Ulishawahi jiuliza ni kwanini wakristo waliokoka wengi wana hali ngumu za kiuchumi japokua biblia imewahidi baraka nyingi sana

Ulishawahi jiuliza ni kwanini wakristo waliokoka wengi wana hali ngumu za kiuchumi japokua biblia imewahidi baraka nyingi sana

Hao bado ni maskini huwezi kuwaita ni bahili kwa sababu hata wanachokipata wao wenyewe hakiwatoshi so hao wanabaki kuwa maskini.

Ninavyojua mimi bahili ni yule baada ya kufanya yote ya msingi (ya lazima) kinachobaki anakitunza hata itokee nini hakitoi,mtu mwenye uwezo wa kula vizuri kwa uhakika,watoto kwenda shule na kulala pazuri huwezi kumsema ana hali mbaya kiuchumi hao unaowajua wewe hawajafikia sifa za kuitwa wabahili.
Sasa we unabisha na kuna watu wanamaisha magumu na ni wabahili vibaya mno na wanafanya kazi kwa bidii zote

Mafanikio hayanauhusiano na ubahili bali yamefungwa kwenye kutatua changamoto, connection na michongo mafanikio ndo yapo huko na sio kua mbahili
 
Kwa kweli hata mimi sifurahi Mungu kutokuwepo.

Kwa sababu, Mungu angekuwepo, yeye ndiye angekuwa na mzigo wote.

Ila, Mungu hayupo, huo ndio ukweli.

Ukweli ni muhimu kuliko furaha yangu.
Unalazimisha ligi kwa lazima
Endelea na furaha yako sababu ndo maisha uliyochagua
 
Unalazimisha ligi kwa lazima
Endelea na furaha yako
Yani wewe unakuja na habari zako zisizothibitishika, zisizo mantiki, zisizo kichwa wala mguu.

Halafu mtu anakutaka uthibitishe hizo habari.

Halafu unamsema huyo mtu anayetaka uthibitisho kuwa ndiye analazimisha ligi?

Yani kujamba ujambe wewe, halafu mtu akikuambia hapa umejamba, ushuzi wako unachafua hewa, unamlaumu huyo mtu anayekuambia ukweli tu kwamba umejamba, unasema kakukosea heshima na anapenda ligi.

Wakati kujamba umejamba mwenyewe?

Kujamba ujambe wewe, lawama unipe mimi niliyesema tu hapa umejamba?
 
Jamani hee acheni uvivu , mungu hayupo chapeni kaxi
 
Yani wewe unakuja na habari zako zisizothibitishika, zisizo mantiki, zisizo kichwa wala mguu.

Halafu mtu anakutaka uthibitishe hizo habari.

Halafu unamsema huyo mtu anayetaka uthibitisho kuwa ndiye analazimisha ligi?

Yani kujamba ujambe wewe, halafu mtu akikuambia hapa umejamba, ushuzi wako unachafua hewa, unamlaumu huyo mtu anayekuambia ukweli tu kwamba umejamba, unasema kakukosea heshima na anapenda ligi.

Wakati kujamba umejamba mwenyewe?

Kujamba ujambe wewe, lawama unipe mimi niliyesema tu hapa umejamba?
Sawa unalingine ambalo umesahau
 
Sasa we unabisha na kuna watu wanamaisha magumu na ni wabahili vibaya mno na wanafanya kazi kwa bidii zote

Mafanikio hayanauhusiano na ubahili bali yamefungwa kwenye kutatua changamoto, connection na michongo mafanikio ndo yapo huko na sio kua mbahili
Wewe kama unataka kubishana sawa lakini kama unataka kuelewa utaelewa tu.

Unamuona bahakresa (kijamii kwa sababu huyu ndiye kama figured hapa kwetu) ukienda leo kumuomba Tsh 50,000/= hakupi siyo kwa sababu hana anazo lakini akikupa zitapungua na hujamzalishia hata mia (huyu ndiye tunaweza tukasema ni mbahili) siyo mimi na wewe tuna hela ya dagaa mfukoni na still haitoshi kununua nyanya tujiite wabahili sisi siyo wabahili sisi ni maskini!.

