PostGE2025 ‘Ulipata’ kura zaidi ya milioni 31 lakini leo umejificha

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ni sawa lakini approach ya NRNE haikua sahihi na kadiri muda unavyokwenda unatuambia!!

Japo Samia hayuko sahihi na bado anaishi kwenye mfumo Magufuli (huu itachukua muda sana CCM kuondokana nao)

Nitaendelea kusema Lissu na ile sura ya harakati aloingia nayo CDM was not an option!!

..nrne ingeweza kuzimwa kwa kufanya mabadiliko ya kweli katika Tume.

..kwa mfano, haikuwa sahihi kupitisha sheria ya tume huru halafu mwenyekiti na wakurugenzi wanabaki walewale.

..chadema ambao mnawalaumu waliomba mpaka uchaguzi uahirishwe, lakini Mama akawapuuza na kuchagua ubabe.
 
CHADEMA walionyesha ubishi tangu mwanzo kabisa. Baadae Lissu akaja na kauli ya 'kukinukisha' na tukashuhudia namna kilivyonuka October 29.

Pia CDM wanadhani wao ndio chama pekee cha upinzani wanasahau kuwa vipo vyama vingine 16, vipi kila chama kingekuja na matakwa yake na kikataka yatekelezwe kwa asilimia 100?.

Lissu na Heche hawazijui siasa za kujishusha kwa faida ya wote.

..Chadema waliomba uchaguzi uahirishwe ili mabadiliko yafanyike.

..kama Chadema wangesikilizwa haya mabalaa yasingetufika.

..hata TLS walishauri hatua za kuchukua kabla ya uchaguzi lakini na wao walipuuzwa.

..hapa Mama asitafute mchawi nje ya timu inayomzunguka na kumshauri.
 
Ukweli ni kwamba wasaliti wa nchi walianza kujenga tabia ya kishetani ya kutaka kufaidika na taharuki ya kwenye mitandaoni.

Hawajali kuwa uchumi mkuu wa TZ unaporoka ilimradi wa kwao binafsi unakwenda juu, watanzania wamewashtukia washenzi hao wanaoishi Ulaya na USA wameamua kutokubaliana na hoja yao ya kusambaza chuki miongoni mwa mwetu.

Walikuja na mikwara ya maandamano yasiyo na mwisho leo watu wameamkia kazini kama kawaida, sasa hao wapuuzi wanaounga mkono wakitaka kuijua hasira ya watanzania wazalendo wajichanganye tu kuanzisha maandamano siku za kazi watajua kilichomtoa kanga manyoya.

Usidhani imewezekana kwa uwezo wa kibinadamu. Pale St Gasper Mbezi Beach tuliweka Novena ya siku tisa iliyomalizika tarehe 8, Mungu amejibu upendo wake. Hatuna utamaduni wa kuishi kwa hofu hao washenzi wanaoishi huko Marekani wameshindwa kutuambukiza roho za maasi zilizoitesa serikali ya Kenya.
Mkuu D9 vijana walitaka kufanya maandamano ya amani na ndio maana jeshi likaweza kuzuia na ni kitu ambacho kilikuwa wazi kabisa kisingewezekana. Kwahiyo kama mnafanya maombi basi zidisheni sana kwa sababu sasa hivi wanachoamua kufanya ni kama walivyofanya Mo29.
 
..Chadema waliomba uchaguzi uahirishwe ili mabadiliko yafanyike.

..kama Chadema wangesikilizwa haya mabalaa yasingetufika.

..hata TLS walishauri hatua za kuchukua kabla ya uchaguzi lakini na wao walipuuzwa.

..hapa Mama asitafute mchawi nje ya timu inayomzunguka na kumshauri.
Lissu alikomaa na no reform wakati huo vyama vyote vimeitwa na kiongozi wa tume ya uchaguzi.

Ubishi na ujuaji unaisumbua CDM hii ya Lissu na Heche.
 
Mkuu D9 vijana walitaka kufanya maandamano ya amani na ndio maana jeshi likaweza kuzuia na ni kitu ambacho kilikuwa wazi kabisa kisingewezekana. Kwahiyo kama mnafanya maombi basi zidisheni sana kwa sababu sasa hivi wanachoamua kufanya ni kama walivyofanya Mo29.
Mkuu wa Polisi mpaka tarehe 8 jioni hajapata barua ya maandamano, hafanyi kazi kwa kutegemea posts za instagram, ofisi yake haitakiwi kuchukuliwa poa tu.

