Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

Ulipokuwa mtoto ulitamani ukiwa Mkubwa uwe nani?

... huyo bibi, enzi zile, alikuwa tishio mtaani kwetu! .... kiasi 'fantasies' zangu zote zilikuwa ni mapenzi mazito baina yetu!

Mbaya zaidi na yeye akajua, kiasi kila tukikutana naye hadi leo huwa anacheka sana!

UKWELI NI KUWA MZURI NI MZURI TU!

YAANI MPAKA SASA BADO NAHISI BIBI YULE ANA KITU NINAKIMISS!
😅

ACHA MAPENZI YAITWE MAPENZI!
Fanya uwe kama Macron.
 
seremala/sonara
mikono yangu ina ustadi sana,

mpira, mbio na ulengaji wa shabaa nilikua namarafiki zangu wana hivo vipaji, hadi nikawa nawaonea wivu muda huo mm sijui kipaji changu
Ila now si upo sehemu alhamdullilaah
Maana kila kitu kinatokea kwa sababu..

Kuna uzi mmoja sikumbuki ni upi ila niliona una shusha sana nondo nikawa nasema jamaa upo smart sana kichwani aiseee
 
Mimi nilitamani sana kuwa dereva. Enzi hizo magari yalikuwa machache sana kiasi kwamba unaweza kutambua gari la nani linapita kwa kusikia mlio tu na ubadilishaji wa gia. Nashukuru Mungu nilianza kujifunza udereva nikiwa darasa la sita tu. Sikuwahi kuwa proffesional driver lakini hadi sasa kila nikiendesha gari nakuwa nimetimiza ndoto yangu. 😂
 
Nilitamani kuwa Afisa mtendaji wa kijiji,kipindi hicho wanaitwa makatibu wa vijiji.

Kilichofanya nimpende ni kwamba yeye ndiye aliyekuwa na baiskeli kijiji kizima inayoitwa Hamilton.

Huku akimiliki redio ya Santuri akiwa ndiye mwenye maisha mazuri kijiji kizima.

Hakika alikiwa Role model wangu eti😂😂
Kipindi hcho baiskeli zinalipiwa insurance
 
Back
Top Bottom