Ulishawahi kuona malaika?

Ulishawahi kuona malaika?

Hello natafuta majibu hasa kwa wenye uzoefu, hebu tupe story

Ilikuwaje

Anaonekanaje

Alisema nini

Na mimi nataka kuona nifanye nini nipo kwenye research nataka kuuona ulimwengu mwingine sasa sitaki kukaa kizembe hebu nipeni uzoefu na mimi niwe miongoni mwa watu wanaotafuta ukweli kwa macho yangu

Ikiwa na wewe mpenda story stay tunned tuwasikilize marafiki zetu

Kuwa mcha Mungu haswa bila makando kando.

Isome mara kwa mara ayat kursi haswa nyakati za usiku mnene, utafanikiwa jambo lako.
 
Sasa wakiwaona watakwambia??? Na watoto wakiwaona malaika ili iweje??? Malaika ni wajumbe wa Mungu wa Biblia hutuma kwa kusudi maalamu! Sasa watoto wadogo watumiwe malaika kwa kusudi lipi hasa???? Hao ni watoto hatakuongea hawajui! Hata kutofautisha huyu ni binadamu huyu ni malaika hawajui! Haya ni mapokeo ya dini!!!
Ina maana mtoto hawatembeliwi na malaika?
 
Mimi pia am curious sana siku nione paradise kukoje Yesu yukoje Malaika niwaone hua natamani sana....ila nachoshukuru Mungu hua nafeel vitu kama ivo
Kama mimi
Ameen kesho utatupa mrejesho
Msijali ila naamini kama nikuona basi ni kwa mapenzi ya Mungu na kama sio pia ni kwamapenzi yake sitalalama hata nitashikuru tu
 
Kwa ufupi malaika ni wajumbe wa Mungu wa Biblia! Kuna malaika wasiokuwa na miili wanaokuja kwa mission maalum na malaika ambao ni Walokole (hapa naongelea walokole wa ukweli sio wale wanaojitafuta) kibiblia wanaitwa "malaika", katika kitabu cha Ufunuo "kwa malaika wa makanisa yale saba", hao malaika wanaotajwa ni "walokole"! Mungu wa Biblia anaweza kuwatumia walokole walioko hapa duniani kufanyakazi kama "malaika" wasiokuwa na miili!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣acha Mwamposa aendelee kutajirika tu.
 
Kuwa mcha Mungu haswa bila makando kando.

Isome mara kwa mara ayat kursi haswa nyakati za usiku mnene, utafanikiwa jambo lako.
Mimi ni mkristo na baba yangu alikuwa ni muislam ila ninajua Mungu wangu yupo tena anaongea na watu kama mimi ninavyoongea na wewe

Je unaijua sauti ya Mungu wako?
 
Malaika ni wengi na hujitokeza katika maumbo ya wanadamu na kusema na watu mara nyingi bila watu hao kufahamu.

Utakutana na mtu usiyemjua akakuongoza katika jambo na baadaye akatoweka na utakuja kushangaa yule alikuwa nani mbona hata sikumuuliza jina au kumtizama sana usoni? Hao huwa malaika mara nyingine.

Kuna wachache hutokewa na malaika live inapokuwa lazima sana.

Pia wengine hukutana na malaika katika ndoto.

Jua pia kuwa mashetani huja kwa watu kwa njia hizo hizo.

Nikwenda Nairobi miaka mingi iliyopita kutafuta chuo. Nilifuatilia registration lakini sikupata. Wakati nipo jijini mle nilichujua hosteli kama kilometer 2 kutoka chuoni. Lakini ilinibidi kuhama hostel hizo baada ya kukosa usajili ili nikae nyumba ya wageni usiku ule kabla ya kurejea Tanzania.

Nilighadhbika sana mchana ule hadi kukaribia usiku. Nilisali sana kumwomba Mungu anisaidie niwe salama. Wakati natoka getini nilikuwa nimebeba shehena ya mabegi yangu kichwani narudi nyumba ya wageni na ilikuwa kuelekea saa 1 usiku.

