Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Kinachofanya watu wanajificha ni pale ambapo wewe kichwani una picha ya beyonce, unashangaa linatokea guluguja la maana... unaachaje kula kona? Mbaya zaidi ukute huko pm mmeshafika mbali hapo mmekutana kumalizia tuu..😂
Ndiyo maana mnatukimbia eeh, "kwani tulijiumba tuwe guluguja" mkuu😜😀 ni uumbaji tu tupendane kama tulivyo
 
Ishawai nitokea hali hii,kwa bahati mbaya yule mhusika anayependwa hakuamini
 
Habari za wakati huu wakuu.

Wakuu hadi naandika hapa binafsi huwa natokewa na hali hii for instance, kupitia mitandao ya kijamii mfano, hapa JF kupitia mada au comment za mtu unaweza jikuta unampenda mtu usiemfahamu.

Mara kadhaa hali hii huwatokea watu na ushahidi anao kila aliewahi kutokewa na hali hii. Note: sio lazima umpende kimapenzi japo inatokea kuna wengine anapenda tu japo aone comments zako au kila anapoingia online lazima apitie profile kwako au timeline yako.

Mbaya zaidi sasa, watu wanaogopana sana humu ndani kiasi kwamba hata ukivutiwa nae au amevutiwa na wewe unapata/anapata shida anaanzanje/unaanzaje kumuaminisha kuwa wewe ni mtu mwema kwake na huna nia ovu.

Mkijitahidi sana mtachat PM akiona niaje niaje anakupiga block kimasihara. Offcoz nafahamu wapo wengi wenye mgongano wa aina hii ya kuvutiwa na baadhi ya watu hususani humu ndani watatoa ushuhuda hapa.

Ninae mpenda akisoma hii thread atajijuwa. Na naomba usione soo mama njoo PM niambie nitakupokea kwa mikono miwili. Huwezi juwa huwenda mimi ndo fungu lako!

Au nasema uongo ndugu zangu?

[emoji23][emoji23][emoji23] Mtu alini PM tukachat tuka fall in love siku ya kuonana Daaaaaa[emoji174][emoji174][emoji174][emoji174] nlichoka mwili na roho sio kitu nilichokitarajia tukaachana hapo hapo
 
Tumblr_l_177804379477796.jpg

Mlimbwende yule, mbali na uzuri wake wa mwili, ana kila aina ya sifa njema na ni 99.99% wife material kabisa. We became very close friends na wasiri wakubwa...mpaka lilipotokea la kutokea. Hatukuwahi kuonana ila ungetuona ungedhani kuwa tumefahamiana kuanzia chekechea huko.

Huwa namuombea apate mume atakayemwelewa na kumpa ndoa ya amani na furaha...na bado naamini siku moja pengine nitapata bahati ya kumuona hata kama ni kwa sekunde moja!
 
Back
Top Bottom