Ulishawahi jiuliza ni kwanini wakristo waliokoka wengi wana hali ngumu za kiuchumi japokua biblia imewahidi baraka nyingi sana

Kwasababu hela yote anampelekea sadaka mchungaji
 
Wewe ni mungu? Mbona unamsemea kua kapanga hivi na vile, wewe ulikuwepo alipokua anampa baraka ya mshahara mdogo na mtu akaukataa.

Tatizo lenu vijana mkishapata tukazi basi mnaona wengine ni wazembe.
 
Huchoki tu? Huna hoja nyingine tofauti na hiyo? Tangu umeanza kuandika hayo ya kumkataa Mungu umefaidika na nini?
Mimi sijaanzisha hii hoja. Nimeijibu tu. Suala la kuchoka halipo. Kwa sababu hata situmii energy kubwa, na flow tu. Labda wewe ndiye nikushangae, kwa nini unategemea nichoke kirahisi hivyo?

Pia, si lazima kusoma ninachoandika. Unaweza kuniweka kwenye ignore list usione ninachoandika.

Jibu hoja zangu. Kuniuliza "Huchoki tu" ni aina moja ya kusema hupendi hoja zangu, huwezi kuzijibu, na unataka kuninyamazisha kwa nguvu.

Tangu nimeanza kuandika haya ya kumkataa Mungu nimefaidika kuelimisha watu wengi zaidi kwamba hizi habari za kuwepo Mungu ni za uongo tu.

Zamani nilikuwa kama peke yangu naandika hivi, nilionekana mtu wa ajabu sana.

Siku hizi watu wengi wamekuja kueleea, na wengine walioeleea lakini walikuwa kimya, wamepata nguvu ya kusema wanavyofikiri, suala hiki limeonekana si la ajabu sana.

Wengine wamekuja kunishukuru kwa kuwafungua macho.

Mpaka wengine wanaoshikikia imani zao za Mungu wanasema wazi kwamba, wanashikilia imani hizo kwa utamaduni tu, lakini, kimantiki, wanaona mantiki katika hoja zangu.

Hapa JF tuna kaulimbiu kwamba tunathubutu kuongea mambo kwa uwazi.

Natekeleza kaulimbiu hiyo.

Na wewe huwezi kuninyamazisha kwa viswali vyako passive aggressive vya "huchoki tu".

Jibu hoja, ama sivyo, kaa kimya.
 
wanawachangia wachungaji wao wajenge majumba ya kifahari na magari alafu wao wanaambiwa watasaidiwa na MUNGU
Mchungaji anakula madhabahuni sio kosa ndo ujira wao
Sisi sawa na wafanyakazi wengi wanataabika huku mabosi zao wakitembelea magari ya million 500
 
We jamaa ni muongo kwamba zaman ulikua peke yako
Kwa hiyo we ndo wakwanza kumpinga Mungu swali je umepewa tuzo hizi cheap popularity hazitakusaidia kitu

Nikusaidie waafrika wengi walikua hawaamini huyu Mungu wa wakristo na waislamu sasa unavyosema wewe ni kwanza huu ni uongo mtakatifu
 
Uzi huu hauzungumzii kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu

Mnaumia nini kwani watu wakiwa bize na Mungu?
Unaongelea Wakristo, walokole. Tayari ushazungumzia kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu.

Kwa sababu Wakristo na walokoke wanaamini kuwepo kwa Mungu.

Ukiondoa uwepo wa Mungu katika imani yako, hakuna Ukristo wala Ulokole katika hiyo imani.
 
Naongelea katika muktadha wa JF. Tena nineweka neno kama.

Jua kusoma kwa ufahamu.

Hujathibitisha Mungu yupo bado.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kitu kidogo tu namkabidhi BWANA sasa hapa duniani bila changamoto hakuna Maendeleo wala Ubunifu.
 
Walokole , watu walio okolewa na dhambi, japo wote wanaendelea kutenda dhambi Kwa kujificha.

Japo mungu Hana mpango wa kusaidia watu masikini, mpaka pale Muda utakapo fika(haijulikani ni Muda Gani)
Ya kwamba unatakiwa ujitafute wewe mwenyewe kwanza mpaka ujipate.

Hakuna kukata tamaa ni kukomaa Tu,japo life ni gumu, coz resources ni chache watu wengi in tz.

NB: Dini, mungu ni vitu vilitungwa Kwa ajili ya Ku control watu masikini, wataishi kwenye nyumba za Dhahabu, mabikira 72, Mito ya pombe,

Hii πŸ‘† yote kuwapumbaza kuwa kuna Maisha mazuri baada ya kufa,
 
Wewe mtu unashinda kansani kila siku hufanyi kazi unategemea hela unazioataje, huko kansani basi kusiwe na sadaka ila sadaka kama zote hela unapataje utajiri.
 
Wewe mtu unashinda kansani kila siku hufanyi kazi unategemea hela unazioataje, huko kansani basi kusiwe na sadaka ila sadaka kama zote hela unapataje utajiri.
Kuna ambao kanisani ndo ofisini kwao mbona unakariri maisha
Mfano Makinisani kuna wahasibu wameajiriwa, kanisa ni taasisi usione ni mahali pa kupotezea mda watu wanaingiza siku
 
Si lazima kama huna nia ya kutenganisha ukweli na uongo.

Ukiwa na nia ya kutenganisha ukweli na uongo, uthibitisho ni lazima.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo kama hayupo.

Na wewe huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
Sawa ni uongo na Mungu hayupo umeshafurahi
 
Rejea Katiba kiranga
 
Kuna watu ni wabahili sana ila wana-hali ngumu sana za uchumi
Hao bado ni maskini huwezi kuwaita ni bahili kwa sababu hata wanachokipata wao wenyewe hakiwatoshi so hao wanabaki kuwa maskini.

Ninavyojua mimi bahili ni yule baada ya kufanya yote ya msingi (ya lazima) kinachobaki anakitunza hata itokee nini hakitoi,mtu mwenye uwezo wa kula vizuri kwa uhakika,watoto kwenda shule na kulala pazuri huwezi kumsema ana hali mbaya kiuchumi hao unaowajua wewe hawajafikia sifa za kuitwa wabahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…