Ni mara ya tatu sasa naenda kwenye duka la linalomilikiwa na serikali linalouza asali ila sijawahi kufanikiwa. Duka lipo karibia na mataa yaA Chang'ombe kama unaelekea mkuki house (dar es salaam).
Lile duka hawapokei cash malipo ni kwa control namba, lakini hata hiyo control namba mara zote husema network inasumbua....kila siku network ni shida??? sasa biashara wanafanya lini??? nakereka sana kufunga safari ndefu halafu nafika majibu ndio hayo, hivi wameshindwa hata kuuza kwa risiti??? Hadi nahisi labda huwa hawauzi je kuna mtu alishawahi kupata huduma pale???