The best_of _me
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 560
- 979
Umesahau kwamba yeye alikuwa mgombea, Je, una uhakika gani kwamba yeye ndo alitoa order kuhusu kilichotokea? Na kwa wale waliohamasisha watu kufanya fujo wao wako salama?Kwa Marais wa nchi maskini ikiwemo Tz ni easy sana kujikuta hatma yako iko mikononi mwa ICC na wakubwa wengine wa dunia hii kutokana na yaliyotokea Oct 29. Rejea kisa cha yule wa Ufilipino na wa Bangladeshi. Ngumu kwa nchi strong militarily ikiwemo China na Urus. ICC kuna uwezekano mkubwa watamwita. Ushahidi wa awali dhidi yake ni mwingi. Anachoweza fanya maza labda tu ni kukataa wito wa mahakama ya ICC na kuanza kuishi kama digidigi. Angekua na power aliyonayo Putin asingekua na hofu. Ila kibongo bongo ataishi maisha very stressful. Pia ataishi na hofu na hatari ya kuuzwa na weusi wenzie wasio na maslahi naye. Binafsi hata wasaidizi wake (makamu, waziri mkuu) siamini wapo upande wake fully. Kwa kifupi hali ni mbaya.
Ndo maana nasema hili suala halihitaji mihemko ya kisiasa na ICC hawafanyi kazi kwa mihemko.