ni ngumu
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 4,292
- 7,197
Hii misimamo ya hivi huwa imekaa kibinafsi sana ingawa n mizuri kwa muhusika
Binafsi kwangu furaha ya viumbe nilowaleta duniani naipa kipaombele sana .kuna namna watoto walolelewa na wazazi wote wawili hujengeka,labda itokee mzazi mmoja ametangulia mbele za haki...familia ni nguzo aise hasa kwa walio na hofu ya Mungu
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Yah ni ya kibinfsi sababu usipokuwa mbinafsi na furaha yako kitakachotokea ni kwenda kuwaamishia stress zako watoto..
Umesalitiwa na mwenzako ila hasira zako unaendea kumalizia kwa mtoto aliyefanana na mumeo.
Kitu kidogo unapiga mtoto mpk unategua mguu ukiulizwa nina stress..
Sijui km unajua kulea ni kazi?na hapa sizungumzii kulisha mtoto ambaye kwa mwezi ht kilo 10 hawezi maliza.Nazungumzia ukomavu wa kihisia wakulea mtoto na mtoto akajifunza kitu kutoka kwa baba au mama yake,mtoto akakua akiwa na haiba nzuri...
Huwezi kuniambia nipo busy kulea mtoto wakati mama yao ameshanipa kidonda ambacho siwezi kupona nikiwa nae.Kila mtu ana kiwango chake cha kuvumilia changamoto,changu kikifika watoto hawatasaidia kitu.
Tupo tunakula baba nimenuna au tunaangalia tv siongei kitu na mke wangu sasa unawafundisha nini watoto yaani kipi hasa wanachojifunza kwa kuwa na wazazi wawili????Watoto wanahitaji kuona baba na mama wanafuraha,wanacheza mziki pamoja mbele yao,wanapiga story huku wanacheka kwa furaha.Hiko ndo watoto wanataka kuona na sio sura ya baba yenye hasira mda wote au mama mwenye majonzi mda wote.Mnawatisha tu na kuona maisha ni mabaya.
Tatizo langu sio ubinafsi tatizo langu ni i am very genuine nitakuvumilia nachoweza kukuvumilia ukivuka mstari sitawaza mara mbili.Naacha familia hata ya watoto 50 naenda ku enjoy maisha yangu tutakutana kwenye matunzo.