Maandamano wayafanyie humu humu JF na instagram huko barabarani watatafuta kifo wakiwa vijana wadogo.

Hatutaki tena kuwaonea huruma akina mama wanaolia baada ya kutowaona watoto wao kwa siku kadhaa!.
 
Unategemea serikali itakubali kuruhusu maandamano? Kipindi cha Magufuli maandamano yalipigwa marufuku kabisa, na leo bado tunazungumzia suala hilo hilo la maandamano.

Kifupi tu mkuu wanachotaka kufanya vijana sasa hivi ni kurudia kuchoma vitu kama walivyofanya oct 29.
 
Lissu alikomaa na no reform wakati huo vyama vyote vimeitwa na kiongozi wa tume ya uchaguzi.

Ubishi na ujuaji unaisumbua CDM hii ya Lissu na Heche.

..vyama vilivyoshiriki vimejitokeza na kukiri kwamba Chadema walikuwa sahihi. Kwa msingi huo tukiendelea kumlaumu Lissu tutakuwa hatuitendei nchi yetu haki.

..Na kama unataka kulaumu watu kwa ubishi na ujuaji utaeleweka zaidi ukimlaumu Mama na Ccm maana matokeo ya ubishi wao dhidi ya mabadiliko yamesababisha umwagaji damu.
 
View attachment 3514408
View attachment 3514407
Judging those you don't know is a sign of low intelligence, kwa Samia na supporters wake at least tuna unshakable evidences.
Binadamu mwenye utu, anayejiheshimu na anayepigania haki hawezi kupost kitu kama hiki kwenye mitandao.
You are slowly become a real monster for the innocent blood spilled. You will not return to be a normal human being, and the Karma will hunt you and all of your generations.
 
..vyama vilivyoshiriki vimejitokeza na kukiri kwamba Chadema walikuwa sahihi. Kwa msingi huo tukiendelea kumlaumu Lissu tutakuwa hatuitendei
nchi yetu haki.

..Na kama unataka kulaumu watu kwa ubishi na ujuaji utaeleweka zaidi ukimlaumu Mama na Ccm maana matokeo ya ubishi wao dhidi ya mabadiliko yamesababisha umwagaji damu.
Umwagaji damu ulianza na kauli mbaya ya Lissu pale aliporekodiwa akisema mwaka huu watakinukisha vibaya sana, asingekuwa jela damu ambayo ingemwagika hiyo tarehe 29 October ingekuwa nyingi zaidi.

Heche nae akarudia kuongea kibabe kwamba uchaguzi hautafanyika mwaka huu, walijua namna zao chafu ambazo walizitumia kutaka kuvuruga uchaguzi mkuu.

Vyama vingine 16 vilivyoshiriki uchaguzi mkuu viongozi wao ni binadamu wenye sifa zile zile za kina Lissu na Heche, tatizo CHADEMA ina viongozi wanaodhani wanajua kila kitu kumbe akili za kawaida sana.
 
Maajabu ya Samia hayo!

Kwamba eti alipata kura zaidi ya milioni 31.

Ambazo eti ni 97.6% ya kura zilizopigwa.

Ila cha ajabu, akajiapisha uani na kuwanyima fursa hao wapiga kura wake milioni 31 kusherehekea huo ‘ushindi’ wake.

Leo ni maadhimisho ya 64 toka Tanganyika ipate uhuru.

Ni siku kubwa.

Lakini cha ajabu tena, yeye huyo Samia [sitomuita Rais kwa sababu hakuna aliyemchagua awe rais] leo yuko mafichoni.

Hajulikani alipo. Kajificha 😀.

Sikumbuki mara ya mwisho Rais wa Tanzania kujificha siku ya uhuru.

Ama kweli huyu Samia ni mtu tofauti sana.

Hata yale maonyesho ya wale makomandoo wake, wale ambao huwa wanaruka ruka na kuigiza kupigana huku wamejipaka masizi usoni na kubeba mabegi yao ya mgongoni, leo hakuna 😀.

GenZ wa Tanzania kiboko aisee.

Yaani they are basically calling the shots.

Hey Samuya, where are you? 😂
Who are you
 
Umwagaji damu ulianza na kauli mbaya ya Lissu pale aliporekodiwa akisema mwaka huu watakinukisha vibaya sana, asingekuwa jela damu ambayo ingemwagika hiyo tarehe 29 October ingekuwa nyingi zaidi.

Heche nae akarudia kuongea kibabe kwamba uchaguzi hautafanyika mwaka huu, walijua namna zao chafu ambazo walizitumia kutaka kuvuruga uchaguzi mkuu.

