Ulishawahi kupatanisha changamoto ya ziada katika ndoa ambayo haina mtoto/watoto? Hii inahitaji hekima na busara nyingi sana

Kiukweli sijawahi fanikiwa zaidi ya kushauri watu watengane
Sawa mkuu. Kutengana ni lazima iwe option of last resort kama njia zote za upatanishi zimeshindikana. Watu wasipotengana inaweza kuzaa mauti baina yao.
 
Nilipitia hili yan ilikua tukikwazana kidogo mi naanza kulia najua kanikwaza sababu Sina mtoto du!! Yale maisha....Asante Mungu kwa kunifuta machozi aisee
Pole sana. Ulifanikiwa baada ya miaka mingapi ndoani dada yangu?

Tunapitia hali hii kwa sasa na wife, hata miaka miwili hatujafikisha ila naona pepo la kukata tamaa limeshatuteka. Ni full migogoro tu
 
Pole sana. Ulifanikiwa baada ya miaka mingapi ndoani dada yangu?

Tunapitia hali hii kwa sasa na wife, hata miaka miwili hatujafikisha ila naona pepo la kukata tamaa limeshatuteka. Ni full migogoro tu

Hujaniuliza mm ila naomba nikujibu kwa experience yangu..kua na subira huku ukimuomba Mungu I mean it sababu nina ndugu yangu alikaa miaka8 bila mtoto ilibakia kidogo watengane mambo yalikua ni mengi mno huwez amini mwaka wa 9 mkewe akaconcieve akapata mapacha3 wawili wa kiume 1 wa kike!

Jirani yetu mwanae alioa 2017...muda huu nnavyotype mkewe ndio ana mimba ya mwezi mmoja.

Ni ngumu kukubali ila wakati wa Mungu ni wakati sahihi mno...Mungu hua hawai wala hachelewi boss.
 
Ubarikiwe sana. Umenipa faraja na somo kwa pamoja.
 
Kwa jinsi ndoa zilivyo na ups and downs nyingi. Kama hujaolewa nakushauri usijiingize kwenye ndoa kabisa kuliko kuingia na kutoka.
 
Pole sana. Ulifanikiwa baada ya miaka mingapi ndoani dada yangu?

Tunapitia hali hii kwa sasa na wife, hata miaka miwili hatujafikisha ila naona pepo la kukata tamaa limeshatuteka. Ni full migogoro tu
Msikate tamaa aisee miaka 4
 
Hii misimamo ya hivi huwa imekaa kibinafsi sana ingawa n mizuri kwa muhusika
Binafsi kwangu furaha ya viumbe nilowaleta duniani naipa kipaombele sana .kuna namna watoto walolelewa na wazazi wote wawili hujengeka,labda itokee mzazi mmoja ametangulia mbele za haki...familia ni nguzo aise hasa kwa walio na hofu ya Mungu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…