Kwanza niliipata huko nyuma sana kwenye dili za kuuza shaba ,nikiwa mdogo sana ...kuna sehemu nyumba ziliungua ,tukaenda kuokota shaba na vyuma tukauza .
Chuo mwaka wa kwanza nilipata pesa ya kujikimu ile batch ya kwanza mara mbili 😅, halafu nikiwa mwaka wa pli nilipiga mil 8 kwa online pyramid scheme ila nishatemana nazo...Pesa kama zote niliweka home kwenye ukarabati wa nyumba fresh ila sio mwekezaji mzuri.
Nilitumia pesa sana ,nilitumia bila ya kuzalisha kwa mwaka 1.5 ikabaki mil 1 ,ghafla napata ajira naanza na take home ya 2.4 acha tu basi ,nili'hang sana watu wanajua mimi tajiri mpaka leo .
Niliishi juu juu ila sikuwahi kubaki mikono mitupu tangu nishike pesa mara ya kwanza.