Vyama vingine 16 vilivyoshiriki uchaguzi mkuu viongozi wao ni binadamu wenye sifa zile zile za kina Lissu na Heche, tatizo CHADEMA ina viongozi wanaodhani wanajua kila kitu kumbe akili za kawaida sana.

..Najua Mama na dola wanatafuta mtu wa kumuangushia lawama.

..basi tumalize ubishi kwa kukubali kuwa Lissu ndiye aliyeteka, aliyepoteza, na hata kuuwa watu siku ya uchaguzi.

..tujiulize kama madai ya Chadema ni ya kweli, au si ya kweli.

..kama ni madai ya kweli basi yafanyiwe kazi, kwani hata Chadema wasipokuwepo kuna chama kingine kitaendeleza madai hayo.
 
Hizo social unrest zipo dunia nzima, hata USA na Ulaya kuna hizi kasheshe za maandamano, haizui ukweli kwamba yale yalikuwa mapinduzi bubu.
Kwanza, ''ukweli wa mapinduzi bubu'' unapatikana tukijua nani alikuwa kiongozi. Nimeuliza huna jibu
Ni wapi mapinduzi yalitokea kama mvua!

Pili, usiangalie hali yetu kwa ''image'' ya US na EU. Mbona hulinganishi vipato na hali za uchumi na nchi hizo!
Hoja ni kuangalia hali yetu kwa mfano wa Marais 5 waliopita. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na JPM
Kwanini leo! Kulikoni!

Tatu, social unrest is real. Inequalities na injustices ni sababu zilivyochagiza sababu zilizokuwepo.
Ni ''Provoking factor'' lakini tayari kulikuwa na grivances. Huu ni ukweli anayoujua kila mtu, kwanini tujidanganye!
Hakuna maandamano katika mazingira ya watu kuchoma moto kituo cha polisi.
Nimeuliza Polisi wangapi wamefariki, huna jibu. Raia wangapi wamefariki huna jibu. Kwanini vituo hivyo?
Sina idadi kamili ya polisi waliouwawa lakini wapo, usidhani wale jamaa wenye fulana nyeusi waliamua tu kupiga watu risasi bila ya sababu, walikuwa wanapambana na nguvu kubwa ya chini kwa chini.
Nani amekuwa arrested kwa kuwa na silaha?
Ule ulikuwa upepo mbaya uliokuta serikali imejikita kwenye uchaguzi ikiwa imepeleka rasilimali watu kubwa kwenye eneo moja wale wahuni wakautumia mwanya huo kufanya vurugu kubwa. Tarehe 9 Desemba hakufa hata mtu mmoja, serikali iliweza kujipanga vilivyo.
Tangu May 2025 watu walionya hapa JF kuna tatizo. Mzee Warioba, mmoja wa watu wenye heshima alionya kuna tatizo linakuja. Viongozi wa dini walionya. Kilichotokea ni mazoea, kwamba, hawa ni Watanzania tunawajua! yale ya JK ni upepo utapita.
Samia ukiwasikiliza wajuaji wa majiji makubwa huku Dar na mikoa michache hajafanya kitu, lakini ukisogea huko mikoani kwa ukaribu utaona mengi sana anayoyafanya.
Sijui kama umeelewa sababu za social unrest. Nimekueleza mara nyingi, chanzo ni inequalities and Injustices.
Watu wanaweza kuishi maisha mazuri na ya kifahari sana, lakini je hiyo ina address inequalities ikiwa kuna anayeishi kwa ufukara. Kwanini watu wanahoji 'wale wanaolipwa milioni 20''

Je, watu wanatendewa haki? hili ni ku address injustice. Kwa mfano, mapendekezo ya Tume ya Haki jinai ya Jaji Chande yametekelezwa? Na unadhani kwanini tume iliundwa.

Madaraja, majumba, magari , ndege n.k. haviwezi ku address inequalities and injustices vitu ambavyo ni precusor for socila unrest.
Hizi negative news zinatengenezwa na kina Maria Sarungi na Mange hawa watoto wa wakubwa hawajui chochote kuhusiana na masuala ya kiuchumi yanayoendelea kwa mapana yake Tanzania nzima, wanadaka umbea kisha wanaueneza kwa kuongezea habari hasi.
Hapa kuna tatizo! hivi kwanini wana ushawishi wa namna hiyo katika jamii? Je, viongozi wamejibu hoja zao? Na kwanini jamii iwaamini. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza si kwanini wapo.
Tafuta chanzo cha tatizo, siku hizi vijana wanasema mtafute aliyejamba siyo aliyetema mate
Tanzania itashinda licha ya uwepo wa mapambano mengi ya mitandaoni.
Tanzania haina tatizo, kuna tatizo la kutowasikiliza Watanzani! that's it.

