Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
Wape pole na wengine waliopata maumivu hapa Duniani kwa matendo yake wakati wa uhai wake. Usiwasahau na wao pia ni binadamu.
 
Daah kabla ya Tarehe 17 tarehe 9 majaliwa anaenda njombe tarehe 12samia ana ziara Tanga siku tatu kabla ya hizo tarehe malaika alikua akizungumza na mimi katika roho...
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiki kiswahili cha wapi
 
Alifariki Baba, alifariki Mama nilihuzunika sana tu bila kutoa chozi.
Ila kwa JPM chozi lilinitoka kwa huzuni kubwa huku mapigo ya moyo yakiwa juu sana.
Hadi leo bado ninahuzuni.
Wewe ni katili
 
Nilikua nimelala,nikaamshwa na simu za wadau!
Binafsi kama kura na hata kampeni nilimpigia sana jiwe awamu ya kwanza mpaka nikakosana na watu wangu wa karibu ambao walikua chadema,lakini baadae nikaanza kumuona jiwe simwelewi yani hasomeki nikajuuuta adi kumpigia kampeni nikajisemea kweli ccm ni ileile!
Nikaamua kuishi huku simkubali,unatamani kitu kitokee atoweke ila ukweli ile siku napata taarifa rasmi kuwa jiwe kafa huzuni ilinijia mana mwisho wa siku nae ni binadamu tu na kifo tumeumbiwa wote!
Aendelee kupumzika mwamba,sasa tuko na mama na kazi inaendelea!
Mama oyeeeee!
 
Binafsi sikushtuka. Nilikuwa nimelala zangu nimefungulia clouds niko zangu twitter naperuzi. Nikaanza kuskia clouds wamechange motion wakaweka nyimbo flani hivi ambavyo sio kawaida yao, nako sikustuka, ghafla mida hiyo ya saa 5 mwanangu mmoja hivi kaniendea hewani, kabla sijapokea nikagundua kuna kitu. Kupokea tu kanipa taarifa huku akiwa na vibe la kutosha. Basi siku hiyo nililala mtandaoni kusoma maoni ya watu. Nilichogundua ni kuwa mwamba alikuwa hapendwi hata kidogo
 
Mpaka umri wa kuoa hujawahi kufiwa hata na ndugu ukaonja machungu ya msiba. Kwa nara ya kwanza ukayaonja kwenye kifo cha JPM jokate mwenyewe alikuwa anasmile tu
 
Aseee[emoji848][emoji848]
 
Mkuu si u download twitter? Kule raia wako fasta
 
Khaaaaaa[emoji134]
 
[emoji16][emoji16][emoji16] ukajua wanakulilia wewe[emoji1787]
 
Honestly nilifurahi.

Kama hukuumizwa na utawala wake hutoelewa.
 
Mimi nilikunywa Whisky mapema nikalala.

Sa saba nasikia sauti dirishani kwangu, mshana, mshana amka tukanywe bia jamaa katili kafariki.
Dah..........
[emoji23][emoji23]
 
Nilikuwa naandaa document flani ya jamaa, akanipigia simu, nikajua anataka nimtumie, ndiposa ananipa ripoti, kama binadamu nilistuka kwa furaha.
Kama binadamu ulishtuka kwa furaha?[emoji16][emoji1787]....nyinyi watu hamko serious
 
Sishangai kuwepo na binadamu wa aina yako wanaomini matusi ndio last option ya kutetea wanachokiamini dunia isingekua na watu kama nyinyi wenye hekima na busara wangeishi ulimwengu upi? Elimika sikufundishi
Busara yako ndio hiyo ya kumlilia Shetani Magufuli. Poor you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…