Ulishawahi kuulizwa swali gani na mwanao ukakosa jibu?

A Smart Question
 
A Smart Question
Anachoshangaa zaidi kama mtoto akizaliwa anafwata kabila kwa baba mbona bibi yake mzaa mama ni mbena kama mama yake halafu bibi mzaa baba ni mchaga kama baba yake kwanini nao wasingekuwa na makabila tofauti mbona wazazi wake tunafanana makabila na mama zetu kwanini yeye tuu ndio awe wa tofauti.

Kila nikijaribu kumuelewesha naona nazidi kumchanganya tuuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hivi gari linauzwa shilingi ngapi ambayo wewe huna? Hapo nimemfuata shule tunarudi nyumbani kwa mguu na rafiki zake wanatupita njiani wakiwa kwenye magari ya kwao
Hili swali nadhani karibia kila mzazi amewahi kuulizwa. Mvua ilikuwa inanyesha nikaenda kumfwata na mwamvuli tukapishana na ndugu yetu amewabeba wanae kwenye gari akaniuliza " mama kwann usinunue na wewe gari uwe unanifwata tusilowe na mvua???" Nikamwambia tuu unavyosali niombee mama yako siku nitanunua tuu
 
Mbona mama akiwa anabadilisha nguo unatufukuza alafu wewe hutoki!!??


Na Mimi nikikuwa baba alafu wewe mtoto ntakukomesha


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ’§
 
mtoto wa miaka 5 aende kuuliza YouTube?
Kingine kitakachokufanya uendelee kusema ni chai isiyo na sukari ni maswali yote aliuliza kwa kiingereza bado anajifunza kiswahili.

Nimemfundisha chochote asichoelewa anauliza Gemini au Youtube majibu yote yapo hapo.
 
Kingine kitakachokufanya uendelee kusema ni chai isiyo na sukari ni maswali yote aliuliza kwa kiingereza bado anajifunza kiswahili.

Nimemfundisha chochote asichoelewa anauliza Gemini au Youtube majibu yote yapo hapo.
hivi unamjua mtoto wa miaka 5 lakini?

umebaki kutuwashia moto tu tuuzunguke
 
hivi unamjua mtoto wa miaka 5 lakini?

umebaki kutuwashia moto tu tuuzunguke
Mkuu unaishi wapi kwani ? Mwanangu wa miaka 5 anajua kusoma, anatumia simu anatupigia wazazi wake simu tunapokuwa mbali, anakaa na kaka yake mdogo na kumlisha, anacheza game zingine mimi nahitaji siku kadhaa kuzimaster.....

Na nimeona watoto wanaofanya vingi zaidi ya huyu.

Mtoto wa jirani yangu ana miaka 10 anatangeneza logos....anawauzia watu na anapiga pesa.
 
Sasa mbona 80% wote humu mnaulizwa maswali yenye uelekeo wa mambo ya kukulana 🀣🀣
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜…πŸ˜… hizi kamba zinatosha mkuu

anawauzia watu na anapiga pesa au sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…