JokaKuu
 
Kwanza, ''ukweli wa mapinduzi bubu'' unapatikana tukijua nani alikuwa kiongozi. Nimeuliza huna jibu
Ni wapi mapinduzi yalitokea kama mvua!

Pili, usiangalie hali yetu kwa ''image'' ya US na EU. Mbona hulinganishi vipato na hali za uchumi na nchi hizo!
Hoja ni kuangalia hali yetu kwa mfano wa Marais 5 waliopita. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na JPM
Kwanini leo! Kulikoni!

Tatu, social unrest is real. Inequalities na injustices ni sababu zilivyochagiza sababu zilizokuwepo.
Ni ''Provoking factor'' lakini tayari kulikuwa na grivances. Huu ni ukweli anayoujua kila mtu, kwanini tujidanganye!

Nimeuliza Polisi wangapi wamefariki, huna jibu. Raia wangapi wamefariki huna jibu. Kwanini vituo hivyo?

Nani amekuwa arrested kwa kuwa na silaha?

Tangu May 2025 watu walionya hapa JF kuna tatizo. Mzee Warioba, mmoja wa watu wenye heshima alionya kuna tatizo linakuja. Viongozi wa dini walionya. Kilichotokea ni mazoea, kwamba, hawa ni Watanzania tunawajua! yale ya JK ni upepo utapita.

Sijui kama umeelewa sababu za social unrest. Nimekueleza mara nyingi, chanzo ni inequalities and Injustices.
Watu wanaweza kuishi maisha mazuri na ya kifahari sana, lakini je hiyo ina address inequalities ikiwa kuna anayeishi kwa ufukara. Kwanini watu wanahoji 'wale wanaolipwa milioni 20''

Je, watu wanatendewa haki? hili ni ku address injustice. Kwa mfano, mapendekezo ya Tume ya Haki jinai ya Jaji Chande yametekelezwa? Na unadhani kwanini tume iliundwa.

Madaraja, majumba, magari , ndege n.k. haviwezi ku address inequalities and injustices vitu ambavyo ni precusor for socila unrest.

Hapa kuna tatizo! hivi kwanini wana ushawishi wa namna hiyo katika jamii? Je, viongozi wamejibu hoja zao? Na kwanini jamii iwaamini. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza si kwanini wapo.
Tafuta chanzo cha tatizo, siku hizi vijana wanasema mtafute aliyejamba siyo aliyetema mate

Tanzania haina tatizo, kuna tatizo la kutowasikiliza Watanzani! that's it.

JokaKuu
Kwanza, ''ukweli wa mapinduzi bubu'' unapatikana tukijua nani alikuwa kiongozi. Nimeuliza huna jibu
Ni wapi mapinduzi yalitokea kama mvua!

Pili, usiangalie hali yetu kwa ''image'' ya US na EU. Mbona hulinganishi vipato na hali za uchumi na nchi hizo!
Hoja ni kuangalia hali yetu kwa mfano wa Marais 5 waliopita. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na JPM
Kwanini leo! Kulikoni!

Tatu, social unrest is real. Inequalities na injustices ni sababu zilivyochagiza sababu zilizokuwepo.
Ni ''Provoking factor'' lakini tayari kulikuwa na grivances. Huu ni ukweli anayoujua kila mtu, kwanini tujidanganye!

Nimeuliza Polisi wangapi wamefariki, huna jibu. Raia wangapi wamefariki huna jibu. Kwanini vituo hivyo?

Nani amekuwa arrested kwa kuwa na silaha?

Tangu May 2025 watu walionya hapa JF kuna tatizo. Mzee Warioba, mmoja wa watu wenye heshima alionya kuna tatizo linakuja. Viongozi wa dini walionya. Kilichotokea ni mazoea, kwamba, hawa ni Watanzania tunawajua! yale ya JK ni upepo utapita.

Sijui kama umeelewa sababu za social unrest. Nimekueleza mara nyingi, chanzo ni inequalities and Injustices.
Watu wanaweza kuishi maisha mazuri na ya kifahari sana, lakini je hiyo ina address inequalities ikiwa kuna anayeishi kwa ufukara. Kwanini watu wanahoji 'wale wanaolipwa milioni 20''

Je, watu wanatendewa haki? hili ni ku address injustice. Kwa mfano, mapendekezo ya Tume ya Haki jinai ya Jaji Chande yametekelezwa? Na unadhani kwanini tume iliundwa.

