Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Nilitamani kuwa Afisa mtendaji wa kijiji,kipindi hicho wanaitwa makatibu wa vijiji.

Kilichofanya nimpende ni kwamba yeye ndiye aliyekuwa na baiskeli kijiji kizima inayoitwa Hamilton.

Huku akimiliki redio ya Santuri akiwa ndiye mwenye maisha mazuri kijiji kizima.

Hakika alikiwa Role model wangu eti😂😂
Dah engineer kwasasa hao watendaji ukiwaona huku vijijini huwezi kutamani Tena .
Wamejichokea Sana ,nahisi wale Kama hawalipwi laki moja Basi elfu hamsini maana hata kulipa pango ni kwa mbinde .

Alafu kwanini wengi wanakuwa ni wazee ? Kibaya ni kuwa Wana maisha magumu ila wanapewa majukumu makubwa na mamlaka makubwa imagine mtendaji ndiye mwakilishi wa mkurugenzi kwenye kata au Kijiji na ndiye yeye mwenye uwezo wa kusema polisi waje kukubeba au akulinde alafu mfukoni Yuko apeche alolo .
 
Mkuu,maisha ni magumu Sana kwa watendaji wa vijiji ,japo baadhi ya maeneo natembea nakutana na watendaji vijana ila asilimia nyingi ni wazee ,pia wakiwa na maisha yasiyoridhisha.
Tuombeane .
 
Mkuu,maisha ni magumu Sana kwa watendaji wa vijiji ,japo baadhi ya maeneo natembea nakutana na watendaji vijana ila asilimia nyingi ni wazee ,pia wakiwa na maisha yasiyoridhisha.
Tuombeane .
Yupo mmoja akiwa mtendaji huu mwaka wa ishirini ,ni mzee aliyetokea kuwa rafiki yangu na Mimi ndiye mshauri wake mkuu masuala ya kata nzima .

Ila maisha anayopitia inafika mahali naumia ila Sasa hata nikisema nimshauri kuhusu maisha binafsi atasema nishalewa ulanzi maana tunakunywa naye Sana ulanzi kila muda kila saa ,huku tunawaza maendeleo ya kata yetu pendwa
 
Mi sijui nilikuwa nataka kuwa nani ila nilkuwa napenda kutengeneza/ kusimulia stori iwe kwa kuandika kwenye daftari au kutumia zile Action figure ambazo ulikuwa ukinunua halafu unaanza kuzi attach mwenyewe kwa kutumia instruction walizokupa kisha nawakusanya ndugu zangu halafu naanza kutengeneza ka movie
 
Astronaut..Mtaalamu wa mambo ya anga huko juu..Nakumbuka hadi baba nlikuwa namuuliza maswali mengi sana kuhusu nyota na anga kwa ujumla.
Nikaingia shule mahesabu yakawa mengi sana.
Kiko wapi sasa 🤣🤣🤣.
Lakini nilipo sio pabaya nashukuru Mungu kuna vitu vinatokea sio kwa bahati mbaya unaona kabisa ni mpango wa Mungu.
 
Back
Top Bottom