Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Wakuu,

Leo ni Siku ya Watoto Duniani! Ulipokuwa mtoto, ulitamani kuwa nani?

Je, umefikia ndoto zako, au bado unazifanyia kazi?

Kumbuka, ndoto za watoto ni halali na zinaweza kutimia! Tuendelee kujenga mazingira yanayowawezesha watoto wetu kufanikisha ndoto zao
Sikuwahi kuhisi kubadilika pale ntakapokua mkubwa, nliamin hata ukubwani ntabaki kua mimi
 
Mimi nilikua natamani nije kuwa mwalimu, ili nichape sana watoto, hii ilikuja baada ya kuona walimu wanafaidi kutupiga 😀.

Baadaye nikaswitch nikatamani niwe muuza duka yaani ile exchange ya unampa mtu bidhaa anakupa hela nilikua naipenda sana😀
yaani ile exchange ya unampa mtu bidhaa anakupa hela nilikua naipenda sana😀.. 🙄🙄🙄
 
Ndoto za watoto wengi huzimwa na wazazi, ama umasikini au uzembe na kutokuwapa ushirikiano watoto wao
Mtoto unamuona tangu mdogo anapiga mpira vizuri ila wewe unampiga na kumwambia anajichafua
Wenzetu wengi wa watoto wanafanikiwa kufanya walichokuwa wanapenda kuwa tangu utotoni
Jana nimemuona mdada mmoja tangu alipokuwa ana miaka 12 alikuwa anapenda kuwahudumia watoto na leo anafanya kazi ya ndoto yake

Mimi nilipenda sana kuwa mjeda
 
Back
Top Bottom