Madaraja, majumba, magari , ndege n.k. haviwezi ku address inequalities and injustices vitu ambavyo ni precusor for socila unrest.

Hapa kuna tatizo! hivi kwanini wana ushawishi wa namna hiyo katika jamii? Je, viongozi wamejibu hoja zao? Na kwanini jamii iwaamini. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza si kwanini wapo.
Tafuta chanzo cha tatizo, siku hizi vijana wanasema mtafute aliyejamba siyo aliyetema mate

Tanzania haina tatizo, kuna tatizo la kutowasikiliza Watanzani! that's it.

JokaKuu
Nadhani uliziona zile video za Pole Pole mwezi mzima kuelekea uchaguzi mkuu, nadhani unafahamu kwamba Waziri wa muhula wa kwanza wa awamu ya sita Mheshimiwa Mwambe yupo ndani muda huu. Wengine ni vigumu kuwaweka wazi hapa kwenye jukwaa.

Pole Pole aliitumia hii social Unrest katika kujenga chuki dhidi ya serikali ya Samia akisema kikatiba haruhusiwi kugombea tena, ufafanuzi ukatolewa na mwanasheria mkuu lakini alichokifanya balozi huyo wa zamani wa Cuba ikawa ni kuendelea kutengeneza chuki dhidi ya SSH.

Hakuna kipindi tangu awamu ya kwanza mtanzania wa kawaida aliwahi kuridhishwa na hali ya uchumi, hata yale mapinduzi ya 1964 yaliyoanzia jeshini sababu isiyotajwa ni hiyo hiyo ya kijamii. Wanaoandaa mapinduzi huitumia hali ya wananchi kwa wakati fulani kuja na sababu ya kwanini wanaamini Rais aliyepo hafai, hivyo October 29 tuliangukia kwenye dhana hizo hizo za wanaofanya mapinduzi barani Afrika.

Polisi waliuawa, sio rahisi kuweka hapa data lakini vituo kadhaa vilichomwa moto na video zipo mitandaoni.

Dunia haijawahi kuwa uwanja sahihi wa utoaji wa haki, hizo social unrest zinatokea mpaka huko USA ambapo panajulikana kuwa ni dunia ya kwanza kimaisha, kila siku ICE wananyanyasa raia wa kigeni, kila siku mabomu yanapigwa mitaani katika baadhi ya majiji, sisi sio wa kipekee sana kiasi cha kukosa kuwa na matatizo ya aina hiyo.

Uzuri wetu tupo vizuri katika suala la inteligensia, na JWTZ limeonyesha uimara kwenye ulinzi. Samia wanamtengenezea chuki kuanzia kwa baadhi ya maaskofu wa kanisa katoliki mpaka kwenye baraza la mawaziri kwa kigezo cha udini na ile dhana kwamba mjomba wake ni raia wa Oman.

Kutendewa au kutotendewa haki hilo ni tatizo la kidunia ndio maana zipo mahakama kuanzia za mwanzo mpaka ile ya rufaa. Ni mchakato wa mapambano uliopo maishani kwa ujumla.

Kwa hiyo zisinunuliwe ndege, usitengenezwe usafiri wa mwendo kasi kisa kuna mtu fulani hapati haki yake?.

Huyo Warioba aliyeonya juu ya machafuko sisi tulikuwa wadogo wakati akiwa AG miaka ile ya 80 mwanzoni, nchi ilikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi kibaya zaidi hapakuwa na uhuru wa habari hivyo waliodai haki wakati ule waliteseka kimya kimya tofauti na hawa wanaoweka kila hatua za mapambano yao kwenye instagram na tiktok
 
Pole Pole aliitumia hii social Unrest katika kujenga chuki dhidi ya serikali ya Samia akisema kikatiba haruhusiwi kugombea tena, ufafanuzi ukatolewa na mwanasheria mkuu lakini alichokifanya balozi huyo wa zamani wa Cuba ikawa ni kuendelea kutengeneza chuki dhidi ya SSH.
Hapana! usifanye spinning. Polepole alizungumzia utamaduni wa CCM kwamba Makamu na PM hawajawahi kugombea. Tena alisema ni utamaduni usioandikwa popote lakini unakubalika ndani ya Chama. Kumbuka alikuwa mwenezi wa CCM. Hakuna mahali aliposema hairuhusiwi kugombea Urais! tofautisha hayo mawili

