Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.
Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.
Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!
Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?