PostGE2025 ‘Ulipata’ kura zaidi ya milioni 31 lakini leo umejificha

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mabeberu wapo kundi moja na hao hao Wakenya. Majirani zetu wanawahifadhi wanaharakati hata zile vurugu za October 29 upo uhusika wa Kenya kwa kiasi kikubwa.

Ngumu kwako kuamini lakini ndio ukweli wenyewe, alipozuiliwa Mange asitumie mtandao wa whatsapp akashindwa kusababisha vurugu tarehe 9 Desemba, njaa inaweza kuwepo lakini pia kuna msukumo unaoletwa na vita za kiuchumi.

Sisi sio wa kwanza kwa vijana kusababisha vurugu lakini nyuma yake zinakuwepo shilingi elfu hamsini wanazopewa katika mgao wa mashirika ya kibeberu yenye nia mbaya na taifa husika.

Siamini kwamba nchi ya Afrika ina watu wenye kudhani ni muhimu sana kufanya siasa huku wakiziacha fursa za kiuchumi zikawatajirisha watu wa mataifa mengine. Hayati JPM alipiga marufuku siasa na tukajikita kwenye ujenzi mkubwa wa taifa.

Samia ameruhusu siasa kwa maana ya mikutano, hao walioruhusiwa ndio hao waliojiapiza kwamba uchaguzi hautafanyika na watakinukisha, kama zisingekuwa zile risasi wapuuzi wale walikwisha iharibu kabisa Tanzania.

Hao vijana wenye kufahamu mambo ndio hao hao waliodanganywa na Mange kwamba nyinyi ingieni barabarani wanajeshi watawakuta huko huko mkiwa katika michakato ya kupindua nchi!. Hao vijana wenye uelewa ndio hawa wasiojua masuala mengi ya kawaida tu ya kimaisha.

Tanzania ina kila aina ya fursa za kiuchumi, ukiiweka akili yako katika kutaka kuzifahamu utatajirika vizuri tu lakini ukiiweka akili yako ikawa kituo cha kuupokea uchochezi kutoka kila kona ya dunia hautakuja kuzifahamu hizo fursa utaishia kuwa mwanaharakati unayesubiri amri za kipuuzi kutoka kwa Mange na Maria Sarungi.
 
Nyie diaspora wajinga sana huwa nikiwasikiliza nawaona Kama wapumbavu kukaa mtoni kote ila no exposer
 
100%
 
Mabeberu wapo kundi moja na hao hao Wakenya. Majirani zetu wanawahifadhi wanaharakati hata zile vurugu za October 29 upo uhusika wa Kenya kwa kiasi kikubwa.
Nimekuuliza ushahidi upo wapi? Hakuna jibu lakini unataka watu waamini Kenya wanahusika
Nimekuuliza yule Mwanajeshi wa Kenya kashtakiwa mahakama gani? Hujui lakini unaaminisha watu alikuja kufanya vurugu.


Nimekupa sababu zaidi ya 5 zilizoamsha hisia na hasira za Wananchi kwa maneno yao , huja 'rebuttal'' hata moja
Je, si kweli kwamba Wananchi wanalalamika utekaji na kutoweka kwa watu?
Je, si kweli kwamba vyama vya siasa kupitia Mahakama, vimezuiwa kufanya shughuli ?
Je, si kweli kwamba Viongozi wa Upinzania wapo magereza na Oct 29 wote walikuwa mahabusu
Je, si kweli kwamba kuna lalamiko la ufujaji na matumizi ya fedha za umma yanayolalamikiwa?
Je, si kweli kwamba Wananchi wanalalamika kuhusu chaguzi za kupanga?
Je, si kweli kwamba kuna mgogoro kati ya serikali na taasisi za dini?

