Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?


Pale Morogoro Bilibi ilikuwa inapiga kwenye kumbi za starahe, siyo majumbani, na DJ wake mkuu (nimesahau jina lake) alikuwa na undugu na DJ wa Clouds (au Mawingu) ya Dar es Salaam ambaye nadhani alikuwa ni Joseph Kusaga.

Yule DJ mkuu wa Bilibi alikuwa anaitwa Justin; alikuwa anatoa nyimbo kali kutoka Clouds (Mawingu) pale Dar na kuzipeleka Morogororo.
 
Vile vile mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini kulikuwa na kundi la muziki la wataliano weusi lilijulikana kama "Black Box" lilitoa nyimbo za spidi kubwa sana wakiimba kwa lafudhi ya kimarekani nao wakazaniwa kuwa ni wamarekani weusi lakini wapi. Kati ya nyimbo zao zilzohit sana ni "Ride on Time" na "Everybody Everybody." Miaka hiyo huo wimbo wa "Everybody Everybody" ulikuwa unatumiwa sana kuwakaribisha maharusi kwenye kumbi hapa Dar. Kitu cha Kuchekesha ni kuwa huyo msicha unayemuona kwenye vdeo akiimba, jina lake ni Katrin Quinol. Yeye siye alieimba wimbo huo ila alikuwa akiigiza (lip-sync) tu wakati wa kushuti video, lakini ndiye aliyepata sifa sana.


View: https://www.youtube.com/watch?v=M0quXl_od3g


View: https://www.youtube.com/watch?v=18N2k1TBBRE
 
Wimbo huu ulitoka nikiwa Primary School; tafsiri yake kamili siijui hadi kufikia kuruka ukuta. Hebu toa tasfri ya kwako.

Bendi ilikuwa inaitwa Vijana jazz ilikuwa inamilikiwa na TANU Youth League ikiongozwa na Hemedi Maneti aliyefariki mwaka 1990 kwa kinachosemekana ni ukimwi.


View: https://www.youtube.com/watch?v=aaRGixRNVqA
 
Listening to new day by Celine Dion, damn she had a magic voice.

My play list, *
new day
My heart will go on .
Fool again
Queen of my heart
 
Listening to new day by Celine Dion, damn she had a magic voice.

My play list, *
new day
My heart will go on .
Fool again
Queen of my heart
Selina alikuwa mimbaji mzuri sana. Alitoa nyimbo nyingi sana nzuri lakini wimbo nilioupenda na hata yeye mwenye ailiwahi kukiri kuwa ndio wimbo wake mzuri na allishindwa kuuimba kwa mara ya pili kwa vile ulikuwa unatumia octaves tatu ni ule wa "Its all coming back to me Now"


View: https://www.youtube.com/watch?v=j8fHNdrZTSI
 
Octaves ndio nini,kama hutojali? Katika nyimbo za Celine mwenyewe naupenda huu sana.
 
Octaves ndio nini,kama hutojali? Katika nyimbo za Celine mwenyewe naupenda huu sana.
Hili ni swali gumu sana. Ila elewa kuwa kwenye muziki sauti zimepangwa hivi "do, re, mi, fa, so, la, ti, do" kukamilisha octave moja. Sasa wimbo huo una hizo octaves tatu kuanzia sauti ya chini sana hadi ile ya juu sana. Niliwahi kuanzisha thread hapa kuelezea misingi ya utunzi wa muziki ila nikakosa muda wa kuimaintain hata sijui thread hiyo iko wapi siku hizi.
 

World cup ya mwaka 1994, kila mechi zilipoisha ulikuwa unapigwa!! Kila niusikiapo kumbukumbu ile hunijia.

Kabla ya mechi watu wamejaa uani kwetu kuangalia mpira kwa upendo mkubwa, wengine walisafiri umbali mrefu kuja kuangalia mpira na hata hatuwajui, kwangu mie ilikuwa ni upendo wa hali ya juu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…