukua MAN moja na trucks za makampuni mengine zenye range sawa ya bei basi utakuta MAN iko organized vizuri kuzidi hao wengine.

Kwanza kwenye MAN kila waya una namba yake, maboya yote yana ID pia. Hizi gari nyingi za siku hizi kuna miwaya mingi sana, ila wengi hawana mpangilio mzuri kama uliopo kwenye MAN hivo kufanya troubleshooting kuwa ngumu. MAN bila hata kuwa na wiring diagram unatengeneza.

Ila tukija kwa ndugu zetu scania aisee ni kichefuchefu, tena hizi zilizopo humu nchini nyingi kupiga shoti gari zima ni kawaida. Kwa uzoefu wangu kesi za truck kupiga shoti gari zima zinaongozwa na scania, ngoma inapiga shoti hadi main fuse box yote haitamaniki. Hii ni kwa sababu hizi gari organization yake ya wiring ni ya hovyo sana, fundi akigusa akachanganya kdg basi ni shida tayari, kwa MAN ni ngumu sana kuchanganya labda uwe hujui kabisa unalofanya
 

Acha uongo hizo gari kauza muda mrefu sasa hivi ni youtong tuu
 
Kila Transporter anataka aanze na truck mpya, hizo Chinese trucks wengi wanaonunua mpya nyingi ni Big companies.

Scania used ndio kimbilio la wanaoanza biashara ya usafirishaji kutokana na gharama ya ununuzi, Howo na Faw tractor trucks bei ni usd 54000 mpaka 56000 ( wastani wa tzs 125million mpaka 135m). Wakati Scania tractor head used ya 2010 ya south unapata kwa 75m mpaka 80m pesa inayobaki unanunua trailer mpya au used na kufanya process ya vibali vyote gari inaingia barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…