Katika hayo, mkono wa Kenya upo wapi?
Ngumu kwako kuamini lakini ndio ukweli wenyewe, alipozuiliwa Mange asitumie mtandao wa whatsapp akashindwa kusababisha vurugu tarehe 9 Desemba, njaa inaweza kuwepo lakini pia kuna msukumo unaoletwa na vita za kiuchumi.
Kuna vita ya uchumi kati ya Tanzania na nchi gani? Sisi tunaweza kumtisha nani kiuchumi.
Kaangalie GDP ya Kenya, Budget yao na yetu kisha ujiulize ni ushindani au vita? Hakuna vita na fukara!
Sisi sio wa kwanza kwa vijana kusababisha vurugu lakini nyuma yake zinakuwepo shilingi elfu hamsini wanazopewa katika mgao wa mashirika ya kibeberu yenye nia mbaya na taifa husika.
Hakuna ushahidi wa maelfu kupewa pesa. Yaani utoe pesa kwa maelfu bila kujulikana! impossible
At least kwa sasa tungeshasikia hilo.
Siamini kwamba nchi ya Afrika ina watu wenye kudhani ni muhimu sana kufanya siasa huku wakiziacha fursa za kiuchumi zikawatajirisha watu wa mataifa mengine. Hayati JPM alipiga marufuku siasa na tukajikita kwenye ujenzi mkubwa wa taifa.
Hizi ni internal strife hazina uhusiano na nchi za nje. Wazungu wakitaka rasilimali tutawapa tu! hawana haja ya kuchochoea vita. Majuzi Waziri Kabudi akihojiwa na Al Jazeera alisema '' Rais amekutana na Kaimu balozi wa USA na kumhakikishia kuhusu uwekezaj wa US nchinii''. Wakitaka wanachukua , sisi ni fukara wa akili !

Yes kuna fursa za kutajairisha watu, jiulize miaka 64 ya Uhuru CCM ndicho chama kimeunda serikali, kwanini hadi leo sisi tupo kundi la nchi masikini! Tatizo sidhani ni Wananchi, nani anawaongoza inaweza kuwa.
Unachokiona ni kukataliwa kwa CCM ingawa kuna denial lakini nyuma ya pazia mnajua hilo.
Samia ameruhusu siasa kwa maana ya mikutano, hao walioruhusiwa ndio hao waliojiapiza kwamba uchaguzi hautafanyika na watakinukisha, kama zisingekuwa zile risasi wapuuzi wale walikwisha iharibu kabisa Tanzania.
Mikutano na shughuli za siasa zimeanishwa katika Katiba, ni HAKI si fadhila. Hakuna anayetoa ruhusa Katiba inapotamka. Hao waliosema watakinukisha wapo jela tangu March, na mwingine alikamatwa bila kosa
Waliotoka ni Wananchi , lazima mkubali ukweli.

Well, Mange ana nguvu kuliko Serikali? Kwanini hao Vijana wamsikilize Mange na si Viongozi wa Nchi. why?
Miaka 64 nchi ipo kundi la nchi masikini sana duniani. Siyo akili ya mtu ni Nchi.
Chama kilichoongoza miaka 64 ni CCM ikianza na TANU. Tatizo linakuwaje la mtu binafsi wakati Nchi ni masikini?

Tuna VX na maderaya ya Polisi mengi kuliko matrekta! gharama za Bunge ni kubwa kuliko Wizara ya Elimu.
Hatutaki kushindanisha mawazo kwa hofu ya kuambiwa ukweli.
Pesa zinapigwa watu wakiambiwa wakae kimya kwa Amani. Leo unalaumu victims

Umemsikia Judge J.S.Warioba? anasema Wananchi waambiwe watu wangapi walikufa. Mzee kasema waliokufa ni wengi kuliko waliokufa Vita ya Kagera! Usinijibu mimi mjibu mzee Warioba
 
Kuna masuala ya kiinteligensia hayawezi kuweka humu jukwaani, siri za kiusalama huwezi kuzianika humu kila mtu azifahamu hata hao hao maharamia wazifahamu.

Unaoitwa utekaji haufanywi kwa kila mtu, mbona mimi na wewe tupo huru tukiendelea kujadiliana humu?, utatekwa ukigundulika una matatizo kwa uwepo wa serikali.

