Bwana Steve , hakuna ligi ! tunajadili unayoleta. Kuzungumzia jambo bila ushahidi ni kutowatendea haki Wasomaji, ni propaganda. Tumepata tatizo linalohitaji suluhu tuwe pamoja. Suluhu haipatikani kwa kukwepa sababu halisi na kudhani propaganda zinafanya kazi. Propaganda zimeshindwa tukawa na MO29.
Huo ugumu wa maisha kwa nchi hii haujaanza jana wala juzi umekuwepo kila awamu ya kila rais.
Hakuna mahali katika bandiko tumeeleza ugumu wa maisha. Tualichosema ambacho Wananchi wanawaambia viongozi na ambacho kipo midomoni mwa jamii ni haya;
Utekaji na kupotea watu. Mikataba ya rasilimali i. Matumizi na ufujaji. Kuminya demokrasia kwa chaguzi. Kufungia vyama vya siasa kutofanya siasa. Kufunga viongozi wa upinzani. Migogoro na taasisi za dini n.k. swali kwako, haya yamesababishwaje na Wakenya?
Vijana wanajazwa sana habari hasi zenye harufu ya uchochezi matokeo yake hawawezi kuona mengi mazuri ambayo ni fursa kwa maisha yao.
Uelewe vijana wa leo si wa 80,70 au 60. Dunia imebadilika, wanaona na wanajua.
Kufungia au kudhibiti vyombo vya habari nchini huenda ikawa ni sababu pia kama uchochezi upo.
Watu wanatafuta habari wanakojua lakini pia hayo mazuri unayosema yamefanyika hayawafikii kwasababu vhawana habari na vyombo vinavyodhibitiwa na serikali.
Mfano, serikali kufungia JF kumesaidia vipi?
Media zinafanya kazi in two way traffic, zinachukua habari kutoka kwa jamii kwenda kwa viongozi and vice versa.Kudhibiti media ni kufanya one way traffic. Wananchi wanatafuta habari wanakojua.
Wasingeuliwa watu huko mtaani, wale wapuuzi wangepindua nchi, yale mauaji ingawa ni haramu lakini yalisaidia kurudisha heshima kati ya wananchi wa kawaida na mamlaka ya kiserikali.
Yalirudisha heshima? Hivi unaifahamu chuki iliyopo mitaani?
Akili zile zile za kizungu, kwamba anayechoma moto treni ya mwendokasi ana haki ya kuendelea kufanya hivyo lakini anapopigwa risasi na kufa basi serikali inaingia lawamani kwa vifo vya raia, vipi kuhusu ubaya wa malengo ya hao raia kwa mustakabali mzima wa uwepo wa Dola?.
Tunasheria za uhalifu hakuna inayosema Watu wauawe wakifanya uhalifu. Sheria zetu zinaruhusu watu kunyongwa si kwa hiari ya Askari bali idhini ya mamlaka ya Mahakama. Kazi za Polisi ni kuwaweka wahalfu chini ya ulinzi na kuwafikisha mbele ya sheria. Hawaruhusiwi hata kupiga kwa
Swali langu kwa Bwana Ntamusana,
Ni mabeberu wa Ulaya au Wakenya au Waliokosa Uzalendo au Vibaka au Wanaharakati?
Hakuna anayejua kila mmoja na ramli yake!