Ulirudisha au kurudishiwa vitu mlipoachana?

Ulirudisha au kurudishiwa vitu mlipoachana?

Akiniambia Tu tuachane namhonga zaidi na kumwambia Kwa heri na vyote nilivyompa namwachia
 
Hivi mpaka mtu unafikia kumnunulia mwanamke gari, nyumba nk anakua amekupa nini hasa chenye thamani kiasi hicho? Aisee mimi bado sijakutana na mwanamke wa kumhonga hata simu tu..[emoji23][emoji23]
Hata Mimi wakati niko choka mbaya nilikuwa nashangaa na kuwaza Kama wewe,lkn Sasa kuhonga naona kawaida tu
 
Kuna pullover aliacha geto, na yeye alichukua tshirt yangu, kuna siku navaaga lle pullover yake alafu napita kwao akiniona ananuna sana,mara ingine anakimbilia ndani mwao , hata yeye nakutaga kavaa tshirt yangu ila sichukii ...[emoji28][emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima achukie yaani t-shirt ya buku tatu Harafu pullover ya buku 12.
Inauma sana
 
Akiniambia Tu tuachane namhonga zaidi na kumwambia Kwa heri na vyote nilivyompa namwachia
Haaa ili baadaye kiwe kigezo cha kuwasiliana naye ukianza kumdai
 
Hakuna kitu kinaumiza kama mkiachana harafu mwenzio alete madoido.
Je, wewe ilikuwaje mlivyo achana.
Rejea STAN BAKORA alicho sema yeye.

Nilimrudishia mpenzi wangu kado alionipa na kanda ya video ya nyimbo ya rose muhando
 
Sichukui hata kukumbushia siwezi tukiachana basi nilivokupa ni vyako ulivonipa kama utavihitaji nitakupa pia, Kuna mama moja nilikuwa nayo rufiji huko ikwiriri nilikuwa nalipa kodi mimi na vitu vya ndani nilikuwa nanunua mimi baadhi ndo vilikuwa vya kwake, tukaja zinguana baada ya kukuta ana msela mwingine anaempa utelezi tukaachana na nilikwenda tu kuchukua koti langu nilioning"iniza kwenye msumari basi na kodi ilikuwa inaisha nikamuachia na pesa ya miezi mitatu mbele ili asitetereke....
 
Back
Top Bottom