Sasa mfano huu uchukue hapo mtaani kwako yupo mtu ana nyumba yake safi,gari,watoto wanakula wanashiba then anakunyima wewe Tsh 2,000/= umekwama nauli huna huyu siyo maskini mwenzako huyu analinda alicho nacho na ndiye mwenye sifa ya kuitwa bahili.
 
Utajiri maana yake nini??
Bongo matajiri ni wachache, na wenye pesa ni wezi kupitia chamani.

Makonda ni billionaire sababu yuko kundini, lakini angesema atafute angekuwa bado mlalahoi, hata elimu ilimshinda lkn saiv ni msomi kwa support za kundi rangi ya forest.

Utajiri upo wazi kwa kila mtu, na njia ni mbili halali na haramu.
Unachagua na malipo ni hapa hapa duniani
 
walokole wa ulaya ni matajiri, tatizo sio ulokole, tatizo lipo kwao japo sio wote sababu hata matajiri wanao pia
 
Hawataki kujishughulisha, wanaamini ktk ujinga na matukio ya bahat nasibu(baraka), wengi wao wameaminishwa kuwa utajiri ni dhambi alafu hapa dunian ni wapitaji watapata utajiri huko katika mbingu za kusadikika.

Wengi wao ni wajinga wasiopenda kutumia akili zaidi ya hisia na porojo za wachungaji.

Wengi wao ni wanawake na baadhi ya wanaume mafukara ambao wameifanya dini kama comfort zone ya matatizo yao kwa kumsingizia shetan ndie msababishi.

Wengi wao wa hao walokole na wafia dini wanaibiwa na kuzidi kuwa mafukara sababu ya kuendekeza kutoa kila walichonacho kwa hayo majambazi yanayojiita wachungaji, manabii, mitume, kwa kuita hiyo michango ni sadaka.

Wengi wa hao walokole hawajui kanuni ya kufanikiwa ni kuattract Mafanikio kupitia juhudi binafsi na kuwasaidia wahitaji tu na sio kupeleka pesa zako kwa hayo majambazi(wachungaji).

Biblia pia imetumika kama dhana ya kuwaharibu akili kwa kuwaaminisha kuwa Utajiri ni mbaya,.

Hakuna mlokole tajiri ambaye kapata utajiri kwa kutumia hizo kanuni za kidini wala biblia, zaidi zaidi utagundua ni juhudi binafsi zisizohusiana na huo ulokole wao.

Yalivyo majinga, yanaweza kupata pesa kwa kusaidiwa na mtu au kupitia kazi fulani, baadae utayaona yakimshukuru Mungu au Mchungaji fulan kuwa madhabahu imewatendea mema, badala ya kuzishukuru juhudi zao wenyewe au kumshukuru mtu aliyewasaidia.

Hawa watu ni vilaza wakubwa na wagonjwa wa akili ambao kama wasipopata msaada wa kisaikolojia basi Taifa lina mzigo mkubwa sana wa umasikini hapo baadae.

Hawa watu ni wanafiki haswa.
 
Mtumishi unawezaje kumsaidia mtu anayepitia vita ya kiuchumi kwa upande wa kiroho

Msaada tafadhali
Fanya kazi kwa bidii hakuna vita vya kiroho acha kuamini ujinga.

Hamisha makazi hapo ulipo na utafute eneo sahihi la shughuri zako, jitenge na upunguze mazoea kwa baadhi ya watu, acha kuanika wazi siri zako na mipango ya maisha yako kwa watu.

Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe hakuna anae kuloga bali ujinga wako wa kuikosa Elimu ya mafanikio.
 
Fanya kazi kwa bidii hakuna vita vya kiroho acha kuamini ujinga.

Hamisha makazi hapo ulipo na utafute eneo sahihi la shughuri zako, jitenge na upunguze mazoea kwa baadhi ya watu, acha kuanika wazi siri zako na mipango ya maisha yako kwa watu.

Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe hakuna anae kuloga bali ujinga wako wa kuikosa Elimu ya mafanikio.
Maisha yangekua marahisi hivyo kama unavyotaka kuaminisha hakuna mtu angekua na shida hapa duniani
 
Hasiefanya Kazi na hasile . Unashinda kanisani unategemea Mungu atakushushia kapu la sadaka
Umemaliza mkuu.
Kanuni mojawapo ya Mungu kumbariki mtu ni pamoja na kazi za mikono yake.
 
