Ulishawahi kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto/watoto? Hii inahitaji hekima na busara nyingi sana

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za muda huu waungwana wa jamiiforums​

Kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto hata mmoja, kunahitaji hekima na busara nyingi sana.

Hakuna ndoa yoyote hapa duniani ambayo ni rahisi kuipatanisha kwa maana kila ndoa ina changamoto zake, lakini ukweli wa mambo ni kwamba ndoa zisizo na watoto ni ngumu sana kuzipatanisha (kukitokea changamoto ya ziada) kuliko zile zenye watoto wengi au walau mtoto mmoja.

Kupatanisha ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 7 bila mtoto alafu iibuke changamoto nyingine mpya (ambayo inaweza kuwa ya kawaida katika ndoa zote hata zile zenye watoto) kama vile baba kuchelewa kurudi kazini, inahitaji hekima na busara ya hali ya juu sana.

Kwanini ninasema hekima kubwa inahitajika katika kupatanisha changamoto za ziada katika ndoa isiyo na watoto? Kwa utafiti mdogo nilioufanya kwa miaka kadhaa nyuma mpaka sasa nimegundua ya kwamba, ndugu na marafiki wengi wanaoitwa kwenda kusikiliza changamoto za ndoa yoyote ile, hukimbilia kwa watoto kama ngao ya kutaka baba na mama (wanandoa) wasitengane bali waendelee kuishi.

Hahahahaaaa unacheka? Unafikiri ninatania mkuu. This is very true my friend. Watu wengi wanaokwenda katika vikao hivi vya upatanishi hukimbilia kuwaambia wanandoa ya kwamba "Sasa Infantry Soldier na Bushmamy mkiachana leo hii, hawa watoto wenu watano wataishi vipi?"

"Sawa nyie ni watu wazima mnaweza mkawa na chuki zenu, lakini vp kuhusu future ya watoto jamani Soldier? Ina maana unataka kutengana na Bushmammy kisa tu chai ya rangi ameiunga kwa nazi? Labda hayo ndio mapishi yao huko Tanga mvumilie tu mzazi mwenzio atabadilika taratibu"
Hahahahaaaa, I'm joking, lakini bila shaka umepata mantiki yangu?

Watoto/Mtoto hutumiwa kama ngao ya kuzifanya ndoa nyingi ziendelee kuwa hai lakini licha ya ukweli kwamba baba na mama kila mmoja anakuwa analala chumba chake huko ndani au wanalala chumba kimoja lakini mwingine anatandika godoro chini.

Kama mtoto anatumika kama ngao kwenye ndoa zilizobahatika kupata walau mmoja, sasa zile ambazo zimekaa miaka 7 hazina kabisa unafanyaje kusuluhisha changamoto ya zaida inapojitokeza?

Ni ngumu sana ndugu zangu. Yaaani ni ngumu kweli kweli. Inahitaji watu wenye hekima na busara level ya ndugu zangu Kiranga na Mshana Jr ndio wanaoweza kunusuru ndoa za namna hii. vinginevyo labda Mungu pekee ndiye aingilie kati.

OMBI LANGU: Mungu tunakuomba uendelee kuwapa moyo wa uvumilivu na subira wanandoa wote ambao mpaka sasa hawajapata watoto/mtoto katika maisha yao na waamini ipo siku wewe kama muweza wa yote utawafungulia milango ya baraka na kuwapa hitaji hilo la mioyo yao kama ulivyomfanyia Sarah, mke wa Ibrahim. Amen.

Maoni ya wadau;
==========
==========
Nilipitia hili yaani ilikua tukikwazana kidogo mi naanza kulia najua kanikwaza sababu Sina mtoto du!! Yale maisha....Asante Mungu kwa kunifuta machozi aisee.
==========
==========
==========
Katika vitu ambavyo siwezi na wala sitokuja weza, Ni kuvumilia kua na mtu kisa malezi ya mtoto. Pamoja na kutambua umuhimu wa wazazi wote, ila siwezi nikariski Furaha yangu
==========
==========

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Nilipitia hili yan ilikua tukikwazana kidogo mi naanza kulia najua kanikwaza sababu Sina mtoto du!! Yale maisha....Asante Mungu kwa kunifuta machozi aisee
Nimeumia kama nakufahamu, kweli kukosa mtoto ni huzuni, kama ni kipimo ni kigumu asee acheni kabisa
 
Nilipitia hili yan ilikua tukikwazana kidogo mi naanza kulia najua kanikwaza sababu Sina mtoto du!! Yale maisha....Asante Mungu kwa kunifuta machozi aisee
Nimeitwa sana katika ndoa za namna hii my dada
 
Ndio maana kwa wenzetu wazungu wanapokua kwenye mahusiano au ndoa, hua wanachukua muda mrefu sana mpaka kuamua kupata watoto. Lengo ni kwamba endapo ikitokea wakashindwana hapo katikati wasije wakajikuta wanaendelea kulazimika kukaa pamoja kisa tu kuna watoto.

Kwa huku kwetu ndoa nyingi zinashikiliwa na watoto kwa maana ya kwamba ndoa ilishavunjika zamani ila watu wanalazimika kukaa pamoja ili kulea watoto.
 
Nachojua mimi siwezi nikauza furaha yangu kwa sababu ya kitu chochote...

Hata tukiwa na watoto 50 pale ambapo kichwni kwangu na uhakika kuna mtu ana mess na furaha yangu its over..

Hamna kitu kitanikwamisha,watoto tutahudumia kila mtu akiwa na hamsini Zake.Na kwanza hawatakuwa watoto wa kwanza kupitia changamoto ya wazazi wake kuachana.Akikuwa akianza kuwa na mpenzi ataelewa kuna kuachana kwenye mapenzi na si jambo la ajabu.Akikuwa ataelewa baba na mama walishindwana ..

Kitu unachopaswa kuniambia ni kuhudumia watoto wangu ndoa ikifa hicho nitakuelewa ila sio niishi na mtu anacheza na amani ya moyo wangu sijawahi kufanya huo upuuzi na Mungu anisaidie nisiwahi kufanya huo upuuzi.Msingi mzima wa mimi kutafuta hela ni ili niwe na freedom hasa ya kuwa na furaha.

Nakupenda sawa nakubali ila ukicheza na furaha yangu nakuwaga mtu mwingine kabisaaa kuanzia sura hadi maamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…