Pili, kwanini kutoa maoni iwe kujenga chuki? Kama mwanasheria mkuu alimjibu ,je hiyo si ndio njia sahihi ya kujadiliana! Unachotaka kutueleza hapa ni kwamba ukitofautiana kimawazo ni kujenga chuki! real?
Wanaoandaa mapinduzi huitumia hali ya wananchi kwa wakati fulani kuja na sababu ya kwanini wanaamini Rais aliyepo hafai, hivyo October 29 tuliangukia kwenye dhana hizo hizo za wanaofanya mapinduzi barani Afrika.
Ni akina nani wanaoandaa mapinduzi? Pili, hivi hujawahi kusikia maoni ya Wananchi wa kawaida!
Sikumbuki kusikia Mwananchi akihojiwa au kusema anakwazwa na hali ya uchumi. Mengine wanayataja
Polisi waliuawa, sio rahisi kuweka hapa data lakini vituo kadhaa vilichomwa moto na video zipo mitandaoni.
Kwanini kuna data za vituo vya mafuta, magari, Bajaji na Bodaboda lakini hakuna data za vituo vya Polisi au kupigia kura au Wananchi waliofariki. Kwanini takwimu zinachagua kipi kipatikane na kipi la!
Dunia haijawahi kuwa uwanja sahihi wa utoaji wa haki, hizo social unrest zinatokea mpaka huko USA
Kwanini hujishughulishi kuzungumzia hali yetu kwa jicho la awamu 5 zilizotangulia. Nani kasema USA ni 'world standard''.
Uzuri wetu tupo vizuri katika suala la inteligensia, na JWTZ limeonyesha uimara kwenye ulinzi.
Intelligence inafanya kazi kwa njia zote, ikisoma yaliyopita (retrospective) na kuona yajao (prospective)
Kazi ya intellegence ni kuzuia tatizo kabla halijatokea.

Kwa walioishi nyakati hizo, Nyerere alikuwa na intelligence kali sana ''local and international'' . Intelligence ya Nyerere ilimweleza tatizo ndani ya jamii ndio maana aliwahi kuzungumzia uhaba wa sukari na kuzungumzia tatizo la unga. Mwalimu aliweza kusoma jamii ndio maana aliweza ku connect na jamii na kuzuia matatizo mengi.
Samia wanamtengenezea chuki kuanzia kwa baadhi ya maaskofu wa kanisa katoliki mpaka kwenye baraza la mawaziri kwa kigezo cha udini na ile dhana kwamba mjomba wake ni raia wa Oman.
No no no! na nadhani ni karata ya hatari sana ! Nyerere alipingwa kwa hayo usemayo? Mkapa je! Mwinyi je, JPM mpaka leo anapingwa akiwa kaburini. Please karata inayochezwa ni ya hatari sana
Kutendewa au kutotendewa haki hilo ni tatizo la kidunia ndio maana zipo mahakama kuanzia za mwanzo mpaka ile ya rufaa. Ni mchakato wa mapambano uliopo maishani kwa ujumla.
Excellent! kwanini Wananchi wamepoteza imani na Mahakama?
Kwa hiyo zisinunuliwe ndege, usitengenezwe usafiri wa mwendo kasi kisa kuna mtu fulani hapati haki yake?.
Hapa ndipo Nyerere anawashinda viongozi wengi, alizungumza na Mwananchi na kujua tatizo lake

Mwananchi aliyedhulumiwa shamba lake la eka 2 anaumizwa sana na dhuluma kuliko kufikiri tiketi ya ATC

Nyerere ali connect na majority si minority ya wapanda ndege.
Ukienda kijijini ukaongelea bei ya tiketi ya ndege utaonekana mpumbavu tu, ongelea shida zao ikiwemo haki
Huyo Warioba aliyeonya juu ya machafuko sisi tulikuwa wadogo wakati akiwa AG miaka ile ya 80 mwanzoni, nchi ilikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi kibaya zaidi hapakuwa na uhuru wa habari hivyo waliodai haki wakati ule waliteseka kimya kimya tofauti na hawa wanaoweka kila hatua za mapambano yao kwenye instagram na tiktok
Well, je alichosema si kweli? Je hakikutokea! Kama ana madhambi ya huko nyuma, hiyo haimuondolei haki ya kutumia uzoefu wake kuonya! alionya na imetokea na anabaki kuwa Mzee mwenye hekima
 
Back
Top Bottom