Kama kinavyosema kichwa cha habari hili ni swali ambalo watu wengi wamekua wakijiuliza kwanini walokole wengi sio wote hali zao za kipato sio nzuri japokua kwenye biblia wameahidiwa baraka nyingi sana na Mungu na huku watu wanaoishi maisha yasiyompendeza Mungu wanamaisha mazuri na familia zao zinaishi vizuri

Unatakiwa uwe jasiri ili urithi ahadi za Mungu
Walokole wengi sana wanataka Mungu awaletee baraka mezani kwenye sahani huku kiuhalisia unatakiwa upiganie kisawa-sawa, baraka yeyote ile Mungu anayotaka kukupa inakipimo cha ujasiri ndani yake hutaipata kirahis rahisi lazima uwe jasiri ili uipate

Mungu hajibu maombi kama unavyotaka wewe
Wengi tunamuomba Mungu mahitaji mengi ukweli ni kwamba alishajibu kitambo ila sisi tunafeli sababu tunataka atujibu tunavyotaka ndo hapo tunafeli mfano unamuomba Mungu kuhusu ajira baada ya mda inatokea kazi ila mshahara ni laki 2 wengi wetu tunakataa ila Mungu anakua ameshakujibu tayari we unaona laki 2 ila Mungu anaona mamilioni na kutokujua hili wengi wetu tunafeli sana

Mungu anataka ufanikiwe kati-kati ya vurugu, kupingwa na kuchukiwa
Wengi wetu tunataka kufanikiwa kwenye comfort zote hiyo ndo changamoto kubwa inayotusumbua
Jambo la wewe kujua baraka ya Mungu kuja inaambatana na vurugu nyingi na magumu mfano Mungu anaweza kupa uongozi kwenye ngazi yeyote ile ila kuwa na uhakika utaibuka upinzani mkali ambao hukuutegemea kosa la wengi wetu tuna-quit ndo tunapokosea

Baraka yeyote ya ki-Mungu lazima iambatane na uchungu mkali sana mwanzoni
Mungu alimwambia eva utazaa kwa uchungu na akamwambia adamu utakula kwa uchungu; ukiangalia keyword hapo ni uchungu
Baraka yeyote kwa asilimia 99 lazima itaambatana kwa uchungu mwanzoni ndo uipate ni baraka chache sana zinaambatana na furaha mwanzoni

Unapokutana na changamoto yeyote usikimbilie kuitoa bali muombe Mungu iwe irrelevant (tafuta namna ya kuishi nayo) na baada ya hapa muombe tena Mungu akuonyeshe utajiri, heshima na utukufu wa Mungu uliopo ndani ya hiyo changamoto

Kosa kubwa sana wanalofanya watu ni kutumia nguvu kubwa kuondoa changamoto zinazowakabili jambo la wewe kufahamu changamoto yeyote ndani yake kuna utajiri, heshima na tukufu wa Mungu
Sasa unapokimbilia kuiondoa changamoto inayokukubali unapoteza hivyo vitu vitatu utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu

Ndo maana unaweza omba Mungu hitaji flani akakuletea changamoto au tatizo kumbe pasipokujua ndani ya hilo tatizo au changamoto kuna utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu
Na changamoto unayoiweza kuihimili hio sio changamoto

Kwako ni changamoto mpaka pale wewe binafsi imekushinda hio ndo changamoto ninayoongolea
Jibu ni Ndiyo, nimejiuliza

Na jibu lake ni kwamba hao wanaodai wameokoka no maskini kwasababu wanategemea kisichokuwepo.

Habari ya miungu ni hadithi zisizo na uhalisia totally.

Hakuna Mungu anayeendesha maisha katika ulimwengu huu.
 
Hasiefanya Kazi na hasile . Unashinda kanisani unategemea Mungu atakushushia kapu la sadaka
'HASIEFANYA KAZI NA HASILE'
Toba ya illahi !!! Jamani kizazi hiki !!! yaani kiswahili hakifundishwi tena mashuleni ? Kama ni mwanamume uliyeandika hivi basi Mungu akurehemu.Lakini kama wewe ni mtoto wa kike na unaandika hivi,basi hata uwe mzuri namna gani wa shepu na kila kitu,hata ukinipa bure sikutaki !!!
 
Back
Top Bottom