Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
 
Kuoa aoe yeye,tabu nipate mimi! Yeye afanye yake nami nifanye yangu.
Kuna siku nilijikuta niko kwenye kundi la WhatsApp la harsi ya jamaa yangu mmoja,wakati nilivyoona tu hivyo,nikajiondoa. Sasa kuna jamaa yetu mmoja akanipigia akanihoji kwa nini nimejiondoa.

Sasa kwani ni kosa?
Akajibu kuwa tumuunge mkono jamaa.
Nilishangaa sana,yaani kuoa siku hizi ni emergency mpaka mtu aombe kuungwa mkono?

Nilimuambia hata mimi niko ktk mchakato huo na keshokutwa ndio siku yenyewe ila kwakuwa sioi mke wa wengi na kwa ajili yangu ni kimyakimya tu.

Km kuna jambo niko tayari kupondwa mawe nife na sito lifanya ni kutoa mchango unao husu sherehe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie nilishindwa kumtunza vitu alivyotarajia.
Na sikuhudhuria, nlimuagiza mtu aniwakilishee.

Tulinuniana kwa muda, baadae yeye mwenyewe akajirudisha.
Noma sana😅😅
 
Mkuu, kuoa siyo ugonjwa au msiba useme ni emergency. Kuoa au kuolewa unapata nafasi ya kuweka ratiba na mipango. Kwa hiyo ufanye sherehe usifanye ni mipango yako tu.
Sasa upange mipango wewe halafu mtekelezaji wa mipango niwe mimi ambaye siyo mnufaika?
Mimi wanitenge dunia nzima lkn huu upuuzi sitotekeleza hata kidogo.
Ukileft group unaonekana kama umejifuta kwenye urafiki wenu😂😂
 
Mkuu,kuoa siyo ugonjwa au msiba useme ni emergency. Kuoa au kuolewa unapata nafasi ya kuweka ratiba na mipango.
Kwa hiyo ufanye sherehe usifanye ni mipango yako tu.

Sasa upange mipango wew halafu mtekelezaji wa mipango niwe mimi ambaye siyo mnufaika?
Mimi wanitenge dunia nzima lkn huu upuuzi sitotekeleza hata kidogo.
Nimeenisha mtu akijitoa kwenye hayo magroup watu huchukulia kama kajitoa kwenye undugu au urafiki. Yaani jambo linakuuzwa kuwa kubwa kisa tu umejitoa kwenye grup
 
Kuna mwamba tulipotezana zaidi ya miaka kumi nyuma, siku amenitafuta, akajitambulisha nikasema poa nafurahi kukusikia tena Mdau. Kesho yake akanipigia kunieleza Jambo lake la kuoa na kuniomba Mchango.

Kwa kweli sikutilia uzito ombi lake nikampotezea pamoja na kunipigia simu pamoja na sms za mara kwa mara kunikumbusha mchango., Akafanya shughuli yake, akamaliza. Leo ni mwaka wa nne toka amemaliza Jambo lake, na hajawahi kunitafuta tena japo kunisalimu Ndugu yake.
 
Ndivyo walivyo.

MSAADA SIYO HAKI YAKO HIVYO UKIKOSA USI LALAMIKE.
 
Wakuu,

Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
Binafsi Kuna marafiki wameacha kuwasiliana na Mimi kwa sababu ya kutonichangia kwenye harusi yangu

Mimi nilikuwa mchangiaji mzuri Sana kwenye harusi za watu, toka nipo chuo nilikuwa nakubali nijibane pesa ya boom ili nitoe angalau 30,000 ya mchango

Mara nyingi nilikuwa natoa 30k Hadi 50k

Kibaya zaidi, kwenye ndoa yangu washikaji wamevunga kabisa, ila wengi wao walisema watatoa mwisho wa mwezi maana harusi ilikuwa mwanzo wa mwezi.

Japo wote Wana kazi za uhakika mwisho wa mwezi, sikushangazwa na kutokutoa bali nilishangazwa kwamba hawakunitafuta kabisa hata ile wiki ya Kwanza ya ndoa, Hadi Sasa

na mimi nimeamua rasmi, sitachangia tena marafiki sherehe yoyote, tena kwa wale niliowachangia halafu hata kusalimia hawataki sitochanga kwa tukio lolote
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nilitoa kwa uwezo wangu ulipoishia, kumbe yeye alitaka zaidi, kheeh nawezaa wapii mie.

Na venye sikuhudhuria aliona nimemdharau sana, kumbe nlikua na dharura.
Huwa hawaelewi kabisa, na hapo unakuta hata umeelezea sababu ila shingo inashupazwa kuwa umedhamiria
 
Miye nashangaa sana hivi unajua sherehe ya harusi wanufaika ni mc, watu wa mapambo, watu wa chakula, na watu watu wa vinywaji na ujinga mwingine MC ndio anamua mkae ukumbini mda gani mc akiwa mhuni masaa matatu anamaliza sherehe yani mmekaa vikao miezi mitatu mc anawaweka ukumbini masaa matatu

Sikia wewe bibi harusi mtalajiwa na baba harusi kafunge ndoa rudi nyumbani kula chakula na wana ndugu na jamaa vizuri , jioni amua sasa unasherekea hapo hapo nyumbani au nje ya nyumbani kama nyumbani funga mziki mzuri dj mzuri kiamshe kuleni hapo wa kunywa wanywe uone itakavyochangamka kwanza hakuna limit ya mda mnajimwaga mnavyoweza.
 
Back
Top Bottom