Sijawahi kutongoza mwanamke yeyote ninaemjua bwana wake, pia sijawahi kumtongoza mwanamke ninaetambua kabisa ni mke wa mtu.
Wanawake wasimbe wapo wengi sana, lakini kwanini ufanye mapenzi na mtu unaetambua kabisa ni mke wa mtu na kila mara anatoka kwa mwanamme kama wewe kipindi anakuja kwako?
Inafikirisha sana.
Wakati fulani sisi wanaume ndio chanzo cha wake zetu kuchepuka.
Mwanaume unaondoka nyumbani kwenda kulala kwa mchepuko. Unamwacha mkeo na watoto nyumbani. Hujui wamekula au la. Huachi mahitaji wala hela ya mahitaji.
Mkeo kawa kama siyo mke wa mtu. Anajipigania yeye na watoto. Unategemea nini?
Akikwama lazima atafute mbinu mbadala. Na silaha pekee aliyonayo mwanamke ni kidudu chake. Lazima ataangukia mikononi mwa mbaharia ili wamsaidie kutatua shida zake.
Nimeyaona mengi na mengine nimehusika. Mwanamke umemsaidia, anaamua kujikabidhi kama shukrani na hata kuhitaji msaada zaidi.
Lakini ukumbuke kuwa na yeye ni binadamu. Unachokifuata huko kwa mchepuko na yeye anacho na kinahitaji kuhudumiwa. Nani amhudumie ikiwa wewe umemtelekeza? Ndiyo maana wengine husema WANANDOA WENGI HUPATA RAHA YA NDOA NJE YA NDOA. Huenda sababu ni
1. Wanaume kutotenga muda wa kutosha kuhudumia ndoa zao. Wako busy na majukumu.
2. Baadhi yetu tukishapewa utamu na mchepuko, nyumbani tunalipua kazi. Mama hashibi, anaamua atafute pa kumalizia hamu.
3. Kitendo cha mwanaume kulala nje ya nyumba yako tena mtaa wa pili tu, husababisha mke kuchukia na kuona kama amedharauliwa. Kifuatacho atatafuta kulipiza.
Ushauri wangu, wanaume tujenge tabia ya kuzungumza na wake zetu kuhusu mapungufu ya chumbani na kutafuta namna ya kuyapunguza ili kuwafanya wake zetu kufurahia ndoa zao. Itasaidia sana kukwepa vishawishi.
Pia tuhudumia familia zetu kikamilifu na kwa upendo. Mama ajue kama analala njaa ni kwa vile mumewe hana kitu kabisa.
Nina mengi, muda hautoshi.