Hii imekaaje wakuu. Mpaka leo nazeeka sijawahi kuona au kusikia mtu maskini yaani mwenye kipato duni na pengine mwenye Elimu duni akihangaishwa na shida hizi za kukosa nguvu za kiume.
Hawa wenzetu wanatumia mbinu gani au ndio vile Mungu hakunyimi vyote?
Vyakula vya sisi masikini na tusio na elimu na life style yetu:
Maboga,
Viazi vitamu na viazi vikuu,
Ndizi,
Ugali wa dona (hatuna hela ya kukoboa mahindi)
Mbegu za matango na maboga tunaanika Kisha tunatengeneza tui la kuungia mboga I we mzito(hatuna hela ya kununulia royco mchuzi mix),
Matumizi yetu ya sukari ni madogo maana sukari Bei juu(hatuwezi kumudu chai na juice kila siku),
alafu,Hatulipwi mshahara,tunapaswa tutoke rukatafute hivyo nguvu zetu ndiyo kula yetu. Kwetu kilimo Ni UTI wa mgongo,hatutoki vitambi kwa kazi ngumu za kilimo.
Most of the time tunakula OMAD(One meal a day) tukizidi Sana ni 2MAD (two meal a day).
Vyakula vyenu wenye elimu na exposure ya maisha:
Chipsi zege na kuku wa kizungu +mayonaizi,
Mnaingia MacDonald kula burger na pizza,
Vyakula vyenu ni sukari. Sukari ambayo ikiingia mwilini haina matumizi maana hamfanyi kazi ngumu,inaishia kuwaletea vitambi ili suti zenu ziwakae vizuri mzidi kupendeza,
Muda wowote mna uhakika wa kula,kwenu msosi siyo tatizo ndiyo maana mnanenepa na kuwa na nuru,
Hamna kazi ngumu,hamfanyi mazoezi,mnatumia magari muda wote.
Mkuu,Kuna kitu unaweza kujifunza kupitia hiyo life style ya Hawa watu wawili. Hakuna uchawi Wala kupendelewa na Mungu.