Vyama vya upinzani vinafanya shughuli zao kama kawaida, zuio aliloliweka hayati JPM liliondolewa na Samia hao kina Lissu na Heche wakashindwa kuheshimu uhuru waliopewa wakaishia kutishia mamlaka kwamba watakanikunisha. Wakasahau kwamba JPM aliwanyima hata huo uhuru unaowanyima heshima mbele ya kiongozi mkuu wa nchi.

Lissu yupo ndani kwa sababu ya kauli zake za vitisho na dharau kwa mamlaka, haswa kwa Rais na mamlaka yake pale alipotishia kukinukisha, kapewa kesi ya uhaini hata ukimsikiliza hana utetezi wenye kuonyesha yupo ndani kwa kuonewa.

Ufujaji wa matumizi ya pesa za umma unakwenda pamoja na maendeleo ya huduma mbalimbali ambayo kwa sasa yapo wazi, hakuna mahali duniani wala serikali isiyopambana na rushwa. Viwango vya wizi hutofautiana lakini rushwa zipo kila nchi duniani.

Huwezi kusema chaguzi za kupanga wakati muda wote wanautumia kupinga kila kinachofanyika, wakaanza na no reform no election uchaguzi ukafanyika wakaanza na matamko ya kutoitambua serikali, yaani hawaitambui serikali wakati uchaguzi mkuu waliususia wao wenyewe!.

Mgogoro na taasisi za dini mara nyingi huwa ni kile tunachokiona kwa macho yetu lakini hizo taasisi zimejaa ufisadi na upigaji wa kila aina kwa miaka mingi. Wafanyabiashara wakubwa walikuwa nyuma ya upingaji wa kampuni ya DP World kuwekeza katika sekta ya bandari kwa sababu walishazoea kula kiulaini kila siku. Samia akawaambia tutakwenda kwa masharti yatakayowekwa na serikali na sio kuongozwa na ufisadi wa kificho unabarikiwa na TEC.

Father Kitima akiwawakilisha mafisadi tulionao katika kanisa katoliki aliupinga uwekezaji wa DP World kwa ubinafsi wake akaliingiza kanisa katika siasa za waraka wa kupinga hiyo biashara pale TPA kumbe alikuwa hajui mengi ya kitaalam kuhusiana na biashara ya DP World na serikali, kaja kuumbuka baada ya wawekezaji wengine kupewa nafasi ya kuwekeza kwenye bandari nyinginezo.

Kenya huwezi kuwaunganisha na hayo mengi yanayohusu siasa za ndani, lakini wamekuwa washindani wetu wanaodhamini ushenzi unaofanywa na Maria Sarungi pamoja na Mange. Tarehe 9 Desemba hatukuandamana lakini wanaharakati wakaandamana katika ubalozi wa Tanzania kule Kenya, kiliwawasha nini wao sisi kutoandamana?.

Kuondoa umaskini ni mchakato wa miaka na miaka, USA wana miaka 250 ya kuwa huru lakini ukienda nje ya white house kuna wananchi wanaolala nje kwenye nyumba za maboksi na plastiki, kule Hollywood California hali ni mbaya zaidi kwenye suala la walalao nje na watumiaji wa madawa ya kulevya.

Tangu JPM aingie ikulu nguvu kubwa inakwenda kutatua matatizo ya kiuchumi yanayoyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja, usitazame hizo VX tazama madaraja ya bei kubwa zaidi yanayojengwa na kumaliziwa kila mkoa.

Usikariri lawama za VX, tazama namna umeme ulivyosambazwa kila kona ya TZ ambao ni ghali kulinganisha na hizo VX.
 
Samia hajajificha kamuachia nafasi Mwigulu Nchemba apambane na wapigaji kwenye sekta mbalimbali.

Namuona mnyiramba akijipigia debe kimtindo, atakuwa anaiwazia nafasi ya urais mwaka 2030.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…