Nairobi ya 2003 ilikuwa na uhalifu wa kutisha. Ghafla ilikuja tax nyuma yangu na mtu mmoja nisiyemfahamu alifungua mlango na kuniambia unafika wapi, nikupeleke? Unajua wakenya sio wakarimu kama watanzania tena ndani ya nairobi na tena kwa mtu asiyekujua ndio usiseme.

Bila kuwa na hofu nipanda tax na kumwambia nilikokuwa nakwenda. Mtu yule alinipeleka hadi hatelini na kuniacha pale huku akinipa namba ya simu na hakunichaji chochote! Kenya tena katikati ya Nairobi?!!! Alikuwa mkarimu ajabu!

Ajabu ni kwamba siku mark sura yake na hata ile namba ya simu sikujua niliiweka wapi!

Niliporudi Tanzania niliwaadithia ndugu zangu wanaojua Nairobi na walitetemeka sana kusikia nimepanda tax Nairobi ya mtu nisiyemjua!

Baadaye nilipata ufunuo kuwa hakuwa mtu wa kawaida ila malaika! Bwana Mungu asfiwe sana!
Chai
 
Ndio. Alinitokea ili kutoa kiburi changu.
Shuleni nilikuwa naonekana kipanga wa somo la Physics, nilijiona kama Mungu duniani.

Sasa usiku wa manane, nikamuona Malaika katika ndoto anawaka sana, nikapelekwa ubaoni, akaandika swali la topic la Heat and Thermodynamics, nikaliangalia nikasema lishaisha, akacheka, aisee nikachukua chaki, nikasolve , aisee nilimaliza ubao bila jibu, baadaye nikaamua kukiri wazi hapa sijui, Malaika akasmile , akachukua chaki akasolve kipande kichache tu na jibu akaliandika, akili yangu ikafunguka na kuona jibu ndo hilo.

Aisee nikaacha kuwa na kiburi kabisa na hata sasa sina kiburi tena.
Bongo muvi
 
Kuna siku nlikua ofisin gafla nkapitiwa na usingizi mzito sana nkawa naota mtu anataka kunikata kucha ya mguu wa kushoto nkawa nakemea nkawa nafumbua macho nashindwa kama kitu kinanikandamiza nilale nikataja Baba wa Mianga aiseeee Yan nlskia kishindo kikubwa as if transformer imeburst ule mlio mara 10 yake hapohapo Ile hali ikaachia nikajua huyo alikua Mungu katuma nguvu zake
 
Sasa wakiwaona watakwambia??? Na watoto wakiwaona malaika ili iweje??? Malaika ni wajumbe wa Mungu wa Biblia hutuma kwa kusudi maalamu! Sasa watoto wadogo watumiwe malaika kwa kusudi lipi hasa???? Hao ni watoto hatakuongea hawajui! Hata kutofautisha huyu ni binadamu huyu ni malaika hawajui! Haya ni mapokeo ya dini!!!
Kwanini asiseme ,mbona vitu vingi Tu wakiviona wanavisema
 
Mara ya pili ikatokea pale shuleni nilipoamua kuwa Atheist, nikasema kwa mdomo wangu Mungu hayupo na Yesu hayupo, Sayansi ndo imechukua nafasi ya Mungu.

Tena usiku wa manane nikaota ndoto, nilikuwa kwenye hatari ya watu waovu baada ya kujua siri zao , akatokea Malaika akanichukua na kunipeleka sehemu ya paradiso, nikakaa nje, sikuruhusiwa kuingia ndani, sasa mageti yakafunguliwa, nikamuona mtu akismile, akiwa na ndevu, Yesu ambaye nilisema hayupo. Aisee nilipigwa na butwaa.
Bongo muvi imekuharibu.
 
Kuna siku nlikua ofisin gafla nkapitiwa na usingizi mzito sana nkawa naota mtu anataka kunikata kucha ya mguu wa kushoto nkawa nakemea nkawa nafumbua macho nashindwa kama kitu kinanikandamiza nilale nikataja Baba wa Mianga aiseeee Yan nlskia kishindo kikubwa as if transformer imeburst ule mlio mara 10 yake hapohapo Ile hali ikaachia nikajua huyo alikua Mungu katuma nguvu zake
Amen Mungu wa mianga unaweza toa maelezo
 
Back
Top Bottom