The druid
JF-Expert Member
- Jun 2, 2020
- 507
- 627
Man, you are a good writerNilihamia katika mji wa watu nikiwa pekeyangu. Familia niliiacha nilikotoka.
Sababu za kuiacha familia huko ni mapambano ya maisha. Tulikuwa na kabiashara, isingewezekana kuhama nako harakaharaka kabla ya kujifunza mazingira mapya.
Kwa kuwa sikuwa ninapika, nilikuwa ninakula kwa mamantilie. Jirani na mamantilie palikuwa na kibanda cha mpesa. Mmiliki ni familia, mhudumu ni mama.
Nilikuwa na mazoea kwenda kupata huduma kutuma na kutoa.
Siku moja nilimkuta yule mama amekaa chini ndani. Nilipofika alijitahidi kuficha lakini niligundua kuwa alikuwa analia. Nilimwuliza kulikoni akajifanya kushangaa.
Mazoea ya kufika pale yaiendelea. Kuna siku nilimwomba namba ili nikitaka huduma niipate hata bila kufika. Alinipa japo kwa kusitasita.
Siku ya siku, nilimpigia. Alipokea, nikagundua sauti haiko sawa. Alikuwa akilia. Baada ya kupata huduma, nilijaribu kumbembeleza anambie ana tatizo gani. Alifunguka baada ya kama kumbembeleza mwezi mzima hivi.
Nilimpa concealing karibu mwezi kwa kuongea naye kwa vipindi tukiongea kwa kama dakika kumi hivi.
Alianza kunielewa na sasa yeye ndiye alikuwa anatuma text akinambia amepata amani na anasonga mbele na maisha yake. Mapenzi yake ameelekeza kwa watoto na mume si tatizo tena kwake.
Mumewe alikuwa anaweza aondoke nyumbani wiki zima anakaa kwa mwanamke mwingine katika mtaa huohuo.
Siku moja nikamwomba anisitiri nina ugwadu. Alinambia hayakuwa makubaliano yetu. Nilikubaliana naye. Nikamsisitiza kwa kumkumbusha mara kwa mara. Baada ya kama miezi 15 hivi aliingia king.
Kosa langu: nilimjali sana. Hakuna alichoomba nikamkatalia. Nilimpa hata asichoomba. Akazama na kuzama. Siri sirini.
Nina miaka mitatu sasa na mke wa mtu.
Ninafikiria kuacha kutokana na watoto wake ni wakubwa sasa, si vema wakagundua mama yao anachepuka. Pia mume wake ni kama ameanza kurejea ngamiani.
Sent using Jamii Forums mobile app